Umoja wa vyama 10 vya upinzani nchini Tanzania vimefungua kesi Mahakamani Kuu kupinga muswada wa sheria ya vyama vya siasa

Umoja wa vyama 10 vya upinzani nchini Tanzania vimefungua kesi Mahakamani Kuu kupinga muswada wa sheria ya vyama vya siasa

Hii kitu sio kituko!! Unapinga mswaada ambao haujawa sheria au wanapingwa usijadiliwe bungeni? Mahakama inaweza kuingilia mswaada ulioko ktk muhimili wa Bunge kwa kujadiliwa?
 
Hii kitu sio kituko!! Unapinga mswaada ambao haujawa sheria au wanapingwa usijadiliwe bungeni? Mahakama inaweza kuingilia mswaada ulioko ktk muhimili wa Bunge kwa kujadiliwa?
Wewe ndio kituko, kasome ibara ya 30 ya katiba ya JMT, mtu yeyote atakayeona haki zake zinavunjwa au ZINAELEKEA kuvunjwa ana haki ya kwenda mahakamani kuzuia,

Mahakama inajua shauri lililopo ndiyo maana imekubali kesi ifunguliwe, kusingekuwa na haki hiyo wala isingesumbuka kusitisha likizo.
 
hizi siasa za hapa nyumbani pasua kichwa tu, yaani mtu unakua mpinzani for more than 20 years wewe unapinga tu kila administration; hatujawahi kukuona ukisupport chochote!

badilikeni jamani.
Kwanza kabisa nakushangaa hivi maana ya upinzani ni kussuport?
Upinzani ni kuibua hoja ili serikali izifanyie kazi, na zinapofanyiwa kazi kazi ya upinzani ni kuibua hoja zingine wakissuport maana yake ni kwamba hakuna changamoto tena, nimekupa elimu kidogo maana naona uelewa wako uko chini kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nafikir sasa ni muda kwa vyama vya upinzani kuwa na makao makuu ya pamoja ili kuimarisha umoja huo, kuliko kukaa ofisi za uchochoroni mnatia aibu, mkiwa katika ofsi halali inayojulikana Tanzania nzima hata vikao vyenu vitakuwa na uhalali wa kiwango kisicho cha kubughudhiwa, sababu kitaaminiwa.

Tujadili hoja iliyo mezani. Ofisi ni watu na kamwe siyo jengo chalii....

Unaweza kuwa na jengo nzuri lakini ndani umejaza mifupa na uchafu mtupu kama ilivyo majengo ya CCM....

Cheki kule Magogoni, jengo zuri, jeupe na bustani nzuri lakini linakaliwa na "kichaa" aliyethubutu kujitangaza mwenyewe kuwa yeye ni kichaa....

TANU iliendesha harakati za ukombozi wa nchi hii toka makucha ya wakoloni wa Kiingereza wakifanyia vikao na makutano yao chini ya miti ama kwenye nyumba za wanachama waliojitolea....!!

Usiwatoe watu kwenye hoja. Huna cha kuchangia hoja lala ama tulia kimya...
 
Hiki kitu ndicho kinanishangaza! Ukianga ule Muswada unakataza tu kufanya mikutano sehemu isiyo yako! Yaani kama Zitto ni mbunge wa Kigoma mjini basi akafanye mkutano huko Kigoma mjini aongee na wananchi wake, asikilize kero zao awape mrejesho lakini hawataki wao wanataka wote waje kufanyia mkutano hapa Dar wakati si sehemu zao! watu wa Dar wanakuja kutumbia nini hasa?
Mbali na kuwa mbunge yeye Zitto ni kiongozi mkuu wa Chama cha ACT WAZALENDO unafikiri ataenezaje sera za chama chake nchi nzima?
Watu wenye damu ya kijani mna shida sana upande wa kufikiri bora hata ya mjusi ana damu ya baridi lakini anajitambua

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sio kukaaaa kmya, nachokisemea ni kusubilia matukio ndio iwe ajenda yao kwa mda wote mpaka pale litakapotokea tukio jingine,, ambapo nao hubadili gear na kugeuza kuwa ajenda kwao.

Sent using Jamii Forums mobile app
Umezisoma sera mbadala za CDM?Mimi nimezisoma,ni sera nzuri sana kwa maoni yangu!
Lakini linapotokea jambo ambalo si sawa,ni muhimu wao kulipa kipaumbele na kulipigia kelele!Nadhani kikokotoo,suala la korosho,ajira,sheria za makosa ya mtandao,sheria za takwimu na sasa sheria za vyama vya siasa ni mambo ambayo haiwezekani kuyakalia kimya,tofauti na hapo vyama vya upinzani vingekuwa havijui wajibu wao!
 
Mbali na kuwa mbunge yeye Zitto ni kiongozi mkuu wa Chama cha ACT WAZALENDO unafikiri ataenezaje sera za chama chake nchi nzima?
Watu wenye damu ya kijani mna shida sana upande wa kufikiri bora hata ya mjusi ana damu ya baridi lakini anajitambua

Sent using Jamii Forums mobile app
Shidanata sio ukijani shida tumezoea siasa holela! ni ukweli ulio wazi kuwa waafrica vichwa vyetu haviwazi kushikamana kwaajili ya maendeleo yetu sie tupo ili tukwamishane tu! hatupendi hata kidogo mtu fulani afanikiwe na hapa ndipo white wanapotutumia kwa udhaifu wetu huu!

Siasa za kiafrica hazioni hatari wanasiasa wake wakikesha barabarani wakiandamana! siasa za kiafrica kila kukicha mikutano ya hadhala. Hizi siasa za kiafrica usitegemee bunge liwe na wabunge wengi wa chama pinzani alafu utegemee bajeti kupita! Hivi ata reli ya SGR isingejengwa kama humo bungeni kungekuwa wabunge wa upinzani na baadae wangekuja wao kuomba kura kwa kigezo wale wameshindwa kufanya sie tutafanya.
 
Nani anayepima mitazamo, wanaosaini mikataba mibovu na kuuza maliasili zetu ndio hao wenye mitazamo chanya?
Naamini kabisa kuna mazuri yaliyofanywa na Serikali ya CCM katika hayo yote mnayoyapinga kama kweli lengo lenu ni kulijenga Taifa ni kwanini hata katika hayo mema hatuwasikii?
 
Hao ni wasanii tu,wameshindwa kabla ya kuanza
Bunge na mahakama ni mihimili isioingiliana,kama abavyo bunge haliwezi kuingilia shughuli za mahakama,vivyo hivyo mahakama imefungwa mikono kuhusu kulizuia bunge kufanya kazi zake
Ingekua rahisi kihivyo wangeenda kuzuia bunge lisipitishe miswada mingi sana,lakini kwa kua upinzani Tanzania umejengwa kwa misingi ya ghilba na hadaa,hapa wanajaribu kuwa enjoy watanzania
 
Naamini kabisa kuna mazuri yaliyofanywa na Serikali ya CCM katika hayo yote mnayoyapinga kama kweli lengo lenu ni kulijenga Taifa ni kwanini hata katika hayo mema hatuwasikii?
Hata la kikokotoo hujawasikia wapinzani.
 
Kwanza kabisa nakushangaa hivi maana ya upinzani ni kussuport?
Upinzani ni kuibua hoja ili serikali izifanyie kazi, na zinapofanyiwa kazi kazi ya upinzani ni kuibua hoja zingine wakissuport maana yake ni kwamba hakuna changamoto tena, nimekupa elimu kidogo maana naona uelewa wako uko chini kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
Wewe utakua ni kiongozi huko upinzani Maana tafsiri ya upinzani waliyo nayo ndio kama yako.

Yanapokuja katika maswala ya msingi ya kitaifa watu huweka itikadi zao pembeni na kulisupport Hilo jambo lakini hapa kwakua tafsiri iliyopo kwenye akili za viongozi wa upinzani pamoja na wafuasi wao kuwa upinzani ni kupinga kila kitu basi wao hata katika Yale maswala ya muhimu yenye faida kwa Taifa wao wanapinga ili mradi eti wabakie na heshima Yao kuwa wao ni wapinzani. Huko ni kupotoka na kujenga tafsiri potofu ya upinzani kwenye akili za watu.
 
Hao ni wasanii tu,wameshindwa kabla ya kuanza
Bunge na mahakama ni mihimili isioingiliana,kama abavyo bunge haliwezi kuingilia shughuli za mahakama,vivyo hivyo mahakama imefungwa mikono kuhusu kulizuia bunge kufanya kazi zake
Ingekua rahisi kihivyo wangeenda kuzuia bunge lisipitishe miswada mingi sana,lakini kwa kua upinzani Tanzania umejengwa kwa misingi ya ghilba na hadaa,hapa wanajaribu kuwa enjoy watanzania
Kwahiyo wewe unajua zaidi ya majaji waliositisha likizo kuja kusikiliza.
 
Back
Top Bottom