Mkaruka
JF-Expert Member
- Feb 5, 2013
- 19,629
- 34,199
Chuoni hakuna sababu ya kushindana GPA. Mimi nimesoma chuo ambacho hostel ni kama Almas, mwaka wa tatu niliuza kitanda nikawa nalala kwa kuvizia na kwenye majengo mabovu.Mkuu hii mada imenikumbusha maisha anayoishi kijana mmoja mwanachuo,ni yatima pia ndugu zake hawana support yoyote kwake.Anaishi kwa shida sana, kwa siku anakula mlo mmoja tu.Hana mkopo,alipomaliza form four alipata div one akaamua kujiunga na chuo kwa ngazi ya diploma.Alipata wasamaria wawili wa kumlipia ada kwa muda wote wa miaka mitatu ya masomo yake.Shida kubwa ipo kwenye gharama za menyu & stationary.Ana jitihada sana hata masomo yake anapata A,ila waswas wangu ni performance yake inaeza kushuka kutokana na hz changamoto anazokutana nazo.
Ada ni Mungu alipita kati tu. Kula tumepika sana na washkaji hostel. Tulinunua rice cooker, hilo hilo tunapikia maharage, ugali, wali, uji 🤣
Hapo bado stress za kukataliwa kufanya papers kwasababu ya ADA. Field nimeenda mkoani nikiwa nina nauli tu ya Tsh 20,000 nimelala sana stand halafu baridi kaliii, asubuhi unaamka kama vile kila kitu kiko poa🤣
Miaka 3 unasota chuo, unamaliza kwa kudra za Mungu unakutana na utawala wa kibwengo Jiwe kila siku anahuburi madaraja tu huku pesa anahonga wapinzani na kurudia chaguzi.
Unaamia kupiga mishe yoyote, naamua kuwa mlinzi Jiwe anazuia fao la kujitoa kwahiyo anafikiri watu wanaweza kufanya hizi kazi mpaka miaka 55?
Unaweza kudhani ni ndoto sometimes.