hivi viwanda vinazalisha hand to mouth au? kwanini wasiweke stock kubwa itakayotumika wakati wa law season? azam waliomba wajengewe bwawa la kinga maji ambalo lingetumika pia kwa umwagiliaji na kunyweshea ngombe za wamasai simba jike akapotezea then leo tunaletewa blah blah za shortage, kimsingi viwanda vizalishe hawana bidhaa traders wa import,
 
Hujawasikiliza na kwa hiyo hata hujawaelewa kabisa...!!!

Uthibitisho ni hiki ulichokiandika na ni kwa sababu tu, wewe ni mtu mwenye upande tayari ambaye hata kifanyike kitu gani mtu hawezi kubadilisha msimamo wako...

Kwa lugha rahisi ni kuwa, wewe FaizaFoxy si mtu huru kimawazo na kimtazamo
 
sijaelewa, kwenye maelezo yako unaelezea ishue za ujinga, upi? nani unaona ni mjinga mie au nani?

Hata wewe unaweza kuwa miongoni mwao, pengine...

Mwenzio amefafanua hoja zilizotolewa na TSPA kwa kirefu sana...

Hoja ya "ujinga" kwa maelezo ya ndugu Richard inamhusu yeyote ambaye hajawaelewa hawa TSPA. Which means hata wewe unaweza kuwa miongoni mwao..

Personally, nimefuatilia PC ya hawa TSPA mwanzo mwisho. They were very calm and genuine kwa kila hatua ya ufafanuzi wao juu ya sakata la sukari hapa nchi...

Whether we like it or not, Wizara ya Kilimo na Hussein Bashe (waziri wake) hawakui - handle situation ya sugar gap wisely...

Bahati mbaya sana kuwa, Bunge nalo ignorantly likaingizwa mkenge na mawaziri hawa wawili (Mwigulu - Fedha na Bashe - Kilimo) kiasi cha kushindwa kulisimamia jambo kwa ukamilifu wake..
 
Kwanini hizi taarifa hazikutoka mwishoni mwa 2023,
Na bado mtatajana wote wezi nyie
 
Inasikitisha sana
 
Angalia video iliyopostiwa utaelewa ninachosema bwashee!
Hapana.
Hizo 'dots' unazoziona wewe hazipo. Jambo hili la sukari halina utata tena juu yake, kwa sababu maelezo ya kujitosheleza kabisa yamekwisha wasilishwa.
Ukitaka 'kuziumba' hizo 'dots' kufurahisha akili zako, hilo ni jambo jingine kabisa ambalo mimi sioni nishiriki vipi kuzijadili hizo 'dots' za kufikirika.
 
Sawa bwashee
 
Ammi Mpungwe
JF kwa mafaili!
 
Nimewasikiliza mwanzo mwisho, wamepiga porojo na wanataka kujiosha tu.

Wao kama wataalam wa sukari wako wapi mpaka sukari Tanzania inakuwa bei ya juu kuliko nchi zote zinazotuzunguka?

Wameliongelea hilo?
 
Wazungu wanasema waafrica wenyewe ndio wanao ruhusu kuwa exploited.

Huko kwa wazungu mbali hawa wazanzibari tu wanatuita watanwa.

Think
Hilo ni ukweli unaouma.

Tazama mijitu mizima imeitisha mkutano na waandishi wa habari kuja kupinga serikali kufanya njia za haraka kuagiza sukari ili mwananchi asiendelee kuumia.

Nilikuwa namuona Ame ni mtu wa maana sana, sasa nimeelewa kumbe ni mtwana kama watawana wengine.
 
Wacha muneno
 
Wazalisha sukari wana mapungufu makubwa, kila mwaka ni Sugar Scarcity, Sugar Deficity, wakati hii ndio secta yao ya biashara.

Walitakiwa wazalishe sukari ya ziada ya kukabiliana na uhaba wa sukari kila unapojitokeza.

Ni kwamba kwa miaka mingi ya uzalishaji sukari, bado wameshindwa kutosheleza mahitaji ya ndani pekee achana na export.

Hapo ndipo muuza vocha anapo take advantage kwa kuwatumia watendaji wa Serikali.

Wazalisha sukari wangefikisha malengo tarajiwa huu mvutano wa kila mwaka usingejitokeza.
 
Shida ni hii bei za sukari ni kubwa mno ukilinganisha na majirani zetu.
Speaker juzi aliwauliza wabunge bei za sukali nchi majirani ni wastani wa sh 2000 kwetu ni sh 4000.licha ya kuwa na viwanda kibao.
Huyu Mzee Balozi tunamheshimu,lakini ummoja wa wazalishaji nchini wametengeneza Cartel ya kutunyonya wananchi.
Pili hawajifunzi wanaendesha uzalishaji kizamani.Wakati wazalishaji Brazil wanazalisha mazao(byproduct) zaidi ya 30 kwenye miwa hiyo hiyo.kwao sukari ni byproduct 1 kati ya byproducts zaidi ya 30,hivyo sukari ina bei ndogo sana sh 600 tu.

Kama hawezi kujitanua jembe la Brazil litapiga hodi kuzalisha sukari na mazao kibao yatokanayo na sukari,itapunguza gharama ya uzalishaji pammoja na kuongeza ajira,na kuna uwezekano wa kutoagiza madawa au spirit,mbolea itokanayo na miwa. Nisikilizie mziku huo wanaogopa hata kivuli cha Brazil.
 
Duuh ni hatar sana.

Watanzania tunakula vitu vingi vya ovyo kama unampa muuza vocha aagize sukari inayoenda kutumia na mamilion ya watu SI ajabu sukar yenyewe ikawa ime expire muda mrefu tu.
 
Mm mwenyewe nimejiuliza haya maswali naona kama watu wamezungukana kwenye madili.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…