Unadhifu na mpangilio wa mavazi kwa mwanamke

Unadhifu na mpangilio wa mavazi kwa mwanamke

Shikamoon wakubwa zangu
Wadogo zangu,hamjambo.

Leo niongee kitu cha tofauti kidogo,hususani kwetu Sisi wanawake, mm mwenyewe si msichana tena,hata mamangu mara nyingi ananihusia hili kuhusu mwenendo wangu na mpangilio wa mavazi.

Hebu Kwanza niulize,
Hivi wanawake wenzangu mnaovaa taiti za kubana,bila hata mtandio,mbaya zaidi mistari wa chupi unaonekana na mtu huna habari wala nini, mbaya zaidi mtu kavaa pedi,na inaonesha kabisa imevimba au imekaa upande,mmmh aibu naona mm!

Hivi mnajisikiaje,
Na hili Tatizo lipo Sana kwetu Sisi wakristo kutojipenda waziwazi,na kuwa na uzungu mwingi.

Binafsi nadhani kuzaliwa na kukulia,au kuchangamana na jamii,ya pwani kumeniathiri na kupenda mavazi na taratibu za kiislamu,yaani kiukweli siwezi kwenda kilomita 3 kutoka nyumbani bila mtandio,siwezi vaa suruali ya kubana,au gauni linalobana,niwapo nyumbani ni vijora ,madela na magauni siwezi vaa suruali wala kaptura,sijui wenzangu mnawezaje.

Hivi hizoo taiti zenu zikichanika bahati mbaya aidha umegusa kitu chenye ncha Kali inakuwaje.
Wengi hamtembei na khanga wala mtandio kwamba utajistiri.

Mmmmh siwezi bora nionekane mshamba

Karibuni tule lunch ya ofisini kwetu🌹o
Judgmental and clueless 👎
 
Marry anapiga personal sana alooo!! 😹😹
Nimemuogopa Marry kuanzia leo simchokozi hata kidogo..!! Anaroast km grok 😹😹
Ah bc ngoja na mm nikae kwa Seran, mbona hata yeye anapiga pasi kama za chama mpaka golini 🔥
 
Back
Top Bottom