Unaita mashahidi ambao unajua fika watakukandamiza. amakweli Lisu kachanganyikiwa.

Yule jamaa ni mhuni sana lazima amejipanga kwa lolote hawezi waita bila kujipanga
 
Mimi sio mwanasheria ila nimewaza na kuona anacho kifanya Lisu ni kujipalia mkaa wa moto usoni. Unaitaitaje walio kushitaki na kukulalamikia eti waje kukutetea?
hata kama ni mtego....sio huo.
Heshimu taaluma za watu, kumbe wewe ni kama Mimi hujui chochote kuhusu Sheria, sasa kaa kwa kutulia maana aliewataka hao watu ni msomi wa Sheria na wakili.

Mimi na wewe tusubilie tupate darasa. Tupunguze ujuaji kwa vitu tusivyokuwa na taaluma navyo.
 
Jamaa siyo mzima, alidhani hawatakuja sasa watakuwa mashidi dhidi yake maana watakubali ni kweli akifanya uhaini na hawezi kuwauliza maswali ya wao waseme hakufanya uhaini.
Nadhani wewe ndio umechanganyikiwa. Mahakama imesema mwenye jukumu la kuthibitisha uhaini ni Jamhuri. Swali, je akina IGP na CDF wanaenda kama Jamhuri au kama mashahidi wa Lissu?. Muwe mnaisikiliza mahakama inapo ongea. Pia kinachobishaniwa kwa Sasa ni je Yale maneno yalilenga uhaini, je kulikuwa na mipango ya uhaini imepangwa? Ndio mahakama inapambania kwa Sasa.
 
Sasa wewe ndio umefafanua vzr lengo la Lissu
 
Maswali ya Cross examination utakayomuuliza shahidi wako ni tofauti na utakayomuuliza mshitaki wako.
Hawezi kuwabishia mashahidi wake wakisema ni kweli ndugu Yao akifanya uhaini.
Sikiliza wale ni mashahidi wa Lissu hata kama ni hostile na Lissu atawaoongoza kwenye examination in chief na wao watawafanyia cross examination Sasa Lissu atarudi kuwafanyia re examination.
 
Polepole, Nchimbi NK wako wapi? Hakuna anayejali Hadi Leo.
Na Lissu atafungwa na hakuna atakayejali pia. Kelele masaa mawili tuu basi anasahaulika.
Labda wewe ndio umesahau polepole na Nchimbi. Halafu issue ya Lissu ni tofauti. Kwa mara ya kwanza mtuhumiwa wa uhaini anapata support ya public. Kasome kisa cha akina Captain Maganga walitaka kupindua serikali Hadi ndugu walimtenga kabisa.
 
Kama haujui kuwa hao mashahidi wataongozwa na Lissu kuhojiwa nyamaza.
Binafsi mimi si mjuzi wa sheria,jambo hili la kuwaita CDF,IGP..... linanitia uoga.

Nafahamu kwamba Lissu ataongoza kuwahoji lakini pia Wanasheria wa serekali watapewa nafasi ya kuwadodosa.

Tuombe yaishe salama.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…