Unahitaji mtoto wa Kambo au Kumuasili?

Asante kwa huo muongozo kutoka serikalini,
Kuna maswali machache ningependa kukuuliza,
1. Ningependa kujua, je kisheria serikali inaruhusu ku adopt mtoto mwenye umri kuanzia miaka mingapi?
2. Endapo ume adopt mtoto kumbe mzazi wake yupo kimya tu, badae mtoto amekua mkubwa mzazi wa huyo mtoto akaja muhitaji Sheria inasemaje?
3. Kwa wale ambao wanatafuta watoto kwa njia ya In vitro fertilization (IVF) Sheria inasemaje endapo mhusika wa mtoto au watoto akatumia surrogate mother na kumlipa??
 
Aleikum Salaam, shukrani 🀲
Naomba jibu ya swali langu, mnapotoa taarifa au kuanzisha mijadala kwenye jamii ni vizuri muwe mmejiandaa kujibu maswali katika nyanja tofauti,
Kuna vitu vingi ambavyo jamii inahitaji kuelimishwa hasa jambo la In vitro fertilization (IVF) lakini hadi sasa hakuna muongozo wa kisera toka serikalini ili hali sasa Kuna hospital nyingi zinatoa hiyo huduma sasa hapa nchini
Maswali niliyouliza kwenye post # 45 ni
1. Ningependa kujua, je kisheria serikali inaruhusu ku adopt mtoto mwenye umri kuanzia miaka mingapi?
2. Endapo ume adopt mtoto kumbe mzazi wake yupo kimya tu, badae mtoto amekua mkubwa mzazi wa huyo mtoto akaja muhitaji Sheria inasemaje?
3. Kwa wale ambao wanatafuta watoto kwa njia ya In vitro fertilization (IVF) Sheria inasemaje endapo mhusika wa mtoto au watoto akatumia surrogate mother na kumlipa??
 
Asante muheshimiwa, ila kuna urasimu mwingi sana. Kuna ndugu yangu aliambiwa lazima awe na milioni ishirini kwenye account ndio aweze kuasili. Yeye ni muajiriwa tu wa serikali kuipata hiyo hela ni ngumu, ila uwezo wa kutunza mtoto anao.
Tunaomba muheshimiwa toa tamko kwa idara zote husika, wasifanye mambo kuwa magumu. Wafanye due diligence yao na kufuata all the necessary procedures bila kumkatisha tamaa mtu mwenye nia njema ya kuasili.
 
3. Kwa wale ambao wanatafuta watoto kwa njia ya In vitro fertilization (IVF) Sheria inasemaje endapo mhusika wa mtoto au watoto akatumia surrogate mother na kumlipa??
Hii kitu mpya tusaidie kuielewa vizuri mkuu
 
Hii ni solution Kwa Wanandoa wenye changamoto ya kupata watoto.

Mnaweza mkakubaliana na Mkeo, mkaenda kum-adopt mtoto wa miezi kadhaa then mkamlea na kumfanya wa kwenu.

Kama litafanyika Kwa upendo, inaweza kusaidia kupunguza watoto wa mitaani ambao wamekosa huduma na Walezi.

Wale ambao wataguswa kufanya hivyo vyema mkawahi mapema.

Dini iliyo safi, isiyo na taka mbele za Mungu Baba ni hii, "Kwenda kuwatazama yatima na wajane katika dhiki yao, na kujilinda na dunia pasipo mawaa"

Yakobo 1:27
 
Hii kitu mpya tusaidie kuielewa vizuri mkuu
Hii inatumika kwa watu wasio na uwezo wa kupata mtoto, labda mwanaume hawezi kutungisha mimba au mwanamke hana uwezo wa kupata ujauzito kwa sababu kadhaa.
Hivyo wanakubaliana kupandikiza ujauzito kwa njia za kisayansi hiyo njia ndio inaitwa In vitro fertilization (IVF) sasa Kuna namna mwanaume anaweza kutumia mayai ya mwanamke mwingine na ujauzito ukabebwa na mwanamke mwingine.
Hili jambo linafanyika sana katika hospital nyingi hapa Tanzania sasa, ila hadi sasa hakuna sera au Sheria kuhusu hili jambo au kama hizo sera na Sheria zipo basi ni vyema wananchi wakajulishwa na kuelimishwa
 
Hongera sana una karama ya kipekee, nahisi umelelewa na wazazi wenye kumjua Mungu vilivyo, itapendeza ukiwa balozi wa kuwawezesha watu wengine kuwa na moyo wa upendo wa kiasi hicho

Ubarikiwe sana mkuu
 
Asante sana Mheshimiwa na sisi tuliozaa nje ya ndoa Ila wake zetu hawajui utaratibu upoje?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…