Unaepuka vipi kuwa "Chikunde" ukiwa unadate na mtu mambo safi?

Unaepuka vipi kuwa "Chikunde" ukiwa unadate na mtu mambo safi?

t
Acha basi, unaona kabisa nilivo chikunde, kweli niwe wakishua???
ena wewe mboga 12 maharage na kabichi, kachumbali, hazihesabiki. ice cream haikauki kwanu! mlo kwenu unaanza na supu na mikate.
utaweza wewe wali maharage?
 
Napenda sana hao dagaa nikiwa Dar huwa haipiti wiki lazima nikiwaona mtaani niwatafune.
Acha kabisa aiseee.

Maisha ya uswazi ukiwa na buku 2 siku imepita.

Unanunua fungu moja la dagaa mchele unaligawa mara mbili, nusu unakula mchana nusu nyingine unamalizia jioni.
Ukiona vipi kama appetite imekata unaongezea na kachumbali silingi 400 tu inatosha,
Unanunua nyanya za mia 2 na kitunguu cha mia 1 na karoti moja ya 100 siku imepita.

Nimeyamisi sana hayo maisha aiseeee.

Niliwahi pia kukaa kule kinondoni shamba, nilikula sana utumbo wa kuku.
Jioni tunayoosha miguu kuelekea msasani kule kuosha macho kwa kuangalia machangu wakijiuza, ukichoka unarudi kulala geto.

Maisha ya uswazi safi sana.
 
I'm a big time fun of plant based food.

Hapa Arusha nimekula msosi karibia fancy restaurants zote town.

Mimi si tajiri lakini nimejaribu aina nyingi sana za vyakula.

Kuanzia Mexican food, Chinese food, European, Indian, Italian food

Kwenye kutembelea restaurants tofauti tofauti nimegundua restaurants nyingi hawana option ya vyakula navyopendelea zaidi.

1.Tofu

2.Vegan Lasagne

3.Felafel in Pita bread (vegan)

4. Vegetable Satay

5. Tacos (hii labda Mexican restaurants)

6. Vegetable dumplings na vyakula vingine vichache.

Labda sababu ni vegan dishes na watu wengi si plant based.

Ukienda na mimi kupata msosi nitakuonyesha aina ya vyakula hujawahi sikia achilia mbali kujaribu.

Hiyo Ketchup ni vitu vidogo tu vyakujua kama upo na mwingiliano na foreigners especially Americans.

Ni kama vile mnasema chips wao wanaita French fries.
Kaka eee. Haya ndiyo mie nisiyoyataka, mie tukienda huko nitasema nataka ugali nyama fullstop. Hivyo visungu siviwesi atiii. Halafu nawaambia walete ya kushiba siyo unapiga tonge la kwanza lapili unajipindua ukae sawa sahani nyeupe. Hilo siliwezi. Yaani Bora tupite kwanza sehemu nipige vitu vyangu tukienda hapo nikapige mswaki tuuu
 
t

ena wewe mboga 12 maharage na kabichi, kachumbali, hazihesabiki. ice cream haikauki kwanu! mlo kwenu unaanza na supu na mikate.
utaweza wewe wali maharage?
Kweli niwe mboga 12 halafu uma na kisu viniaibishe? Haiwezekani
 
Hahahaha,mmenikumbusha uma na kisu wakati naanza form one,Kwa mara ya Kwanza I nkavikuta mezani.Hamna kijiko ni vyenyewe tu.Dining leader anatangaza huruusiwi Kula na mkono.Nlipata tabu Sana siku za mwanzo.Nkitoka dining shati halifai michuzi ya maarage au makande.

Ni vyema kama kitu ni kigeni kwako ukaomba maelekezo.Kuna watu kuuliza hawataki wanaishia kuabika.Na kama huezi bora kufanya ulivozoea ndo mtu unakua comfortable.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Auntie upo kama mm
Hahahaaaa!! Hebu nicheke kwanza.
Yaani naviweka viuma hivyo pembeni namsosomora kuku kama sina akili nzuri, siwezagi kupretend walah. Menu kama siielewi namwambia tu "hapa nimetoka kapa ndio vinini hivi!!!"
 
Hahhahahahh umenikumbusha chikunde
Yaan mm jamani kula na uma na kisu vimenishinda nakulaga na mikono acha tu nionekane wa uswazi

Shualina,

Kwani kula kwa mkono ni ushamba/ jambo la kiswazi?

Mbona hata huko kwingine watu wa kada zote hula kwa kutumia mikono!

Hakuna ubaya wowote ule kwa mtu kula kwa kutumia mikono yake.

Kwanza ndo moja ya kazi za mikono.

Na wala si ushamba.

Ushamba ni kushikilia dhana potofu kwamba kula kwa kutumia mikono ni ushamba.
 
Shualina,

Kwani kula kwa mkono ni ushamba/ jambo la kiswazi?

Mbona hata huko kwingine watu wa kada zote hula kwa kutumia mikono!

Hakuna ubaya wowote ule kwa mtu kula kwa kutumia mikono yake.

Kwanza ndo moja ya kazi za mikono.

Na wala si ushamba.
Ngabu wengine wanaona ushamba ile umeletewa uma na kisu unaviweka pembeni mm kiukweli vimenishinda acha nijilie tu na mikono yangu

Aliyekuteka anakufanya usionekane akuachie achie kidogo Ngabu
 
Hii mitoko bhn kunasiku niliwaambia washkaji hii misosi yenu mie sishibi kabisa niliwaleta uswazi wakapiga chipsi za uswazi waka zisifia kinoma yaani ndio ikawa chimbo lao nikaja tena kuwalisha miguu ya kuku wanabaki tu kusifia kumbe ndio mitamu hivi,halafu wanashangaa bei chee msosi wa kusaza kisha wananiona mimi nalalamika wametupunja
Umeuwaaa
 
Back
Top Bottom