Wakuu jf amani ya Bwana ikawe juu yenu kila mmoja kwa imani yake ,poleni na Tanzania pia.
Kwa mara ya kwanza nchi ya tz inaweza kwenda kwenye uchaguzi mkuu katika alert kubwa , why , na nini kipo Ikulu kisa madaraka tu ambayo huwezi zikwa nayo, baki nayo milele.
Leo wenda vijana wetu katika vyombo vya usalama wa nchi wapo katika wakati Mgumu kuliko kipindi chochote kile , achana na hao wakubwa zao watoaho Maagizo wakiwa kwenye viyoyozi, hii ni hatari sana.
Wananchi wanasema 29 Oct wanakiwasha ila bado kama viongozi mmeziba masikio ila kikiwaka kweli si ndo nyie wa kwanza kukimbia na kuwaacha vijana wetu mnaowategemea wawalinde kwa sasa katika mzozo mkali na jamii zinazo wazunguka au nao mtawapa passport , why fika hapa?
Napendekeza kwa mda huu nyie viongozi acha uchu wa madaraka na badala yake angalia nchi / taifa kwanza mengine badae .
Kauli za watu kama Nape haziwezi saidia taifa kwa sasa tulipo, mfano hao sisimizi ukisha wauwa unafikiri utabaki salama, na je wa kuonja joto la jiwe kwa wakati huo ni Nape au mwenyekiti wake sasa na watu walio chini yake.
Nape amekua kiongonzi ila bado yupo na ushamba wa uongozi na bado hajui Dunia .
Mwisho
Bado Mungu wangu ananiambia mwaka huu hakuna uchaguzi ,jitafakarin na chukua hatua
Thanks