Unajisikiaje kumuona binti chuoni hapati mahitaji kisa hana pesa?

Unajisikiaje kumuona binti chuoni hapati mahitaji kisa hana pesa?

Mkuu hii mada imenikumbusha maisha anayoishi kijana mmoja mwanachuo,ni yatima pia ndugu zake hawana support yoyote kwake.Anaishi kwa shida sana, kwa siku anakula mlo mmoja tu.Hana mkopo,alipomaliza form four alipata div one akaamua kujiunga na chuo kwa ngazi ya diploma.

Alipata wasamaria wawili wa kumlipia ada kwa muda wote wa miaka mitatu ya masomo yake.Shida kubwa ipo kwenye gharama za menyu & stationary.Ana jitihada sana hata masomo yake anapata A,ila waswas wangu ni performance yake inaeza kushuka kutokana na hz changamoto anazokutana nazo.
 
Mkuu hii mada imenikumbusha maisha anayoishi kijana mmoja mwanachuo,ni yatima pia ndugu zake hawana support yoyote kwake.Anaishi kwa shida sana, kwa siku anakula mlo mmoja tu.Hana mkopo,alipomaliza form four alipata div one akaamua kujiunga na chuo kwa ngazi ya diploma.Alipata wasamaria wawili wa kumlipia ada kwa muda wote wa miaka mitatu ya masomo yake.Shida kubwa ipo kwenye gharama za menyu & stationary.Ana jitihada sana hata masomo yake anapata A,ila waswas wangu ni performance yake inaeza kushuka kutokana na hz changamoto anazokutana nazo.
Mtu wa hvy akitusua ndugu zake wataleta matercall yao nsaidie nsaidie pumbav
 
Nikiona habari kama hizi huwa nakumbuka jamaa mmoja alikuwa anahangaika na maisha akiwa analea watoto wake baada ya mama yao kufariki
Alipambana na mmmoja wa watoto wake wa kike akafanikiwa kufika chuo kikuu
Jamaa alikuwa na furaha sana na kusema nimepambana haswa ila mwaka wa pili msichana karudi home kwao mjamzito

Aliponiambia roho iliniuma sana ila alikuwa strong na kuikubali hali ile
Dah!!!,hapo ndipo watoto wa kike huwa wananichosha.
 
On a Serious note kama unawafahamu wa hivyo nipe address zao. Ni kwa wema tu mkuu
Nenda kituo chochote cha yatima ukatoe msaada. Kama hujui vilipo sema hapa tukutajie makumi ya vituo vya yatima na wazee.

Kama unataka kusaidia katika elimu ya chuo. Pitia kwa dean ana list ya wanafunzi wanaosuasua fedha hasa vyuo private
 
Tatizo watoto wa kike nao ni pasua kichwa sana. We utadhani ana mawazo ya maisha yake kumbe anamuwaza boyfriend wake tu sio maisha wala nini. Na wengine wakishaanza kupendeza full kunata na kuiga maisha ya wenzao.
Hoja ya msingi.
 
Pale Ardhi, nilikutana na binti amekesha studio anaandaa michoro, akaniomba mia tano. Nilimpa hela yote niliyokua nayo siku hiyo.

Hawa watoto wa kike bana, kunyanyaswa sababu ya shida ni rahisi kuliko sisi vidume. Bora umpe mahitaji yote muhimu, ili akifanya ufuska iwe ni kwa ridhaa yake mwenyewe!
 
Kuna rafiki angu nae yupo SAUT, kajifungua karibuni hivi, [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Kuna mdogo wangu anamalizia dip ila kozi yake wamejaa wazazi wakati age yao wengi ni 19-20. Uvaaji wao sasa nao ni utata kupindukia. Kila nikimpigia simu mara ameshika mtoto wa nani, marafiki zake wengi nilikuwa nawamezea wamwjifungua.
Hasa wale wa Education wanajifungua balaa. Wanataniwa na kozi nyingine kuwa wanaamua wazae wanafunzi wao wenyewe.

Mimi course yangu mpaka mwaka huu wa pili namjua mmoja tu aliyejifungua.
 
Hii ya mimba imetokea juzi tu kwa jirani yangu, kuna binti yake anamsomesha kwa hela ya kudunduliza lakini mwanafunzi kapachikwa mimba na wahuni, halafu cha kuumiza zaidi binti hana mkopo.
Nikiona habari kama hizi huwa nakumbuka jamaa mmoja alikuwa anahangaika na maisha akiwa analea watoto wake baada ya mama yao kufariki
Alipambana na mmmoja wa watoto wake wa kike akafanikiwa kufika chuo kikuu
Jamaa alikuwa na furaha sana na kusema nimepambana haswa ila mwaka wa pili msichana karudi home kwao mjamzito

Aliponiambia roho iliniuma sana ila alikuwa strong na kuikubali hali ile
 
Back
Top Bottom