UN kupinga mradi wa Steigler's Gorge ni uhujumu

Kwahiyo hoja yako kwamba UN wanapinga in favor of kampuni zao za kuzalisha umeme kumbe uliamua tu kupiga porojo sio?!

Au unataka kutuambia hao akina Aggreko na Dowans walikuwepo tangu enzi za Mwalimu?
Fikiria kwa mbali zaidi na kujiuliza kama hizo nchi zinazowafadhili UN, na wanakotoka Aggreko na Dowans, kama zilikuwepo toka enzi ya Mwalimu.
Hizo dots jiunganishie mwenyewe.
 

Mpongeze kwa kuthubutu kuropoka kuwa ataanzisha huo mradi lakini mtausubiri hadi kiama
 
Tatizo lako husomi na kufuatilia mambo!! Gesi ya Mtwara kuwa full kwa matumizi hapa TZ itachukua 36 years inayotumika sasa ni kidogo tu pia bado ni gharama ukilinganisha na maji.
Kwa hiyo mkuu wewe unapingana na wataalamu wetu ambao walikua wakisema mpaka 2025 tutakua tukizalisha Megawatt 10,000 ambazo zingine zingeuzwa nje?!

Hayo ya miaka 36 ndo kwanza nasikia kwako,sisi tuliambiwa 2025 tunaanza kuuza Umeme nje tena mpaka vijana wakapelekwa China kusomea kuja kuendesha mradi
 
Wambie wao ndo wachafuz wakubwa wa mazingira wakome
Kutuingilia
 
Mpongeze kwa kuthubutu kuropoka kuwa ataanzisha huo mradi lakini mtausubiri hadi kiama
Ewe mtanzania umelogwa na nani?
Hii shortsightedness inatisha.
Jiulize, siku za kiama watu hawatahitaji umeme wakutosha?
 
This is what we call Mental slavery
Free yourself from that...
 
Siamini kwamba eti mradi wa umeme wa Stiegler's Gorge utamaliza tatizo la umeme Tanzania.

Kwanza Duniani nzima, watu wanahama kutoka kutegemea vyanzo vya umeme wa maji kuelekea vyanzo vingine kwa sababu vyanzo vya maji kwa sasa siyo sustainable kutokana na mabadiliko ya Tabianchi. Sisi tunapoteza pesa kuelekea wenzako wanakokimbia.

Miradi mikubwa ya uzalishaji umeme wa gas imeishia wapi? Miradi ya uzalishaji umeme kutokana na makaa ya mawe ya Mchuchuma, na upepo (Singida na Makambako) imeishia wapi?

Kutokana na sera zetu mbovu miradi ya gas imekufa na wawekezaji katika sekta hiyo kufunga miradi yao na kuhamia Mozambique. Tumeacha gas yetu, kwa ujinga tunashabikia bomba la mafuta la Uganda ambalo mapato yake ni ushuru tu. Ni sawa na mtu anayeacha kulima shamba lake lenye rutuba lakini anafurahia kupangisha ghala lake kuhifadhia mazao ya jirani yake, tena ambaye shamba lake ni dogo kuliko la kwake.

Sera mbovu za uwekezaji za awamu hii zimeua uwekezaji. Sasa miradi ya gas na makaa ya mawe imeyeyuka.
 
Very well argued. Kama mtu haelewi haya uliyoyaandika hataelewa milele. Huyo ni hasara kwa nafsi yake, familia na nchi nzima.
 
Ewe mtanzania umelogwa na nani?
Hii shortsightedness inatisha.
Jiulize, siku za kiama watu hawatahitaji umeme wakutosha?
We jidu, huo umeme hautakuwepo asilani,kelele za yule jibwana syo za kuamini sana,tunaingia mwaka wa tatu sasa hakuna jambo la maana alofanya,bomberdier mmeambiwa ni hasara,bomberdier imekamatwa,ujenzi reli ya kisasa utakuwa kama mv dsm ni muda tu utasema,saaana atakamilisha uwanja chato na hasara kubwa 2025 kurudisha wizara dsm,mabweni udsm viraka viraka
 
Fikiria kwa mbali zaidi na kujiuliza kama hizo nchi zinazowafadhili UN, na wanakotoka Aggreko na Dowans, kama zilikuwepo toka enzi ya Mwalimu.
Hizo dots jiunganishie mwenyewe.
Sina uwezo wa kufikiria mbali kwahiyo ningekuomba ujibu swali nililokuuliza!

Kwavile umesema UN kupitia UNESCO wamekuwa wakiupinga huu mradi tangu enzi za Mwalimu!

Na pia unasema hawa UN wafanya wafanyayo kwa ajili ya kulinda makampuni yao ya kuzalisha umeme kv Dowans & Aggreko!

The question is: hayo makampuni yalikuwepo wakati wa Mwalimu? Au wakati huo ilikuwa ni kwa ajili ya kulinda makampuni yao yapi?!
 
Nasubiri umeme urudi ninyoshe nguo niende kazini!
 
Mpe moyo
 
Ndio maana nimekuuliza ili uweze kufikiria steps mbili au tatu mbele.
Jiulize kwamba wakoloni walipoondoka Tanzania walikufa au?
Na interests zao zilikoma?
Kuwa na Aggreko na Dowans ni kielelezo tu cha interests za hao wakubwa.
Kesho inaweza ingia kampuni lenye jina tofauti.

Mwafrika, kila mtu anataka upumbazwe ili daima ubaki tegemezi.
Na ukiwa tegemezi, umeshatawaliwa upya.
 
Weupe wanatumia mbinu na vyombo mbalimbali kudumaza maendelea yetu.Msthslan vyombo vya habar na hizo international Organs. So katika mambo ya msingi haya Wantanzania maxima tuwe kitu kimoja .Acheni upinzai was kiuchwara kupinga kila kitu
 

Usichokijua ni kuwa gesi YOTE ILISHAUZWA. na gharama ya umeme wa Gesi ni kubw amno kwa sasa maana gesi sio yetu..
 
Google ESIA hata za 1940s zipo by zinanataa mradi down towards Rufiji.
Nitazisoma na kuzielewa, lakini nitakukumbusha maana ya dunia na maendeleo. Mimi ni mtu ninayejifunza kila siku na nimejenga uelewa. Je, unafahamu kwamba karne ya 19 tu hapa juzi, Ulaya ilijaa misitu ya asili na wanyama porini? Wakatumia misitu yao kwa ujenzi wa nchi na kuwinda wanyama kujifurahisha na leo hii wanalazimisha Afrika iache mapori kwa manufaa ya Dunia?

Maliasili yetu lazima itumike kwa maendeleo yetu na siyo ya mtu wa 'UN' kama tunavyoeleza. Hakuna anayetaka kutoa fidia kwa utunzaji wetu na Mahathir Mohamad aliwaeleza wakiwa Brazil kwamba tupeni pesa tulinde dunia, hamtaki tutatumia tunavyotaka, tuishiwe wote halafu tuanze upya!

Jiulize kwa nini Mjerumani alijali sana hiyo steigler lakini hakujali kuona binadamu akiuzwa kama bidhaa. China imejenga dam kwa miaka 17. Dam kubwa la umeme kuliko lolote duniani, 20,000 MW za umeme zaidi hata ya nuklia zote za UK. Je, unajua ni watu wangapi walihamishwa kwenye eneo la kilomita mbili?

Nakuuliza haya yote ili uone tofauti ya uelewa tulionao ndani ya JF. Acheni ushabiki wa kusoma taarifa za WWF na kuamini ndo mema ya TZ. Siamini kama WWF ina utaalamu kuliko tulioko nje ya ofisi zao, maana wanachokifanya ni kama wanafunzi wanaofuata maelezo ya mwalimu bila kuangalia uhalisia.
 
UN wafunge makambi ya wakimbizi yanayo haribu mazingira... watu wanakufa wao wanaleta ishu ya mazingira... Uhai Uhai Uhai... watu kama wapo misri wanataka kwenda kanani... wao wanasema mazingira? UN... wana angalia manufaa yao tu... na watu wa magharibi...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…