Unajua kwanini 90% ya wana-hiphop huamini kuwa 2pac ni king wao?

Unajua kwanini 90% ya wana-hiphop huamini kuwa 2pac ni king wao?

NI kama Bob Marley kwenye Reggae Kuna waimba Reggae wengi lakini Bob alikuwa wa Tofauti ukija kwenye Hip-hop kuna marapa wengi wakali lakini PAC alikuwa na kitu cha kipekee ambacho mpaka leo ameacha Legacy
Hakika wewe unaongea ukweli na uhalisia wa kile tunachojadili hapa.

Wengi hawajui kuwa Pac ndio nembo ya mziki wa Hip Hop kama ilivyo kwa Mohammed Ali masumbwi, Michael Jordan basketball na wengine wengi wa aina hiyo.
 
Huwa nashindwaga kuuelewa u bora wa BIG over 2pac..nimejaribu nimeshindwa
Big alichokuwa anaweza ni kuruka ruka na kutingisha kichwa tu basi, au kidogo kuimba kuhusu maisha yake binafsi hakuna kingine.

Tofauti na Pac ambae aligusia political, ubaguzi wa rangi, aliimba nyimbo ya kuwaasa wazungu na mablack wawe kitu kimoja, wasibaguane maana mbele ya Mungu hakuna rangi iliyokuwa bora isipokuwa ni matendo yako tu ndo yatakuokoa, nyimbo hiyo ni 'CHANGE'.
Ameimba 'Dear mama' ambayo imekuwa kama kioo cha ulimwengu kwa mama zetu wote waliohai na waliokufa mpaka kupelekea kina Christian Bella, Banana Zoro, Mr Nice, GK na wengineo nao kuona umuhimu wa kuimba nyimbo za kuwasifu mama zao (zetu)

Pac aliimba my unborn child ambapo ujumbe wake unatumiwa na wazazi wengi kwa watoto wao kule Marekani maana alitoa usia wa maana sana. Pac aliimba ain't mad cha pia ni ujumbe mzuri sana kwa vijana mabaru baru kutulia na kuweka akili chini ili kujenga maisha yao upya yalioharibiwa na madawa, wizi nk.

Ki ukweli ukona mtu anasema Big ni zaidi ya Pac basi ujue huyo sio mfuatiliaji au mjuaji wa maana ya miziki inayoimbwa na wasanii hao.
 
Wakuu inakuaje, nina amini kila mtu yuko vizuri kiafya au sio wakuu.

Sasa leo nawaletea mada muhimu, na yenye kueleweka vizuri kwa kila mtu atakaesoma thread hii. Mada hii inamhusu rapper maarufu wa muda wote 2pac Amaru Shakur, ambae pamoja na kwamba ameshafariki miaka 26 iliyopita, Lakini mziki wake au ujumbe wake katika mziki unaendelea kuishi.

2pac au makaveli, ambapo wamarekani wenyewe wamempa sifa kwa kumpachika jina la 'The GOAT,' kirefu chake 'The Great Of All Time' (msaani bora wa muda wote) ni msaani aliefanya mambo makubwa katika mziki huo, hadi kupelekea wasanii wengi wakubwa katika mziki huo, walitoka kimziki kupitia baadhi ya mistari waliyoiba au ku copy kutoka katika nyimbo za mfalme huyo wa hip hop au rap. Na wasanii hao walioiba au ku copy kutoka kwa 2pac nimewaweka katika makundi matatu ya A, B na C.

A) Wapo waliotoka kwa ku copy au kuiba beat zake. Wasanii hao ni[emoji116]

1) Jay z ft Beyonce - 'Me and my girlfriend', Jay z aliu copy wimbo huo kutoka katika ile nyimbo ya 2pac ya 'Me and my girlfriend.'
Kwa wafuatiliaji wa mambo ya hip hop bila shaka washawahi kuzisikia nyimbo hizi. Na ikumbukwe kabla ya 2pac kufa, 2pac na Jay walikuwa na diss (ugomvi) ndo maana 2pac alimchana jay z live katika wimbo wake wa 'Bomb first'

2) Nas - huyu ashawahi ku copy beat ya 2pac afu akaingiza mistari ambayo ilikuwa imechanganywa na baadhi ya mistari iliyo katika nyimbo za 2pac (wimbo nimeusahau) Lakini tofauti na wasanii wengine, Nas ali copy nyimbo ya 2pac huku 2pac mwenyewe akiwa hai.
Pac alipotoka hospital baada ya kutolewa risasi tano alizopigwa, kitu cha kwanza alitunga nyimbo kuhusiana na tukio hilo la kupigwa risasi tano. Sasa baada ya siku chache baadae Nasi nae akatoa ya kwake inayolingana na ya Pac ikiwa na beat pamoja na ujumbe unaofanana na ule wa 2pac, jambo lililopelekea 2pac achukie na kutunga nyimbo ya kumpaka Nas mazima. Wimbo huo unaitwa 'Against all odds' 2pac alimpaka Nas, pamoja na Puffy Daddy live bila kumung'unya mung'unya maneno. Hapo chini naweka baadhi tu ya maneno katika verse ya kwanza akimchana Nas baada ya ku copy kutoka kwa 2pac [emoji116]

[emoji445] This little nigga named Nas thinks he live like me, talking bout how he left the hospita took five like me.
You living fantasies, nigga i reject your deposit[emoji445] Kwa tafsiri isiyo rasmi (Huyu dogo anaeitwa Nas anafikiri anaishi kama mimi, anaongelea kuhusu kutoka hospital baada ya kupigwa risasi tano kama mimi.
Unaishi kwa nguvu za soda dogo, nigga sikubaliani na kile ulichoimba) hapo chini aliendelea kumchana kupitia verse ya mwisho ya wimbo huo [emoji116]

[emoji445] Hey Nas you whole damn style is weak you heard my melody, read bout my life in the papers.
All my run-in with authorities felonious capers now you want to live my life, so what's the deal niggas that don't ride right.
You've seen too many movies, load em up against the wall, close his eyes since you lie, you die, goodbyee.
Let the real life niggas hear the truth from me,
What would you do if you was me nigga (against all odds)

B) wapo waliotoka kwa ku copy tu mistari yake, wasanii hao ni [emoji116]

1) 50 Cent - hail marry, wimbo huu 50 alikuwa akim diss Ja rule, kuna baadhi ya maneno mengi katika verse yake aliyatoa kwenye wimbo wa 2pac wa Against all odds. Ngoja nitawawekea mistari ya 2pac na 50 cent hapo chini muone ninachomaanisha [emoji116]
Verse ya 2pac [emoji117] [emoji445] This little nigga named Nas thinks he live like me, talking bout he left the hospital took five like me.
You living fantasies, nigga i reject your deposit.
Verse ya 50 cent [emoji117] [emoji445] Lil nigga named Ja (Ja rule) think he live like me, talking bout he left the hospital took nine like me. You living fantasies, nigga i reject your deposit.

2) Eminem nae hakuwa nyuma kwenye wimbo huo akaimba baadhi ya mistari ya verse kwenye nyimbo husika wa 2pac (kabla ya hapo Eminem alikuwa anaimba rap katuni, ile ya uchale chale) kwa wafuatiliaji wa ngoma za Eminem kuanzia mwaka 2012 kushuka chini wanafahamu ukatuni wake [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23].

3) Lil Wayne huyu nae ashaiga mengi mpaka kupelekea kutunga nyimbo inayofanana na ya 2pac, alipohojiwa na yeye alieleza jinsi anavyomkubali na kumheshim 2pac hadi kupelekea kutunga nyimbo inayofanana na ya 2pac inayoita 'Keep ya head' wimbo huu 2pac alikuwa ameutunga mahsusi kwa wanawake.
Hili kundi 'B' wapo wengi ila kwa kufupisha mada acha niishie kwa hao wawili.
C) Wapo waliotoka kwa ku copy style ya maisha ya 2pac, aidha kwa kutembea kama Pac, kuvaa kama Pac, kuchora tattoo zinazotaka kufanana na za Pac nk.

Muda kidogo nitakuja na baadhi ya wasanii wakubwa walio copy style hizo nilizoandika hapo juu. Hii inaonesha ni jinsi gani mfalme huyo wa hip hop anavyoheshimika na kukubalika kuliko msanii yeyote wa mziki huo na ndio maana wengi wametoka kupitia nyimbo zake na style zake.
View attachment 2399871View attachment 2399872
Tupac alikuwa na beats zake? Beat karibu zote za hip hop huwa wana-sample toka aina nyingine za muziki so obviously hakuna aliyeiba beat za Tupac.

Tupac alikuwa mkali na kinachomtofautisha na rappers wengi ni passion aliyokuwa nayo. Lyrical deliveries zake ziko very emotional na zinagusa. Pia Pac alikuwa multitalented, that doesn't hurt either. Kwangu mimi Pac ni mkali kuliko Biggie. Is he among the greats? Yes. Is he the GOAT? Lyrically no. In my opinion Nas, Jay, Jadakiss, Mos Def and Rakim wako juu kuliko Pac kwa mashairi.
 
😂😂😂😂 hakwepeshi
Pac hakuwahi kukwepesha. Sikiliza 'Out On Bail' uone au usikie alivyowachana chana polisi, jaji na wanasheria wa serikali tena anawataja live bila kuogopa wala kumung'unya maneno.

Ile ngoma yake ya You wonder why i call you bit..ch alikitolea kimama kimoja cha serikali tena ni kiblack chenzake ambacho kilikuwa kinahamasisha watu na studio za mziki Marekani wasipige nyimbo za 2pac redioni au majumbani.

2pac akamshukia na huo wimbo kibibi kikafunga domo lake, maana alikichana chana vibaya.

Pia kuna ule 'we can't stop' alioimba na kundi lake la outlawz (watoto wa mbwa) akamchana tena yule bibi na makamu wa raisi wa wakati huo, tena kwa kuwataja majina live bila kuogopa system wala mamlaka.
 
Ukiachana na maisha ya u Niga, u hustler na Dis hits jamaa alikua na ma songi ya makali makali sana.

Yan nyimbo ya mapenz ambayo wewe kama mgumu huoni tabu kuisikiliza mbele za watu.
"LITTLE DO YOU KNOW"



Ukweli ni kwamba Marekani nzima bado hajapatikana msanii kama 2pac.
 
mkali tuko mashabiki wa hip hop wngi ila unaonekna una mapnzi yako binafsi na 2pac
Nas hkuwa mkali kipindi icho ila for what NAS has done to this hip hop game up to now Put some respect on his Name
Kila mtu ni mkali kwa muda flani not forever ndo mziki
Nas namkubali pia mkuu. Kwangu mimi nampa nafasi ya pili after Pac, japo kuna watoto wadogo watakuja kukwambia kuwa Nas anashindwa hata na Eminem, Wayne nk.
 
Ni kweli kabisa kuwa 2PAC ATABAKI KUWA MSANII BORA DUNIANI AKIWA NAMBA MBILI NYUMA YA THE NOTORIOUS B.I.G(biggie small)
 
2Pac bhana
"They Got money for war but they can't feed Poor's"
FB_IMG_16461708966915210.jpg
 
Si ndio utuwekee tuone Big ashafanya mangapi mazuri ya kuigwa.
2pac ashaimba nyimbo za maana kama vile
1) Dear mama
2) Change
3) Ain't mad cha na nyingine nyingi za kumtetea mtu mweusi. 2pac ashawahi kuwapiga risasi maafisa wa polisi wawili kwa kisa cha kumkamata kijana mdogo mweusi na kuanza kumpa kipiga bila sababu. Kitu ambacho kilimuuzi 2pac aliekuwa anapita na kuwamiminia risasi, 2pac alifungwa kesi hii na baadae aliachiwa baada ya wale maofisa kuonekana walifanya kazi yao kinyume cha sheria. Kwamba washamfunga dogo pingu afu bado wanamshushia kipigo. So Big ashafanya yapi ya maana au nyimbo ipi ya maana kuhusu haki za watu weusi, jamii yake au hata kumuimbia mama yake.
Dear mama kila mwaka ikifika ile sikukuu ya mother's day huwa inapigwa na studio za dunia nzima, sasa Big yeye kaimba kipi cha maana cha kukumbukwa? Au wewe unasikiliza mdundo tu haujui maana ya kilichoimbwa?
Uongoooooooo......
 
Tupa qumerr tu..Msikilize notorius B.I.G
Tupa alibamba kwasababu ya lifestyle yake, ila kimziki yani punch to punch, mistari mikali, biti kali, style kali...tupa hamgusi BIG hata kwa mbali
Nikumbushe hv ameuza record ngapi vile huyo notorious BIG na jumla ana nyimbo ngapi...movie je anazo ngp vile nikumbushe tu....Tuzo je? Vp kuhusu ile museum ya Tupac Wake me when I'm free na vp kuhusu ile siku inayoazimishwa ya 2pac
 
Back
Top Bottom