Unaepuka vipi kuwa "Chikunde" ukiwa unadate na mtu mambo safi?

mambo ya wazungu tuwaachie wenyewe. mimi kulia hata kijiko tu huwa naona mateso sana.
Mi hadi kwenye ndege nilikataaga haya mambo yao ya visu na uma nikagonga kwa mkono tu. Tatizo sasa hawana maji ya kunawa, ni vitishu fulani tu wet (wipes), ilibidi tu nijiongeze nikaenda kunawa chooni, teh!
 
Siku moja nililazimishwa kula burger nilihangaika aisee kujilazimisha kidogo nitapike
 
Umeonaa uzi hata auhusu misosi ndo washaubadili content, ilikua jinsi ya kudeal na ka ushamba ukienda sehemu mambo safi, vitu huvijui
Binafsi nilitegemea kuona wadada humu mlivyo wajanja wa maeneo ,sehemu za ukweli na za kishua Mnavyojiachia ,kuanzia kuagiza,hadi kuvitumia ,mfano hotel siku ya kwanza jacuzzi mnavyopza maji baridi na moto, kucheza na remote za ac , kuweka uma kisu kushoto Kijiko kulia, nijifunze kitu,

Sasa Uzi umekua wa menu tena
 
Mi hadi kwenye ndege nilikataaga haya mambo yao ya visu na uma nikagonga kwa mkono tu. Tatizo sasa hawana maji ya kunawa, ni vitishu fulani tu wet (wipes), ilibidi tu nijiongeze nikaenda kunawa chooni, teh!
ni ujinga tu msosi mtu unakuwa hauufaidi vizuri. mikono ndio unaenjoy
 
Kulala kwenye jakuzi hatujazoeaa tushazoea kuoga tumesimama tu[emoji23][emoji23][emoji23] ndio nataka nianze kujaribu sasa hivi
 
Unaeza shangaa wote ni kina chikunde ila kukubali ndo ishu
 
I'm a big time fun of plant based food.

Hapa Arusha nimekula msosi karibia fancy restaurants zote town.

Mimi si tajiri lakini nimejaribu aina nyingi sana za vyakula.

Kuanzia Mexican food, Chinese food, European, Indian, Italian food

Kwenye kutembelea restaurants tofauti tofauti nimegundua restaurants nyingi hawana option ya vyakula navyopendelea zaidi.

1.Tofu

2.Vegan Lasagne

3.Felafel in Pita bread (vegan)

4. Vegetable Satay

5. Tacos (hii labda Mexican restaurants)

6. Vegetable dumplings na vyakula vingine vichache.

Labda sababu ni vegan dishes na watu wengi si plant based.

Ukienda na mimi kupata msosi nitakuonyesha aina ya vyakula hujawahi sikia achilia mbali kujaribu.

Hiyo Ketchup ni vitu vidogo tu vyakujua kama upo na mwingiliano na foreigners especially Americans.

Ni kama vile mnasema chips wao wanaita French fries.
 
Hahhahahahhaha mbona kuliarrest
 
Hiyo yote hamtaki kuja vijijini kulima.
Njooni mashamba yako mengi sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…