Unafanya nini kuhakikisha kinywa chako hakitoi harufu mbaya?

The Eric

JF-Expert Member
Joined
Feb 23, 2019
Posts
6,446
Reaction score
10,976
Salaam!

Ni njia zipi unatumia kulinda usafi wa kinywa chako na kufanya mdomo usitoe harufu.

Kuna kuswaki kila baada ya mlo lakini wakuu imagine unaswaki asubuhi na jioni during day ila tambua kuna ile umepata breakfast then mchana lunch alafu mdomo unabaki bila usafi wa uhakika.

Kuna harufu iliyopo kiasili kwa kinywa au wengine meno yanalika na wadudu au kupekechwa hivo harufu lazima izidi.

Does there any solution or medical care to carry out this problem.....

Mawazo yenu yanahitajika.
 
Kinywa kinachosafishwa mara mbili kwa siku, ni nadra kutoa harufu inayokera. Labda kama ana magonjwa mengine ya kinywa.

Ukimaliza kupata mlo, sukutua mdomo wako na maji safi. Unaweza kutumia MouthWash kwa ajili ya kuua vijidudu. Mouthwash hiyo ni rahisi sana kubebeka iwe kwenye gari ama begi lako, hata vipochi vya wanawake. Zipo madukani zimejaa, pia kwenye maduka ya dawa.

Lakini muhimu sana ni usafi wako wa kinywa. Safisha meno yako vizuri pande zote, sugua ulimi taratibu. Watu wengi sana kinywa wanaparua tu, huwezi kutumia dakika moja kisha useme kinywa chako sasa kimetakata. Kunywa maji mengi. Epuka kutafuna vitu vyenye sukari nyingi.
 
Umeeleweka asante daktari
 
Back
Top Bottom