Unakumbuka nini wakati unafanya mtihani wa Kidato cha Nne

2012 Nilifanya pepa ya chemistry ya kupima uelewa mpaka nikawa nafurahi huku najibuu...!! matokeo kutoka ndalichakoo akatunyoosha balaaa shikamoo mama ndalii 😀 😀
Aisee kumbe mtoto wa juzi
 
Nimepiga awamu 2 .2004 nilipata channel Five masomo yote saba.Nikarudi kivingine 2007 nikapata C nne.Nachokumbuka kwenye paper la mathee nilikariri swali lolote la polynomial function likija jibu lake ni all real numbers except 4.Kwa sasa nadunda tuu.Asante Mama ,asante Mungu.
 
Sintosahau paper limevuja, tukafanya solving usiku mzima, kuingia kwenye mtihani kitu chenyewe kabisa, ile imefika nusu saa tukaambiwa tusimame wakakusanya makaratasi yao wakatugawia mtihani mwingine, nusu ya darasa tuliangua vilio
Chai
 
Chai
 
Aisee
 
Chai
 
Kipindi hicho, sie wahenga, ule mtiani uliofutwa! 1998,kwenye paper ya Physics practical, nikawa nachora kwa peni, zimebaki DK 10,muda uishe, ticha wangu akaja taratiiiibu akaninonngoneza, "ukichora kwa peni, unapigwa faini, hiyo paper ndio umeferi" Nilihisi nimemwagiwa maji,nikaona ndoto zangu za kuwa engineer ndio zimeisha, nilikuwa nachukua PCM, sie ndio wale tulikuwa tunajiita sayansi pure, staki combination nyingine, nikaweka nguvu kwenye PCM tu,!
Paper likaisha, jioni wakaja wadogo zetu na kaka zetu wa form 3,2,1,na five na, six, wanatuuliza paper vipi? Mi nilikuwa mmoja wa vipanga pale shuleni, form 4 yetu, ilikuwa inategemewa ifute machozi na Historia ya kufelisha, kabla yetu, shule ilikuwa haijawahi kupata div one au two, ya juu kabisa ilikuwa div 3,ya mwisho!
Ikafika jioni, taarifa ya habari,tukasikia paper imefutwa! (Mungu ananjia nyingi za kumfikisha mja wake apaatakapo) , nikasikia ahueni, tukrudi January 1999! Nikajipanga sawa sawa, piga paper vibaya Sana, nikaitoa kimasomaso shule na one ya point kadhaa, PCM ni Vibanda tu!
Fast forward, Leo na kula matunda ya uinjinia, nikiwaza, nimesoma shule haina umeme, nimetumia kibatari na TAA za chemli,maji mpaka mtoni au ziwani, hakuna smart phone, wala internet, techinolojia kubwa ilikuwa radio zenye FM!, harafu Leo, kuna mtoto hata kama upo st kayumba, material ya kusoma yapo kila Kona, harafu unafeli!
 
Nilipata dv four 😂🤣🤣🤣🤣🤣
Ila mindset ya kusoma Azania ilinisaidia sana chuo..
Maana nilianziaga certificate🤣🤣🤣 up to the top
Ndiyo SIASA hiyo BOSS wangu 🙏🏽🙏🏽
wee ngoma ya ndalichakoo ilikuwaa
Hapo utasikia kuna SPECIAL SCHOOLS kama MZUMBE, ILBORU, TABORA BOYS na KIBAHA SECONDARY. Lakini ukijaribu kuangalia TOP TEN YA MWAKA 2007 ya KIDATO CHA NNE, wote niliwaburuza m'maee...😂😂
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…