Mkuu mbona umewaka Sana kwa kitendo cha mwannchi mmoja kutaka kujua jinsia yako.
KWANI ungemjibu ME au KE ingekuwaje?
anyway...na mie naomba kujua jinsia yako tafadhali. ...kwa manufaa ya jukwaa tambulisha jinsia yako.
Hapo sijawaka kaka, nimeongea kwa upole tu.
Kutamburisha jinsia yangu hakutomsaidia muuliza swali/mwanzisha mada kupata majibu, tahadhari, au ufahamu wa alichouliza.
Na kwa kuwa mimi sio mkuu wa wilaya, mkoa, mbunge, wala waziri siwezi jibu swali nisiloulizwa.
Mwanzisha mada kauliza kuhusiana na "umri sahihi wa kutahiri mtoto wa kiume." Hakuuliza kuhusiana na jinsia ya God Heals, hivyo basi nimejaribu kujibu kile kidogo ninachofahamu.
Sasa anapotokea mtu mwingine, bila kuwa na busara na utuli, anakurupuka tu eti "wewe ni me/ke?" Hii itamsaidia nini muuliza swali? Je, ndicho alichotaka kujua?
Hatujuani, hatufahamiani, tumekutana tu hapa tukiwa nyuma ya "keyboard" zetu, basi tujaribu kujibu tunachoulizwa. Ukitaka kujua mimi ni wa namna gani, nitafute nje ya hapa. Asante!