Unakula nini/unakunywa nini huku ukiwa unabarizi hapa JF?

Mara nyingi usiku mimi huwa nakunywa dry red wine na hutafuna chilly clips au black coffee na tende
 
Nimechelewa leo hapa nakula ugali na dagaa mchele. Nitashushia na kakinywaji kidogo kuweka kichwa sawa huku naendelea kuperuzi JF.
 
Nimechelewa leo hapa nakula ugali na dagaa mchele. Nitashushia na kakinywaji kidogo kuweka kichwa sawa huku naendelea kuperuzi JF.
Jitahidi michango yako hapa jukwaani isiwe ya kidagaa dagaa
 
Uko sahihi, hapa tunaweza kuzalisha maswali mengine, inachofanya ile iitwe chai ni majani au ni muunganiko wa viungo? Na chai ni nini?
Nafikiri chai ni majani (tea) yakiwa ya aina mbali mbali! Wengine huongeza viungo kwenye chai mfano majani yanaongezewa tangawizi bado itabaki kuwa chai lakini itaitwa chai ya tangawizi! Chai ya iliki, etc.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…