Unamiliki iPhone ya macho matatu wakati hata kiwanja huna, wewe ni bure tu

Wapo wengi hao,vijana wa kizazi hiki tabu sana,nilikutana na kijana graduate kabisa,yupo na ajira,28yrs Bado anakaa nyumbani,salary laki 4,Kuna siku nikamuona ana simu ya apple,kuuliza akasema amedunduliza mishahara ya miezi mitatu Ili apate milioni akanunua cm,Tena haoni hatari kabisa.
Anataka aonekane kwamba ana cm,
Ikabidi nimpe makavu,
Nikamuambia hiyo salary yake mi nilikuwa nalipwa 12 yrs ago!!aache ujinga,atafute gheto,awekeze pesa yake,unachokiona Cha maana sana leo,ndani ya 10 yrs kitakuwa hakina maana,sasa Cha nini?wekeza kwenye vitu vya kujenga uchumi wako,kama nyumba,viwanja,
 
...kweli mkuu... Mwingine kilele cha mafanikio yake hapa jijini ni kuwa ka IST kake...mwinginge ni kumiliki boda boda Tano...mwingine ni kumiliki VX kama ya Wabunge!..basi ili mradi kila mmoja wetu ana ndoto zake. Tunatofautina. Na ndio maana dunia yetu ina raha sana. Tunatofautiana....
 
...Umemaliza Mkuu! [emoji16][emoji16][emoji16][emoji16][emoji120][emoji120]
 
...Neno [emoji120]
 
Mwambie bana,wote tukijenga nani atapanga?

Aendelee kununua viwanja,sisi tunatembea na viwanja vyetu mfukoni,komaa kununua dunia kama unaishi milele.
 
Umeongea mengi lakini ni PUMBA TUPU; mtoa mada hajawaongelea hao unaosema kwao wana viwanja. kawaongelea makapuku ambao hata hela ya kula ni shida na anaishi nyumba mbovu ya kupanga badala ya kununua kiwanja ananunua simu ya bei mbaya cha muhimu anachofanya na hio simu ni kuangalia umbea instagram,facebook na kutuma messages whatsapp; hana lingine lolote na hio simu ilio mcost pesa nyingi sasa huo si ujuha!!! Kingine ulaya watu hawajengi nyumba wewe, nyumba wanazikuta zishajengwa tena na serikali hata wenye pesa zao ni kununua tu. Hata hao matajiri wenye eneo kubwa la ardhi pia, hawaruhusiwi kujijengea tu kwa vile wana pesa lazima wakubaliwe kujenga na serikali hizo ndio taratibu zao. Simu nunua ya bei mbaya lakini iwe at least iwe inakuingizia pesa pia sio show off za samaki samaki huku pa kulala dhofli hal.
 
sijaandika Pumba bro najua nilichoandika hata kama mtu ni kapuku kila mtu ana plan za maisha yake huwezi lazimisha unachofikiria wewe mwingine afikirie.
 
hata wewe unaonyesha hujatembea je unamuonaje mtu ana nyumba ya majani kwao na kwake lakini nje amepaki shangingi la milioni60 hali hii iko Tabora na Zambia huyo na wewe nani mjinga.Kama ni nyumba anayo lakini ya majani na ana simu ya bei mbaya the life is choice kilicho akili mwako sio kilicho akilini kwa mwenzio ndio maana mungu akaumba mrefu mfupi mweupe mweusi.
 
Kiwanja cha nini mimi kwani nataka kuanzisha timu ya mpira?
 
Kwan inauzwa bei gan hyo iPhone mkuu
 
Ni sawa lakini unakuta jitu lipo lipo tu sasa utasema hio ni aki

Siyo kila mtu anatakiwa amiliki kiwanja, wengine hatuna hata mpango wa kujenga tunatafuta hela kinatumia
 
Ngoja wala vya gaidi waje kukuzodoa wakati umesema kweli kabisa.
Nawewe wacha ushamba basi. Inaelekea huna elimu ama elimu unayo ila umekosa expossure.

Fahamu kuwa kila mtu anaishi duniani kwa lengo la kutimiza ndoto yake wala si yamwigine.

Sasa we mimacho inakutoka kwa sababu gani wakati mtu anapambana atafute pesa kwa njia anazozijua ili kutimiza ndoto yake?

Tatizo we unataka watu watimize ndoto zako za viwanja na mashamba badala ya kutimiza ndoto zao.

Watu kama nyie mara nyingi huwa na roho za kichawi kufuatilia maisha ya watu wengine kwa kujilinganisha.

Ukijitambua wewe ni nani huwezi kuwa na muda wa kufuatilia watu wengine bali utafocus kweye vipaumbele vyako na si vya wengine.

Kila mtu ana kipaumbele chake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…