Unakumbuka nini kuanzia Mwaka 1998 hadi 2000?

Kifo cha Mwalimu JK Nyerere mwaka 1999!
 
1999
Nakumbuka nipo primary tupo dinning room mida ya mchana TV inawashwa tunaona nyimbo za maombolezo baba wa taifa amefariki
Tunarudi class darasa zima ni kilio πŸ˜† dah
 
Uuuuiiiiii πŸƒπŸΎβ€β™€οΈπŸƒπŸΎβ€β™€οΈπŸƒπŸΎβ€β™€οΈπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ kumbe,,m ata siwafaham
Shauri yako πŸ˜‚πŸ˜‚
Sema mtu mmoja muelewa sana.!
 
1. Elnino pale home maji yalijaa balaa.
2. Ugaidi ubalozi wa marekani yani yale mabomu tuliyasikia.
3. Kifo cha Nyerere.
4. Kufutwa kwa mtihani darasa la saba 1997 na kurudiwa 1998. Nilikua mdogo sana ila nakumbuka.
5. Kuanza kwa michango ya wazazi ili kujenga shule za sekondari, ilikua kila mwanafunzi buku 5 kama sijasahau. Michango hii ndio iliwezesha kupata shule kadhaa ambapo baadae nilisoma moja ya shule hizo.
6. World cup ufaransa 1998.
7. Yote ya yote kirusi cha Y2K kilivyotishia computer kuzima dunia nzima 1999 kwenda 2000.
8. Bwana Kibwetere kuwachoma watu kanisani Uganda.
9. Kutangazwa kwa mwisho wa dunia 2000.

N.k n.k
 
Dah!....those were your days...
 
Ma Bro wengi walienda Marekani miaka hii kwasababu enzi hizo hakukuwa na akili ya kwenda nchi nyingine tofauti na Marekani
 
Shuleni kwetu tulikuwa na michango 3 maarufu,kama hujalipa hiyo husogei darasani!


1.UPE
2.ULINZI
3.UMITASHUMTA
 
Iko kama hiv

- 1998 nimempoteza mama angu mzazi nikiwa mtoto mdogo tu Darasa la pili. Hii ndio kumbukumbu yangu kubwa mpaka leo

- 1999 nakumbuka msiba wa mwalimu nyerere ndio kumbukumbu yangu kubwa maana ilikua inasemekana akifa Nyerere Tanzania kutatokea vita. Siku ile nikiwa shulen nakumbuka kuwaona walimu wakiwa na huzuni sana, nilikua darasa la 3

- 2000 nakumbuka ndio kwa mara ya kwanza kabisa nafanya mtihani unaoitwa wa Taifa wa Darasa la 4. Tulikua tunaambiwa huo mtihani hutakiwi kukatakata hovyo majibu πŸ˜‚
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…