Nimetoka zangu kwenye mihangaiko ya hapa na pale, nikaingia bandani nikachukua mayai mawili kutoka kwa kuku wangu wa kienyeji, nikayachemsha na kuyafanya kitafunwa na chai yangu ya kahawa, huku hawa kuku zangu wakinitazama ninavyokula uzao wao.
Baada ya nusu saa, nikaingia shambani na kuvunja mahindi sita, nikayachemsha, na sasa nayatafuna huku nikisoma jumbe zenu hapa JF.
Hii ndio fahari ya kuishi kijijini/ nje ya mji, unakula kitu kisichokuwa na kemikali, hewa safi; natamani na nyie wananzengo mje huku.
Hapo ulipo, unakula nini/unakunywa nini huku ukiwa unabarizi hapa jf? Au unabarizi huku mdomo ukiwa mkavu?
View attachment 3591249