Unadhani kama tungekuwa na tume ya uchaguzi kama ya USA, Samia angeweza kutoboa hata kwa 10%?

Weka hii comment kwa rejea yako, mwakani Dkt. Samia atashinda vikubwa sana, hata kama hupendi lakini ndio hivyo tena. Waislamu wanampenda, Wakristo wanampenda na hata Wapagani wanampenda. Sema wewe ndio hutampigia ambayo ni kura almost negligible kwa kura zote.
 
Sijasoma mpaka chini kwani ni pumba tupu.

Kumbuka kwamba wizi na ufisadi umekuwepo tangu Nyerere akiwa madarakani miaka 40 iliyopita.

Nchi haina adabu wala uoga tangu miaka hiyo, uonevu na ushenzi wa kila aina pale wizara ya ardhi upo ulikuwepo na utaendelea kuwepo siku zote.

Report chafu za CAG zinatolewa kila mwaka hazijali ikulu yupo ME au KE.

Cha muhimu ni kuachana na hizi kasumba za kishamba kwamba Mwanamke hawezi kuwa rais, ndio keshakuwa sasa ndio yupo pale ikulu tangu 2021 March na nchi inakwenda vizuri sana.

Tazama uwekezaji ulivyopanda kuanzia alipoingia ikulu mpaka leo, tazama mazingira ya biashara yalivyo mepesi muda huu.

Jinsia wakati mwingine ni upuuzi mtupu, Ujerumani imeongozwa na Chancellor mwanamke kwa miaka 15 na uchumi wake ukiwa juu kuliko mataifa yote ya Ulaya.
 
Hapo hakuna issue ya jinsia bali ni kuuzika kisera.

Samia ana sera gani kwa mfano ambazo zitakupa hamasa kumchagua ?

Miaka yake mitatu aliyookota dodo kwenye mbuyu si unaona alivyopwaya?

Samia ukiondoa PR na kulipa machawa hana ushawishi hata wa kumkaribia Lipumba na CUF ile ya 2005 na wakati huo hakukuwa na mitandao ya kijamii inayounganisha watu kutokana na watumiaji wa internet kuwa wachache.
 
Huo ndio uhalisia katika jamii za watu Duniani,hata wewe leo hii sio chochote kukiwa na uchaguzi wa haki katika hii nchi tukiwasimamisha one to one na SAMIA ambaye ni maarufu na kila kitu,wewe utashinda.
 
Umeongea upuuzi wa Hali ya juu sana, unajaribu kukimbia ukweli ambao uko wazi kabisa.

Samia anamlizia miezi almost 10 sasa ya Urais wa URITHI, labda kama mbinu yenu ya wizi wa kura, kupiga kura na kuweka kwenye mabegi ilikujazia na kupata ushindi wa uongo.

Lakini pia kutumia vyombo vya dola kama Polisi , lakini kura kama kura za watanzania, Samia hana chake, nafuu yenu Jaribuni kumpa MAJALIWA agombee, lakini hiyo Mama hamna kitu, ajiandae akalee wajukuu kizimkazi.

Au aende OMAN kwa wajomba zake ambao amewauzia kwa mnada maliasili za Tanzania Bara, lakini kawauzia Bandari za Bara.

Kama kweli Watanzania wana akili sasa ni wakati wa kukataa Rais ambaye anauza rasilimali za Nchi.
 
umedema 10 au 110? CHADEMA na kelele zote inakosa wagombea kwenye vitongoji na mitaa- uwe unaficha aibu yako
 
Tuendelee kukataa wanawake sababu wanaume wametupa maendeleo makubwa sasa TZ ni kama mbinguni 😂
 
Hata asilimia Mbili hawezi kupata.
 
Chukua hii itakusaidia. Mwenyekiti wa CCM ndiye anateua wafuatao;
1. Mkuu wa majeshi (CDF)
2. Inspekta Jenerali wa polisi (IGP)
3. Jaji mkuu
4. Kamishna wa TAKUKURU
5. Mwenyekiti wa tume ya uchaguzi
6. Mkurugenzi wa uchaguzi
7. Kamishna wa idara ya uhamiaji
8. Mkuu wa usalama wa taifa (TISS)
9. Wakurugenzi wa wilaya ambao pia ndo wasimamizi wa uchaguzi majimboni
10. Msajili wa vyama vya siasa.

Mwenyekiti wa CCM ni mhimili wa mihimili mingine.
 
Ni dhahili kwetu huku siyo sera bali ni chama mhusika anachotoka na affliation yake na vyombo vya ulinzi na usalama. Dkt Samia ili ashinde basi vyombo vya ulinzi na usalama vimkubali (kitu ambacho mpaka sasa hana maelewano navyo-ushahidi kabadili DG Tiss mara kazaa), maana yake ni dhahili kuna vitu alitaka kulazimisha TISS wakakataa kata kata akafukuza DG, na maana yake uchaguzi utakuwa huru na haki na hivyo kupelekea kushindwa uchaguzi. Kosa lake kubwa Dkt Samia ni kuacha kutumia mfumo halali na kujitengenezea wake, sasa hivi CCM hawatembei na image ya rais bali wanaimarisha brand ya CCM
 
Angalau mmeanza kufikiri vizuri! No fair competition no winner! Mama atapewa urais
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…