Unakumbuka tukio gani ulilonusurika na ukaamini ni mkono wa Mungu umekunusuru?

Nikiwa mdogo wa miezi mitatu,house girl aliondoka akaniacha kitandani kwangu akanigubika na manguo. Jiko la ndani akaacha kainjika maharagwe kwenye jiko la umeme. Akaacha milango wazi akaondoka zake. Mama yangu akiwa kazini akasema arudi nyumbani kidogo. Anafika home akakuta hali kama hiyo. Mama alinisimulia mwaka jana tu. Nikasema hakika Mungu ni Ebeneza.
Jambo jingine nilikwenda Clinic ya kawaida nikiwa mjamzito. Nafika DR ananipima pressure 190/120.Anapima mkojo akanikuta na protein kibao. Akaniambia haurudi nyumbani tunakuinduce sasa hivi maana nilikuwa nimebakiza wiki nne nijifungue.
Mind you that nilikuwa najiona poa tu. Kumbe pamoja mwenyewe najiona vizuri kumbe ndani ilikuwa imejificha pre eclampsia.
Hakika Mungu ni Ebeneza kanishindia mambo mengi sana yaliyo nje ya uwezo wangu na ataendelea kunishindia.
 
Hmmm..mkuu hebu elezea zaidi.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pole sana mkuu! Nimecheka sana japo si jambo la kuchekesha
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilinusurika shaba mwaka 2017.
Tulikaa tumekaa sehemu na rafiki zangu tunalipa kodi.

Meza nyingine ambayo ilikua nyuma yangu wakaanza zogo. Mara nikasikia mlio ambao sikuulewa ila kwa akili yangu nikahisi ni chupa yenye pombe imerushwa na wale watu imepasuka.

Ghafla nikasikia lala chini. Wamepiga risasi.
Aiseee. Niliishiwa nguvu kabisa. Ile risasi ilipita pembeni kidogo sana na mimi.
Ningekufa siku ile.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwaka 2006 natoka shule kwenda nyumbani niko seat ya mbele nmepakana na dereva, ilikuwa hiace, tumetokea tengeru kuelekea Arusha mjini, tulipofika mwanzoni mwa daraja la mto Nduruma abiria akapiga mluzi kutokea migombani huko, kumbe konda alimsikia bhana, akagonga dereva akafunga breki gari ikasimama ukingoni mwa daraja, nusu iko pembeni na nusu iko barabarani, nyuma kuna mteremko na mbele kuna mteremko yaan daraja liko bondeni, ghafla tukasikia mlio wa honi mfululizo kutokea nyuma kumbe ilikuwa trela ya mchanga zinazojenga barabara, kule mbele linashuka semi trela la kontena pa kupisha hakuna maana gari yetu ukiisogeza tu inadumbukia mtoni na mto wenyew uko kina kirefu kweli afu kuna mawe ( wenyeji wa arusha wanajua), naa hapo tunatakiwa tupishe yale malori yapite, hatukuwa na la kufanya zaidi tu nilimwona dereva kalalia usukani na kinamama wanapiga mayowe, hadi leo sisahau tulivyonusurika maana yule jamaa wa mchanga angetugusa kidogo tu angetushusha mtoni na tusingebaki hata mmoja.
Dereva yule alishika breki huku akitukwepa hadi nkahisi harufu ya matairi km yanaungua, km yupo hai Mungu ambariki huko aliko.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
raha ya jaamii forums, asante sana
 
Hiyo pre eclamsia ndo nini em tuelezee kidogo
 
Mmmmmmm,, niliskia hivi ndo unakua umekufa, ukizikwa ndo Nawwwe unapotea kimoja
 
Umefupisha sana story jamaa aliporudi lindo uliendelea na mgegedo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…