Unahitaji mtoto wa Kambo au Kumuasili?

Asante sana kwa hii elimu sikuwahi kujjua kama sayance imefika huko, vipi DNA itasoma takwimu za mwanamke yupi kati ya hao wawili
 
Asante sana kwa hii elimu sikuwahi kujjua kama sayance imefika huko, vipi DNA itasoma takwimu za mwanamke yupi kati ya hao wawili
DNA itasoma kwa mwanamke alietoa yai, ila wataalam wataelezea zaidi
 
Tunahofia wake zetu wakijua patatimka hapo nyumbani. Hakuna namna ya kumfunga mdomo bi mzuri?
Hukumuhofia wakati unamsaliti uje kumuhofia tayari ushaleta kiumbe duniani??
Chukua mtoto wako lea yy hata akinuna akipasuka haiwezi kubadili ukweli ww una mtoto na ulimsaliti.! Kingine unamnyima mtoto haki zake za msingi na yy hakukutuma umlete ni shobo zako.
 
Hii thread nilikua naisibiria kwa hamu sana, ngoja nimalize kibanda changu then nianze mchakato, plan ni ku adopt mmoja tuu na jukumu langu kubwa ni kimlea kama sehemu ya familia yangu, Mungu baba nipe nguvu kweny hili...asante....
 
Me naomba mh uniasili mimi niwe mwanao wa kambo
 
Samahani dokta gwajima nipo nje ya mada nilikua nauliza hivi bado unajifukiza kama kipindi kile cha korona na je ina msaada gani na madhara ki afya
 
Ahsante Sana kufuatilia mjadala huu na kuchangia. Tumetoa namba hizo za call center za wizara Ili kama ikitokea tumechelewa kuona hapa basi fuatilieni kwenye namba hizo.

Ufafanuzi kwa ufupi;

1. Sheria imeruhusu kuasili mtoto wa umri wowote ila limitation ya umri imewekwa kwa waombaji/adoptive parents (mwombaji mwenye umri wa kuanzia miaka 50 ataruhusiwa kuasili mtoto wa kuanzia miaka 10 na mwisho wa kufanya applications ni miaka 65).

2. Ikitokea mzazi amejitokeza kwa ajili ya kuasili, Mahakama ndiyo imepewa mamlaka hivyo, atawasilisha kesi yake Mahakamani ambapo, Kamishna wa Ustawi wa Jamii atashirikishwa kwenye kufanya tathmini kwa sababu ndiye aliyetoa kibali cha kuwasilisha shauri Mahakamani baada ya kipindi cha malezi ya Kambo kwisha.

3. Ikumbukwe, kabla ya kuruhusu mtoto kuwekwa kwenye malezi ya Kambo Afisa Ustawi wa Halmashauri amepewa jukumu la kufanya uchunguzi wa kina kwa ushirikiano na Polisi ili kujidhirisha kwamba hakuna mzazi na kama Kuna mzazi ridhaa ya kisheria inatakiwa ya mzazi ila wakati mwingine kutegemeana na mazingira ya mzazi au mlezi Kamishna au Mahakama inaweza isihitaji ridhaa mfano, kama mzazi ana changamoto ya afya ya akili au amemtelekeza mtoto.

Kuhusu IVF; mpaka Sasa suala la IVF au surrogacy haijaingizwa kwenye Sheria ya Mtoto. Tutawasiliana na wizara husika.

Shukrani, πŸ™πŸ½
 
Kifupi alidanganywa, angeibiwa, huo ni utapeli na ula rushwa. Hakuna malipo. Kama Yuko tayari anitumie ujumbe tuchunguze Ili aliyeomba hizo hela achukuliwe hatua. Hapa nahitaji ushirikiano wako tafadhali.
 
Ahsante Sana kwa kujitoa kuelimisha, huu ndiyo ushirikiano wa wadau πŸ™πŸ½
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…