Kinywa kinachosafishwa mara mbili kwa siku, ni nadra kutoa harufu inayokera. Labda kama ana magonjwa mengine ya kinywa.
Ukimaliza kupata mlo, sukutua mdomo wako na maji safi. Unaweza kutumia MouthWash kwa ajili ya kuua vijidudu. Mouthwash hiyo ni rahisi sana kubebeka iwe kwenye gari ama begi lako, hata vipochi vya wanawake. Zipo madukani zimejaa, pia kwenye maduka ya dawa.
Lakini muhimu sana ni usafi wako wa kinywa. Safisha meno yako vizuri pande zote, sugua ulimi taratibu. Watu wengi sana kinywa wanaparua tu, huwezi kutumia dakika moja kisha useme kinywa chako sasa kimetakata. Kunywa maji mengi. Epuka kutafuna vitu vyenye sukari nyingi.