Unajua Mungu aliumbwa na nani?

Unajua Mungu aliumbwa na nani?

Kwanini iwe ni lazima kujua majibu ya ulimwengu na kifo ili kuipinga dhana ya uwepo wa Mungu?

Unajua kuwa tunaweza kujua uongo wa kitu bila kujua ukweli halisi ni upi?
Uongo unafutwa na ukweli, kama ukweli haupo uongo unabaki sehemu ya ukweli mpaka ukweli utakapokuwa wazi. Kwa sasa Ukweli uliopo ni uwepo wa MUNGU kama ni uongo njoo na ukweli uliosababisha huo Uongo uwepo na utafutika. Kinyume na hapo ni kupoteza muda.

Kwann mtu anayeamini uwepo wa MUNGU aamini hayupo sababu mtu mmoja dhaifu anayekisubiri kifo na asiyejua kifo ni nn, asiye na jibu kuhusu sababu na chanzo cha uwepo wa ulimwengu kasema?
 
Mimi kutokujua mechanisim hizo zilianzaje kunafanya muanzilishi awe ni mungu?
Binafi sjamtaja muanzilishi wa hizo mechanism ila nmekuuliza hizo mechanism ziliwekwa na nini au nani ?
 
Kijana unatikisa mbuyu umejikuta unatikisa makalio yako mwenyewe.

Hata kama huamini achana na hilo DUDE linaloitwa MUNGU. Lipo nje ya uwezo wako kulielewa.

tafuta muda wa peke yako, uyaangalie mazingira yako milima na mabonde, nyota angani, wanyama, samaki, wadudu, ndege, n.k (angalia usiku na muda wa mchana)

Utaanza taratibu kugundua kuwa kumuamini MUNGU inahitaji kuuvua huo ujuaji wako.

tuliza akili kijana!
Sasa na yeye Mungu kwanini ajiweke complex hivo? Kwann asirahisishie maisha viumbe wake kama mtoa mada ili wamwelewe kiwepesi.
 
Na uzima wa Milele ndio Huu, Wakujue Mungu wa pekee wa kweli na Yesu Kristo uliyemtuma.

Yohana 17.3.

Ila Quran.
Imeandikwa na Jesuit+ Mohamed+ Shetani+ Majini.

MJUE SANA MUNGU.
SOMA SANA BIBLIA.
 
Mungu hakuandika kitabu kama unavyojidanganya Aya ndo zilikuwa kama maneno yake yalitufikia kupitia malaika. Mwanadamu kadri zama zilivyoenda ndo baada ya ummah (kizazi) kile cha mitume, wakaja maswahaba, tabii, tabi tabiina, ile series mpaka kufika kwetu ndo itabidi wafanye ukusanyaji za vile Aya ndo wakaweka kweny vitabu.

Unaweza kusoma hata historia ya kutoka fasihi simulizi mpaka fasihi andishi..

Qur an kwa mda husika na Aya zilivyoshuka mpaka kumfikia mtume kupitia malaika ipo vile vile. This is why tunasoma kama ilivyo unapoitafsiri kwa kupeleka katika lugha nyingine a bit of semantic will be missed. Ndo maana tunasoma kama ilivyo ili isipoteze maana.
 
Utoto wako umeanza kwa kusema Mungu ameumbwa na mwanadamu na nikikuuliza binadamu ametoka wapi au kaletwa na nani?? Si ndo utaniletea hoja za mtoto wa chekechea.
Umeniuliza swali hilo?
 
Umewahi kujiuliza ni nguvu ya aina gani inayotumika kumfanya mwanadamu alale au asinzie usiku??
Hakuna nguvu inayohusika kwenye usingizi.

Labda kama sijaelewa unavyosema nguvu unamaanisha nini.
 
Wewe mwenyewe ullikujaje duniani?

Ikiwa Mungu aliunbwa wewe, wewe mwenyewe uliumbwa na nani?

Huna jipya ndugu, Mungu yupo jana leo na hata milele.

Acha upumbavu
Umeelewa hoja yangu vizuri?

Mimi sijui chanzo cha uhai ni kipi. Wewe unakijua?
 
Mimi ni kijana ambaye Kwa muda wa miaka 2 nimekuwa nikifatilia mijadala mbalimbali hapa Jf katika jukwaa hili la intelligence. Moja ya mijadala ambayo imekuwa ikinivutia sana ni hii ya dhana ya uwepo wa Mungu.

Swali kubwa ambalo nimeku wa nikijiuliza ni " Mungu alitoka wapi"

Baada ya kuisoma sana biblia na Quran pamoja na kuwahoji viongozi mbalimbali wa dini, hatimaye nikapata jibu la swali lililonitatiza muda mrefu, Mungu alitoka wapi?

Nimegundua kuwa muumba wa Mungu ni mwanadamu. Yes mwanadamu kama Mimi na wewe ndiye aliyemuumba Mungu.

Kwanini nimefikia hitimisho hilo?

Vitabu tunavyoaminishwa kuwa ni vya Mungu mkuu asiyeshindwa na kitu ( biblia & Quran) ni vitabu vyenye makosa mengi sana ya kimantiki na habari nyingi zenye utata, jambo ambalo tusingetegemea liwepo katika kitabu kilichoandikwa kwa muongozo kutoka kwa Mungu mkuu mwenye uwezo asiyeshindwa na kitu.

Uwepo wa habari hizo zenye utata zinadhihirisha moja kati ya mambo yafuatayo.

1. Mungu hana ukuu tunaoambiwa ndio sababu ameshindwa kutoa mwongonzo mzuri katika kuandika kitabu kisicho na makosa ya kimatinki.

2. Habari hizi ni zao la fikra za mwanadamu aliyeishi katika zama za giza na ujinga. Mwanadamu ambae alitaka kutafuta majibu mepesi katika maswali magumu yaliyomzunguka ndio sababu zina utata.

Kama jibu ni 1 basi Mungu mkuu asiyeshindwa na kitu hayupo Bali aliyepo ni dhaifu na mbabaishaji aliyeshindwa kuandika vizuri kitabu kinachomuelezea yeye mwenyewe.

Kama jibu ni 2 ,basi Mungu mkuu asiyeshindwa na kitu hayupo ndiyo sababu akatokea mtu akatunga habari kutokana na fikra zake mwenyewe. Angekuepo asingeruhusu magepu katika fikra za mwanadamu ambayo yamepelekea mwanadamu huyo kujitungia majibu mepesi na habari zenye utata ili kuziba hayo magepu katika fikra zake.

Pointi zote mbili utaona zinaonyesha kuwa Mungu mkuu asiyeshindwa na kitu mjuzi wa yote hayupo Bali " ama aliyepo ni dhaifu,mbabaishaji na asiye na uelewa wowote kuhusu ulimwengu, ama dhana nzima ni hadithi ya kutungwa katika fikra za mwanadamu aliyeishi katika zama za ujinga na kukosa access ya taarifa mbalimbali.

Nawasilisha.
Ungeweka kwanza hayo makosa yaliyopo kwenye quran kisha tuendelee
 
Vijana wakishavuta bangi lazima waanze kuchachawa
Huyu kijana hata ukitaka kumuelesha bado ataleta ujuaji mwingi

Basi muacheni anachoona yeye na akili zake

Maana huyu sio wa kwanza kumletea mungu dhihaka na wala hatakuwa wa mwisho.
 
Mungu hakuandika kitabu kama unavyojidanganya Aya ndo zilikuwa kama maneno yake yalitufikia kupitia malaika.. Mwanadamu kadri zama zilivyoenda ndo baada ya ummah(kizazi) kile cha mitume ,wakaja maswahaba, tabii,tabi tabiina ,ile series mpaka kufika kwetu ndo itabidi wafanye ukusanyaji za vile Aya ndo wakaweka kweny vitabu.

Unaweza kusoma hata historia ya kutoka fasihi simulizi mpaka fasihi andishi..

Qur an kwa mda husika na Aya zilivyoshuka mpaka kumfikia mtume kupitia malaika ipo vile vile..This is why tunasoma kama ilivyo unapoitafsiri kwa kupeleka katika lugha nyingine a bit of semantic will be missed ...Ndo maana tunasoma kama ilivyo ili isipoteze maana.
Una uthibitisho kuwa kilichoandikwa humo ni maneno ya Mungu na si stori za watu tu?
 
Mimi ni kijana ambaye Kwa muda wa miaka 2 nimekuwa nikifatilia mijadala mbalimbali hapa Jf katika jukwaa hili la intelligence. Moja ya mijadala ambayo imekuwa ikinivutia sana ni hii ya dhana ya uwepo wa Mungu.

Swali kubwa ambalo nimeku wa nikijiuliza ni " Mungu alitoka wapi"

Baada ya kuisoma sana biblia na Quran pamoja na kuwahoji viongozi mbalimbali wa dini, hatimaye nikapata jibu la swali lililonitatiza muda mrefu, Mungu alitoka wapi?

Nimegundua kuwa muumba wa Mungu ni mwanadamu. Yes mwanadamu kama Mimi na wewe ndiye aliyemuumba Mungu.

Kwanini nimefikia hitimisho hilo?

Vitabu tunavyoaminishwa kuwa ni vya Mungu mkuu asiyeshindwa na kitu ( biblia & Quran) ni vitabu vyenye makosa mengi sana ya kimantiki na habari nyingi zenye utata, jambo ambalo tusingetegemea liwepo katika kitabu kilichoandikwa kwa muongozo kutoka kwa Mungu mkuu mwenye uwezo asiyeshindwa na kitu.

Uwepo wa habari hizo zenye utata zinadhihirisha moja kati ya mambo yafuatayo.

1. Mungu hana ukuu tunaoambiwa ndio sababu ameshindwa kutoa mwongonzo mzuri katika kuandika kitabu kisicho na makosa ya kimatinki.

2. Habari hizi ni zao la fikra za mwanadamu aliyeishi katika zama za giza na ujinga. Mwanadamu ambae alitaka kutafuta majibu mepesi katika maswali magumu yaliyomzunguka ndio sababu zina utata.

Kama jibu ni 1 basi Mungu mkuu asiyeshindwa na kitu hayupo Bali aliyepo ni dhaifu na mbabaishaji aliyeshindwa kuandika vizuri kitabu kinachomuelezea yeye mwenyewe.

Kama jibu ni 2 ,basi Mungu mkuu asiyeshindwa na kitu hayupo ndiyo sababu akatokea mtu akatunga habari kutokana na fikra zake mwenyewe. Angekuepo asingeruhusu magepu katika fikra za mwanadamu ambayo yamepelekea mwanadamu huyo kujitungia majibu mepesi na habari zenye utata ili kuziba hayo magepu katika fikra zake.

Pointi zote mbili utaona zinaonyesha kuwa Mungu mkuu asiyeshindwa na kitu mjuzi wa yote hayupo Bali " ama aliyepo ni dhaifu,mbabaishaji na asiye na uelewa wowote kuhusu ulimwengu, ama dhana nzima ni hadithi ya kutungwa katika fikra za mwanadamu aliyeishi katika zama za ujinga na kukosa access ya taarifa mbalimbali.

Nawasilisha.
Kujua kama kuna Mungu wala sio complex issue.
Ipo hivi.. Mungu=Muumba(aliyekuumba wewe, huyo ndiyo Mungu wako). Labda kama useme wewe haujaumbwa umejileta mwenyewe hapa duniani na wazazi wako uliwaleta wewe hapa duniani, na wazazi wa wazazi wako uliwaleta wewe hapa duniani. Labda ikiwa hivyo unaweza ukasema hakuna Mungu.

AHSANTE
 
Huna lolote unalojua wewe pamoja na kufatilia hili jukwaa kwa miaka miwili bado hujapata kitu cha kutushawishi zaidi ya kutaka watu wakujazie comments Tu "NI KIJANA KIMWILI ILA KIFIKRA WE NI MZEE TENA KIKONGWE" Huna tofauti na mtoto aliyetoka kuachishwa kunyonya na mama yake
 
Vijana wakishavuta bangi lazima waanze kuchachawa
Huyu kijana hata ukitaka kumuelesha bado ataleta ujuaji mwingi

Basi muacheni anachoona yeye na akili zake

Maana huyu sio wa kwanza kumletea mungu dhihaka na wala hatakuwa wa mwisho.
Umeshindwa kujadili hoja ya Cornwallis, badala yake una mjadili Cornwallis mtoa hoja..
 
Back
Top Bottom