Kama wazalishaji wameshindwa kuzalisha kwa bei ya chini hakuna haja ya kuendelea kuwalinda. Na kuwapa wao tu vibali vya kuagiza ni kuwakosea wananchi.
 
Japo hata wewe hujaonyesha ushindi wa Bashe kwa hoja walizoziibua. Wamesema waliitaadharisha serikali juu ya upungufu wa sukari mara mbili,na hawakujibiwa. Pia wao ni wazalishaji wa sukari na siyo wanunuzi. Sasa unawapaje jukumu la kuagiza sukari?
Hekima ituongoze kwenye hili wengi tunajua serikali Ina urasimu sana, japo inawezekana haukusababishwa na Bashe, lakini ni mtendaji/ msemaji mkuu wa wizara ya kilimo, hivyo hata kama wameharibu ni lazima asimamie nao tu.
 
Huwezi kuelewa kwa sababu unaangalia juu juu tu. Ni lazima uunganishe dots ili uelewe!
Hizo 'dots' za kuunganisha ziko wapi?
Kama ni 'dots' tu, si ungeweka mifano miwili mitatu hivi, tuone kama kweli zinakubali kuunganika?

Sasa najiuliza, sijui ni kipi kilicho ingia kichwani mwako na kuwaza kuandika haya uliyo andika hapa, ambayo hayana msaada hata kiduchu!
 
Umoja wa Wazalishaji wa sukari nchini (TSPA) umekanusha madai ya kuficha sukari ili kuongeza bei kwa faida yao binafsi

Wamesema hawana nia ya kuwa waagizaji kwa sababu lengo lao ni kuzalisha zaidi, huku wakilalamika kwamba wametuhumiwa na kuhukumiwa bila kupewa nafasi ya kusikilizwa

Wamesema wao hawana nia ya kuwa waagizaji wa sukari, kwa sababu lengo la biashara yao ni kuzalisha zaidi.

Akizungumza kwa niaba ya wazalishaji wa sukari leo Jumatatu, Julai 1, 2024, mbele ya vyombo vya habari jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Wazalishaji wa Sukari nchini, Ammi Mpungwe, amesema tangu utabiri wa hali ya hewa ulipotangazwa na kuonesha kwamba kutakuwa na mvua za El Nino, wazalishaji waliwasiliana na mamlaka za Serikali kuzitaarifu kwamba Desemba mwaka jana kungekuwa na tatizo.

Kwa hivyo, waliomba utaratibu wa uagizaji sukari uwekwe.

Licha ya ufafanuzi huo, itakumbukwa siku chache zilizopita, kulikuwa na mijadala sehemu mbalimbali ikiwamo kwenye Bunge lililoahirishwa Ijumaa Juni 28, 2024 iliyokuwa ikiwatuhumu wafanyabiashara hayo kuhusika katika kusababisha bei ya sukari kupanda bei.

Baadhi ya watu katika mijadala hiyo walidai wazalishaji wanatengeneza nakisi ya sukari kwa makusudi ili waweze kujinufaisha, jambo ambalo Mpungwe anasema si kweli.

β€œKulikuwa na mawasiliano na si mara moja wala mbili, tulikuwa tunakumbushia na kweli ilipofika Desemba hali ikaanza kuwa vile tulivyosema,” amedai Mpungwe.

Amesema cha kushangaza, hadi Desemba vibali vya kuagiza sukari vilikuwa havijatoka na Kampuni ya Sukari Kilombero ikalazimika kuizuia meli yake iliyokuwa inapeleka tani 45,000 ya sukari nchi nyingine na kuagiza iingizwe nchini kwa lengo la kufidia upungufu mkubwa uliojitokeza.

Mpungwe ambaye pia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Kilombero Sugar, amesema si kweli kwamba kampuni hizo zilipewa vibali vya kuagiza sukari na kuviuza.

Amesema kazi ya uagizaji sukari kutoka nje si yao, wao ni wazalishaji tu na hulazimika kuingilia kati kwenye usambazaji kama kuna uhaba nchini kama walivyofanya kwa lengo la kukabiliana na uhaba na vurugu kama zilizokuwepo.

β€œSisi kama Kilombero hatutaki kuingia katika biashara ya kuagiza sukari, tuko katika biashara ya kuzalishaji sukari, hili wazo la kuweka chombo cha Serikali kuagiza sukari nadhani lingekuja tangu mwanzo tungeunga mkono,” amesema Mpungwe.

Amesema wazalishaji hao waliamua kukaa kimya pale waliporushiwa maneno kwa sababu walikuwa wakiwasiliana na Spika wa Bunge ili wapate nafasi ya kuzungumza na Kamati ya Kilimo na Viwanda, lakini walipangiwa kukutana Agosti, mwaka huu.

β€œTulipewa nafasi ya kukutana na kamati ya uchumi na bajeti wiki iliyopita, lakini ilikuwa ni kuzungumzia muswada wa fedha, tulijitahidi kuwa na mawasiliano lakini uamuzi umetoka bila sisi kuhusishwa tumekuwa watuhumiwa hadi tumehukumiwa bila sisi kusikilizwa,” amesema Mpungwe.

Amesema kutuhumiwa kwamba hawawafikirii Watanzania zaidi ya milioni 60 si sawa, kwa sababu wamefanya uwekezaji mkubwa unaodumu kwa zaidi ya miaka 60.

β€œTumeshutumiwa kuwa sisi ni cartel ni tuhuma nzito katika biashara, huwezi kuwa na mpango mkubwa wa kuwekeza ukajiingiza katika mambo haya na tuhuma hizi haziamriwi kisiasa,” amesema.

Amesema kama kuna hofu kuwa wawekezaji hawa wanacheza mchezo mchafu kwenye biashara, wapelekwe Tume ya Ushindani (FCC), wakajibu tuhuma zao huko.

Naye Mwakilishi wa Bagamoyo Sugar, Hussein Sufian amesema kauli ya kuvitaka viwanda vya sukari kutoficha sukari wakati hakuna kiwanda kilichowahi kuficha sukari, sio sahihi.

Amesema wamejengewa taswira mbaya isiyo na ukweli kwa washirika wa maendeleo ya sekta ya sukari na umma kwa jumla.

Kuhusu dhamira ya kuondokana na uzalishaji sukari nchini ili kuleta sukari ya nje na wakulima kuhamasishwa kulima mazao mbadala kama mpunga, amesema inadhoofisha jitihada zilizokwishafanyika za kuleta utulivu kwenye sekta ya sukari.

Wakati hayo yakisemwa, Sufian amesema pia sekta hiyo inaendelea kukabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya gharama kubwa za uzalishaji.

β€œGharama za mahitaji muhimu kwa kilimo cha miwa na uzalishaji sukari zimeongezeka sana katika miaka ya hivi karibuni pia uwepo wa sera zisizotabirika za soko la sukari ni tatizo,” amesema Sufian.

Mwananchi ilimtafuta Msemaji wa Serikali, Thobias Makoba kutaka kujua undani wa malalamiko hayo, akajibu kwa ujumbe wa maandishi kuwa; β€œNingekushauri kwa hoja kama hizi ni vyema ukaanza na wizara ya sekta husika.”

Katibu wa Bunge, Nenelwa Mwihambi alipoulizwa kuhusu barua zilizoandikwa na TSPA aliomba kutumiwa ujumbe mfupi ambao haukujibiwa.

Kwa upande wa Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe na Naibu wake, Joseph Silinde na Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Gerald Mweri simu zao ziliita bila kupokelewa.
 
Mkuu, usiongee bora umeongea tu, bila shaka umesikiliza video mpaka mwisho ingawa imechakachuliwa.

Kwanza Mzee Mpungwe ni "distinguished figure" kwenye nchi hii, hivyo ukimwongelea uangalie kila kona ya kazi zake katika nchi hii kabla hajaingia katika biashara miaka ya 90s.

Huko nyuma viwanda vilikuwa vikimilikiwa na serikali hivyo baadae vikabinafsishwa.

2015 sukari ilikuwa tani 200,000 kwa mwaka.

Tani 400,000 mwaka 2023 na sasa hivi mahitaji ya sukari yanaweza kutoshelezwa kwa asilimia 93.

Mwaka huu kuelekea mwishoni kutakuwa na Tani 528,000 kuanzia 2025/2025 yategemewa kuwepo na uzalishaji wa tani 660,000 na hata kuuza sukari hiyo nje ya nchi.

Kilombero Sugar wenyewe watarajiwa kuongeza uzalishaji sukari kutoka tani 130,000 kuwa tani 230,000 na pia wakulima wazungukao eneo la kiwanda nao watarajiwa kuongeza uzalishaji wa miwa 150,000 hadoi tani 300,000.

Tani 30,000 ni Gap sugar au nakisi na hii ni sukari ambayo ndo yagombewa na wauza vouchers.

Usisahau pia wakulima wa sasa wengi ni vijana ambao ni wasomi, hivyo wakopa kwenye mabenki ili walime mashamba ya miwa na wafanya hivyo wakichukulia kuwa kilimo hicho ndo njia bora ya kujiajiri badala ya kuzurura mijini.

Pia miwa ikiishatumika kupata sukari mabaki yake huweza kutumia kutengeneza nishati ya umeme ambao waweza kupelekwa kwenye NG.

Sasa angalia viwanda vyetu na ikiwa vyote vitakuwa na uwezo wa kuzalisha umeme wa taka za miwa wategemea kuwepo na tatizo la umeme kweli?

Ujinga huja pale mtu na akili zake anapokuwa akisema kwamba wakulima wa sukari washawishiwe kuacha kilimo cha miwa ili walime mazao mengine, what is this nonsense?

Hayati mwalimu Nyerere aliwahi kusema ujinga una "levels" na ukifika kiwango cha juu ndo twaona yanoendelea saa hii huko bungeni, ni vituko.

Mtu mwingine akisema sie waafrika tuna matatizo na huwa twajiroga wenyewe na kisha akakupa facts tupu utambishia kivipi?
 
HApa umefafanua vizuri, na inaonesha uko na uelewa kuhusiana na masuala ya sekta ya sukari
 
Huyo metl aliwahi kuleta sukari ya kk ambayo baadae iluzuiwa.
ilikuwa imeisha muda wake wa matumizi.

Watanzania hulishwa madubwana mengi tu sukari, mafuta ya kula kutoka nje ni hatari kwa afya kwani husababisha saratani.

Uswahili wachina nao wapo kazini na midubwana yao ya pombe kali.

Kuna issue ya mchele na kadhalika.
 
Kwann mnamwonea bashe?tulikuwa hatuwasikii mawaziri wa kilimo ni km hyo wizara haipo,leo iko kwa bashe mnatupia mawe. why? huyu jamaa ni mchapakaz napia ni hodari.bashe piga kazi wache wapige kelele watanyamaza
 
Shida ya kuruka stages katika ukuaji katika kazi. Kuna nafasi kama ulivyoeleza Zina hitajika experience na maturity baada ya kupitia changamoto mbalimbali na kuweza ku solve...Sasa wewe una kimbizwa kama mgonjwa na ambulance mpaka highest level unadhani Itakuaje?

Tujifunze kuandaa viongozi siyo kuwapa nafasi ya opportunism...
 
Bashe kamalizana lini na Mpina? wapi? ilikuwaje?

Kamati ya bunge haikutakiwa kumtetea Bashe, Bashe anatakiwa kujitokeza personally mbele ya watanzania kujisafisha juu ya tuhuma za kutudanganya watanzania.

Yeye ni kiongozi wa serikali, serikali inafanya kazi kwa ajili yetu watanzania, Bashe aje kwetu ajisafishe tumsikilize, tuchambue, kisha tulinganishe na kile alichosema Mpina tupate majibu.

Mpaka sasa Bashe ni bubu, amegoma kuongea, kwa maana nyingine huyu ameshindwa kumalizana na Mpina, hana majibu ya tuhuma dhidi yake, analindwa na bunge na Samia.
 
Kwann mnamwonea bashe?tulikuwa hatuwasikii mawaziri wa kilimo ni km hyo wizara haipo,leo iko kwa bashe mnatupia mawe. why? huyu jamaa ni mchapakaz napia ni hodari.bashe piga kazi wache wapige kelele watanyamaza
Unadhani ni nani awajobishwe?

Naomba unielimishe.
 
Kwann mnamwonea bashe?tulikuwa hatuwasikii mawaziri wa kilimo ni km hyo wizara haipo,leo iko kwa bashe mnatupia mawe. why? huyu jamaa ni mchapakaz napia ni hodari.bashe piga kazi wache wapige kelele watanyamaza
naona bashe unajichatisha...mnajua kabisa mlizoea piga ela kirahisi kwa kutoa vibali...now mmepigwa chembe mmekua wadogo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…