Unakula nini/unakunywa nini huku ukiwa unabarizi hapa JF?

Hapo nina kinywaji kimeandikwa (kombucha)
 
Nakula muhindi wa kupaka chumvi ya pilipili na ndimu. Kipande cha miambili, nabarizi jf huku nasubiri daladala za Kisenvule.
 
Acha ubahili, nunua mhindi mzima
Mkuu muhindi mzima kuumaliza shughuli, mahindi mengi ya Dar huwa yanakaa mda mrefu hadi radha inaisha kabisa na unakuwa mgumu kwa kukaa mda mrefu ndo maana muhindi unaungwa na chumvi,pilipili na ndimu. Sasa ukinunua muhindi mzima utatafuna hadi taya ziume kwa ugumu wake.😁😁😁 Sehem nyingine unavunja muhindi na kuuweka jikoni kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…