Unajua kwanini 90% ya wana-hiphop huamini kuwa 2pac ni king wao?

Unajua kwanini 90% ya wana-hiphop huamini kuwa 2pac ni king wao?

Mimi ni shabiki wa 2Pac haswaaa
Big najua nyimbo 2 tu Hypnotize na One more Chance ila niseme ukweli flow ya Big kwenye hizi ngoma ni tamu balaa. Ila kwenye uandishi na vina vyenye maana 2Pc kamuacha mbali sana Big
Wewe umeongea kweli. Big alikuwa mzuri kwa upande wa ku flow ila kwa utunzi wa maana, life style ya kuigwa nk Pac alikuwa far ahead mbele ya Big.
 
Kwanza tujue tunaongelea maisha au mziki?
Kama ni maisha 2pac yupo juu kuliko BIG na ameacha alama kubwa kwasababu ya harakati zake.
Na ndio kinachofanya watu wamkumbuke.

ila tukiishia kuangalia mziki tu purely bila kufuatilia sijui nani alikuwa anapigania haki za kina nani.
BIG kimziki alikuwa anajua kuliko Pac.
Tukiangalia tu flow, style, wordplay BIG yuko juu.
Sema BIG mziki wake haukuwa kiharakati.

Hata saivi tukiangalia kimziki tu 2pac anazidiwa na wasanii wengi wa sasa ila kiharakati bado hawajamfikia.
No nakataa, hakuna msanii wa kumzidi Pac japo wengi wanajitahidi kupita mle mle alipopita Pac aidha kwa kuchomoa baadhi ya maneno katika mistari yake na kuweka katika nyimbo zao nk.
 
Nani anatazamwa zaidi kati ya pac & big?? Tuanzie hapo kwanza..licha kuwa wote walikufa kwa risasi.
Pac is pac 4 ever.
Big ni watu wachache sana wanaomjua. Na ukiangalia hata huko Marekani kwenyew Big jina lake lilisambaa zaidi New York, tofauti na Pac ambae jina lake lilikuwa limesambaa Marekani nzima hasa LA California, Auckland na Ney York.

Kumbuka Pac alizaliwa New York na akakulia huko, lkn alipofikisha umri wa miaka 12, akaondoka kwao na kuhamia katika miji mingine ya Auckland, LA nk. Kwahiyo huko kote alikuwa na jina na alijulikana zaidi ya Big aliezaliwa, kukulia na kuishi maisha yake New York tu peke yake.
 
ITOSHE Kusema huu nyimbo ndio iliyomuua PAC😁
Pac aliuwawa na system. Kumbuka system ilijaribu kumnyamazisha kwa kutumia vifungo mbali mbali vya kesi za kutengeneza, lkn alishindikana. Kwahiyo solution ikawa kumuondoa tu duniani ili serikali ipumue.

2pac alianza kufungwa jela akiwa na umri wa miaka 13 kutokana na harakati zake za kupigania na kutetea haki za watu weusi. Na ndomaana 80% ya nyimbo zake hakuacha kuwataja na kuwatukana polisi ambao ndio system yenyewe ya serikali. Kwahiyo kwa system ya Marekani kipindi kile ilikuwa ukiisema serikali vibaya hasa kwa aina ya mtu kama 2pac ni lazima uwawe tu.

Hiyo ya Big ilitumiwa kama chambo ili serikali itapofanya yao lawama ziende kwa Big na genge lake.
 
Inaonekana zamani walikuwa wanauana na risasi sana, inaonekana kila mtu ana mguu wa kuku Akilihuru
Hata miaka hii si unasikia mauaji yanafanyika kila iitwayo leo. Sema mauaji ya zaman yalikuwa zaidi ni ya wasanii kwa wasanii ila Pac hakuwawa na wasanii wenzake bali serikali ndio ili mset him up. Soma post yang namb #67 hapo juu nimeelezea vizuri tu mkuu.
 
Pac alitrend hata kabla ya Kifo !!!
Achana nao hao vijana walioanza kufuatilia hip hop miaka ya 2000s. Wengi hawajui kitu.

2pac kaanza kujulikana na kufanyiwa mahojiano na wanahabari mbali mbali akiwa na umri wa miaka 17.

Serikali nzima ya nchi kama Marekani ilifikia kipindi mpaka inapambana kuzuia nyimbo zake zisiwe zinapigwa kwenye station mbali mbali za radio na tv, afu mtu anakwambia eti ame trend baada ya kifo.
 
Wamarekan wenyew wanakwambia kuwa toka mziki wa rap ulipoanzishwa mpaka leo, hakuna ngoma ya diss iliyowahi ku hit kama Hit em up.

Hiyo ngoma ukiisikiliza hata leo unaweza kuhisi imerekodiwa jana.
Yani sio tu hakuna, bali haitatokea kamwe katika ulimwengu wa mziki.

Kina 50c na Ja rule waliwekeana beef lkn mwisho wakajikuta wanatumia nyimbo za 2pac kutupiana madongo, na sio kutunga nyimbo zao wenyewe.
 
Sisi tulioanza kufuatilia mziki wa hip hop toka miaka ya 90s tunamkubali sana huyu mwamba. Ukiona mtu anamkataa au kujaribu kumfananisha na wasanii wabovu kama Lil wayne, Eminem, Ja rule nk jua huyo ameanza kusikiliza na kufuatilia mziki wa rap miaka ya 2000s. Huyu mwamba hata kina Big, Nas, Mr P nk walikuwa wamshamshindwa kumdhibiti katika game la mziki.
Unawezaje kumdhibiti mtu ambae unajifunza kwake kuimba na kutunga mistari yako?
 
No nakataa, hakuna msanii wa kumzidi Pac japo wengi wanajitahidi kupita mle mle alipopita Pac aidha kwa kuchomoa baadhi ya maneno katika mistari yake na kuweka katika nyimbo zao nk.
Wewe umelewa mahaba, na hakuna chochote ntakachosema kukubadilisha.

Nitajie wimbo mmoja wa pac unaouzidi huu.
Sing about me im dying of thirst-K.Lamar
 
Haijawahi kutokea kwa msanii yeyote yule duniani qoutes zake kuwa na maana na mashiko kama ilivyo kwa 2Pac na ndio maana vyuo vikuu ndani ya Marekani wanayatumia (Lyrics & quotes).
Hapa umeongea ukweli japo ni wachache sana tena wasiojua mziki ndo watakupinga.
 
Wewe umelewa mahaba, na hakuna chochote ntakachosema kukubadilisha.

Nitajie wimbo mmoja wa pac unaouzidi huu.
Sing about me im dying of thirst-K.Lamar
Hit Em Up imemaliza kila kitu. Hao polisi wenyew na serikali yao walipokuwa wanasikiliza 'out on bail' aliyotoa mwaka 93 akiwa na umri wa miaka 22 tu, walikuwa hawana ham nae alivyowachana vibaya na kuwaambia polisi system yao ya kumuweka ndani ili kumbadilisha imeshindwa, labda watafute njia nyingine za kumdhibiti. Na kweli walimdhibiti kwa kumpiga risasi.

Big hana la maana aliloimba zaidi ya kuruka ruka na kutingisha kichwa tu basi.
 
Haijawahi kutokea kwa msanii yeyote yule duniani qoutes zake kuwa na maana na mashiko kama ilivyo kwa 2Pac na ndio maana vyuo vikuu ndani ya Marekani wanayatumia (Lyrics & quotes).
NI kama Bob Marley kwenye Reggae Kuna waimba Reggae wengi lakini Bob alikuwa wa Tofauti ukija kwenye Hip-hop kuna marapa wengi wakali lakini PAC alikuwa na kitu cha kipekee ambacho mpaka leo ameacha Legacy
 
Back
Top Bottom