Unaikumbuka zawadi ya kwanza uliowahi kumpa/kupewa na mpenzi wako wa kwanza?

Nakumbuka miaka hiyo ya 2000 mwanzoni.
Nilikuwa na mchumba nikiwa secondary wa kuitwa Felista Mapunda, mrembo wa kishua huku Mimi nikiwa digidigi tu wa mtaa. Nakumbuka siku Moja aliniletea kadi ya Christmas ukifungua ilikuwa inapiga ringtone tamu sana. Siku Moja Maza akaingia ghetto akaikuta Ile narudi kutoka shule naikuta kaiweka sebureni na akaniambia nisijichanganye kuitoaπŸ˜„
 
Dah! Manzi alikupenda mkuu!
Mimi nakumbuka, nikiwa form six, nimewahi mzawadia mtu flani, kidani "bracelet" safi angavu cha kuitwa "Le couer de la mer".
Mpaka leo waga abaniambia ndio zawadi yake kubwa amewahi pewa na mwanaume! 😊
Huyo ndio mama wa mtoto wangu na hiyo saa alinizawadia siku ya send off yake, mtoto na hiyo saa ndio zaidi pekee kutoka kwake za thaman kubwa sana kwangu , japo saa imeharibika ila nimeitunza tu.
 
Niko sawa Mkuu, kwani Mzee Baba wewe nawe ulipiga goti?

Siwezi mkuu, wakati namchumbia shemeji yako (Mke wangu), kulikuwa na hiyo session ya kuvishana pete, mimi nilisimama muda wote, wakati navisha na wakati navishwa.
MC wa tukio lile si akamwambia msindikizaji wangu aniambie nipige goti, nikamwambia achana nae asitumudu. 😁
 
Thanks Brother....Hata mimi nilisimama kama mlingoti.
 
Mwaka 2008, alinipa kadi fulani ina Slide chini juu, kwa chini ina picha ya msichana juu ina maandishi.

Ilikua nzuri sana na niliyo ipenda.
Japo tuliachana ila mpka leo ninayo zaidi ya miaka 15 sasa
 
😊ulianza vizuri bro
Hatukudumu hata. Alihamia shule nikamuwahi ila akawa na mambo mengi tukaachana na alikuwa anapenda sana hela.
Kumbe alihama shule kisa alitoa mimba. Baadae nikasikia alifanya kazi lounge moja iko Kigamboni, akapata mtu pale wakaoana. Unfortunately hawakutimiza 2 years anniversary wakaachana.
 
Dah! Manzi alikupenda mkuu!
Mimi nakumbuka, nikiwa form six, nimewahi mzawadia mtu flani, kidani "bracelet" safi angavu cha kuitwa "Le couer de la mer".
Mpaka leo waga abaniambia ndio zawadi yake kubwa amewahi pewa na mwanaume! 😊
Ajitafakari
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…