Mkuu kama uko na tatizo la kusahau..!mbona hizi habari ujazisahau?
Sent using Jamii Forums mobile app
Nikiwa nimejilaza kitandani kwa kupumzika tu,miguu iko chini, yaani nilikaa kitandani halafu nikaamua kujilaza. Nilikaa kwa upande ambao mtu akiwa amelala kawaida huweka au kuelekeza miguu yake, baadae nikajilaza.
Baada ya dakika kadhaa nilimuona nyoka akinitazama, akiwa amesimama upande wa kushoto wa kitanda, tukawa tunatazamana yeye akiwa chini sakafuni. Tulitazamana hatimae nyoka akaamua kushusha kichwa chake na kugeuka na kuondoka zake.
Niliishiwa nguvu, sikuamini kabisa nilichokiona.yaani kitendo cha kuinuka nusu mzima nyoka ndio kilinishangaza, hapo ndipo nilipojua kuwa kumbe nyoka anaweza kupanda kitandani kirahisi tu.
Naamini ni Mungu tu ndio alikuwa mwamuzi wangu siku hiyo.
Unaamini katika Mungu? Wewe ulinusurika vipi, uliokoka vipi? Ulipona vipi? Tuwekee tukio lako tafadhali.
Mwanang umetusanua ni xai story za wanyabilee van cliff, Sasa mpka nyoka aingie chumbani kwani unakaa porini? Halafu haujamalizia baada ya hapo nyoka alienda wapi? Hii ni chai
Sent using Jamii Forums mobile app
Unashangaa nyoka kuingia chumbani ,wewe ladda utakua unaishi Manhattan New york City.Kama nyumba ina maua mengi tegemea kuwa na nyoka kama wageni wako,hasa wa Kijani.Lkini alinitazama alikua mweusi .
[emoji849]Mwaka 2005 kama Vijana wengi wa Kibongo nilidhamilia kuzamia South Africa... Niliondoka Dar Mimi na Rafiki yangu tukapitia Mtwara tukaibukia Mji wa Pamba Vijijini Upande wa Mozambique....
Tukiwa njiani tulikutana na Mbongo 1 so safari yetu ikawa ya watu 3...
Usiku ulikua Umeingia tukaenda kwenye Nyumba moja Maeneo ya Kijiji kimoja huko Pemba kuomba Hifadhi japo kwa usiku huo then Kesho yake asubuhi tuendelee na safari....
Mwenye Nyumba akaenda kushauriana na mkewe baadaye akaja na Mifuko ya Salfeti, akatwambia wametupa Hifadhi ila si ndani ya Nyumba, akatuonesha sehemu ya kulala chini ya mti wa Mwembe ambao Upo jirani na Nyumba yao.
Hatakua na jinsi kila mtu akachukua kilago chake tukaenda kutandika chini Mwembe na kujilaza.....
Wale wenzangu wawili hawakua comfortable kulala pale chini, wakashauriana wakaamua wapande juu ya mti na kujiegesha huko.... Mimi nikaamua kuendelea kulala pale chini.....
Kifupi asubuhi kunakucha Mimi nimejikuta naamka pembeni kabisa ya Makazi ya ile Nyumba, ile kuangalia pembeni naona Mistari ya Mburuto wa kile Kiroba nilichotumia kulalia, nikafata ule Mburuto mpaka pale chini ya mti, naona alama zingine za Unyayo zimekatiza pale pale nilipokua nimelala, alama Zile za Unyayo zinaonekana juu ya Mburuto wa kile Kiroba, Nikiwa Najiuliza nini imetokea.... Kutizama juu naona wenzangu wanatetemeka hatari na mmoja wetu Suruali yake Ilikua imelowa..... Nawauliza kuna nini....?
Wananambia kama Nusu saa iliyopita Simba kapita pale chini ya mti nilipokua nimelala, wao wameshtuka wanagundua Simba yupo chini ya mti... Wakashindwa kufanya chochote juu yangu baadaye kulivyoanza kupambazuka kidogo wakawa hawanioni pale chini zaidi ya kuona Mburuto kwa mbali..
Mpaka Leo sinaga jibu ni nini kilitokea, nani aliburuta Kiroba nilicholalia....!
Wale wanadamu....,bahati mbaya.Asubuhi saa 12 naamka na wenge nikimbie shule.. naenda kushika kitasa ili nifungue nakuta black mamba kajizinga pale kwenye kitasa ananikodolea macho..
Yaani umbali wa nyoka na mkono wangu kama inch 5 tu.
Nilishtuka sana..hua siui mdudu yoyote baada ya mbu so niliamsha wengine waje wamtoe nikawaambia wamfukuze nje. Bahati mbaya wale binaadamu walimuua yule nyoka
Mkuu itanichukua muda sana kuamini hii stori yakoMwaka 2005 kama Vijana wengi wa Kibongo nilidhamilia kuzamia South Africa... Niliondoka Dar Mimi na Rafiki yangu tukapitia Mtwara tukaibukia Mji wa Pamba Vijijini Upande wa Mozambique....
Tukiwa njiani tulikutana na Mbongo 1 so safari yetu ikawa ya watu 3...
Usiku ulikua Umeingia tukaenda kwenye Nyumba moja Maeneo ya Kijiji kimoja huko Pemba kuomba Hifadhi japo kwa usiku huo then Kesho yake asubuhi tuendelee na safari....
Mwenye Nyumba akaenda kushauriana na mkewe baadaye akaja na Mifuko ya Salfeti, akatwambia wametupa Hifadhi ila si ndani ya Nyumba, akatuonesha sehemu ya kulala chini ya mti wa Mwembe ambao Upo jirani na Nyumba yao.
Hatakua na jinsi kila mtu akachukua kilago chake tukaenda kutandika chini Mwembe na kujilaza.....
Wale wenzangu wawili hawakua comfortable kulala pale chini, wakashauriana wakaamua wapande juu ya mti na kujiegesha huko.... Mimi nikaamua kuendelea kulala pale chini.....
Kifupi asubuhi kunakucha Mimi nimejikuta naamka pembeni kabisa ya Makazi ya ile Nyumba, ile kuangalia pembeni naona Mistari ya Mburuto wa kile Kiroba nilichotumia kulalia, nikafata ule Mburuto mpaka pale chini ya mti, naona alama zingine za Unyayo zimekatiza pale pale nilipokua nimelala, alama Zile za Unyayo zinaonekana juu ya Mburuto wa kile Kiroba, Nikiwa Najiuliza nini imetokea.... Kutizama juu naona wenzangu wanatetemeka hatari na mmoja wetu Suruali yake Ilikua imelowa..... Nawauliza kuna nini....?
Wananambia kama Nusu saa iliyopita Simba kapita pale chini ya mti nilipokua nimelala, wao wameshtuka wanagundua Simba yupo chini ya mti... Wakashindwa kufanya chochote juu yangu baadaye kulivyoanza kupambazuka kidogo wakawa hawanioni pale chini zaidi ya kuona Mburuto kwa mbali..
Mpaka Leo sinaga jibu ni nini kilitokea, nani aliburuta Kiroba nilicholalia....!
Na huu ndo ukweli.ndo maana tunapaswa kumshukuru Mungu kwa kila jambo ni mengi anatutendea anatukinga nayo lakini hatuoni,,tunataka miujiza ya kuonekana tuHuwezi ukahesabu matukio makubwa na ya ajabu anayokuepusha nayo Mungu kimiujiza hata ndani ya dakika moja tu, ni mengi muno kiasi kwamba akili yako haina uwezo huo. Kwa hiyo hili swali lako katika uhalisia haliko sahihi!
Tuchukulie mfano, ukitoka nyumbani asubuhi halafu ukarudi jioni, ni muujiza wa ajabu mno ambao watu wengi huwa hatuelewi ila ni kwa sababu tu kuwa tulio wengi huwa tunatoka salama na kurudi salama, na kwa sababu hiyo tulishachukulia kuwa ni granted na ni kawaida, na si muujiza. Kwa hiyo katika hili huwa wengi wetu tunashindwa kuuona mkono wa ajabu wa Mungu katika haya yote ya kila siku, unless mtu anusurike kwenye tukio kama la kukoswa koswa na moto wa tank la mafuta, hapo ndiyo tunadai kuuona muujiza wakati kumbe Mungu huwa hata katika hali tofauti na hiyo, huwa anatuepusha na matukio mengine mengi makubwa sana, na wakati mwingine ya ajabu kuzidi hata yale ambayo huwa anatuonyesha, lakini huwa hatuuoni muujiza wake kwa sababu tukio hakutuonyesha; aliamua kulimeza mwenyewe na sisi tukawa hatukuliona. Na pale anapoamua kutushirikisha katika kuliona tukio, ndiyo pale tunapoona kuwa ametenda muujiza wakati katika hali ya kawaida, every coming second Mungu yuko na wewe na anatenda miujiza ya ajabu sana kwako, bila wewe mwenyewe kujua. Mungu akiamua kukuacha wewe just a second, YOU ARE GONE! Kwa hiyo ninachoweza kusema ni kuwa Mungu anatenda muujiza kwako kwa idadi ambayo matukio yake huna uwezo wa kuyahesabu kwa namna yalivyo mengi, tuseme hata ndani ya dakika moja tu,! Anatenda kimya kimya bila kukuonyesha.
Nilishangaa sana siku moja tuko kwenye mkutano wa nje wa injili, mhubiri mmoja akajisifu kuwa ana uwezo wa kujilinda dakika 15 bila Mungu. Hii possibly ilikuw ni shibe ya chakula kwa sababu ilikuwa jioni. Alikuwa ameshiba!
Me nataka kujua hayo mengi katika ulimwengu huu,nijuze@WAKUG-OOGLE
Unataka kujua sababu...au namna nilianza mpaka kufikia hapo?
Kama ni sababu ..mpaka kesho siijui...
Imenifanya kujua..mengi.. ..tunaishi katika ulimwengu ambao ni machache mno tunajua kuuhusu!
Sent using Jamii Forums mobile app
Mungu ndio anayejua alafu kuna uwepo tena wa supernatural power?[emoji848]Niliwahi kupata ajali ya Toyo Makumbusho pale asee hata sijui nilitokaje maana hata nguo nilizokuwa nimevaa hazikupata hata angalau vumbi.
Watu walibaki wanatuangalia mimi na boda wangu kwa mshangao maana tuliserereka kwenye lami kama meter zaidi ya kumi hivi ila Mungu ndio anajua ilikuaje maana hata ile toyo haikuvunjika hata indicator au mirror.
Kuna muda huwa tunaonyeshwa kuwa kuna uwepo wa supernatural powers hapa duniani.
Yeah Mungu mwenyewe ni supernatural being, au?Mungu ndio anayejua alafu kuna uwepo tena wa supernatural power?[emoji848]
CIA wangebahatika kuzuia sahmbulio la Septemba 11, wamachi wa kawaida wa Marekani wala wasingejua kuwa CIA imewakinga na tukio gani baya, wao wangeona shwari tu. Na Mungu mara nyingi anafanya kazi kama CIA. anankukinga na majanga mengi makubwa, halafu hatangazi au hakujulishiNa huu ndo ukweli.ndo maana tunapaswa kumshukuru Mungu kwa kila jambo ni mengi anatutendea anatukinga nayo lakini hatuoni,,tunataka miujiza ya kuonekana tu
Mkuu ebu njoo nayo upya taratibu taf hii kaliMmmh.. .
Nilikaa I.c.u..mda sana tu..
Lakini ajabu..nilikuwa pembeni ya mwili wangu ulipolala...natoka na kuingia wodini...naona ndugu na madoctor...tatizo nilikuwa siwezi kushika mtu au kitu wala kuongea na nikitembea nilikuwa sikanyagi ardhi!
Nikajiuliza sana sana...kwa nini iwe hivi? jibu sikupata!
Kwa ufupi...nilirudi .. katika hali ya kushangaza mno.
Lakini ndugu zangu ... huu ulimwengu
una mapana!
Sent using Jamii Forums mobile app
Boga gani Mkuu?
Mkuu acha kabsa