Unampigia simu kwa namba ngeni halafu hapokei baadaye anakwambia hapokeagi namba ngeni

Unampigia simu kwa namba ngeni halafu hapokei baadaye anakwambia hapokeagi namba ngeni

Naona watu wengi wanajitahidi kubadili mada baada ya kukosa hoja zenye mashiko...

Hatujazungumzia kuhusu kupigiwa simu mara 5 nk....tunazungumzia hata ile mara moja tu namba ngeni imeingia hupokei.

Kuna jamaa ana namba yangu ya Tigo ila ya Voda hana. Sasa siku hiyo nikawa namtafuta kwa ajili ya shida yake halafu nikawa sina credit kwenye tigo. Dakika zilikuwa kwenye voda.

Nikampigia. Ikaita sana, wakati inakaribia kukatika ndio akapokea. Nikamwambia Fohadi hapa.

Akasema una bahati huwa sipokei namba ngeni. Sikumjali, nikamwambia ile dili imetick na fanya hivi na hivi kakamilishe swala. Akashukuru.

Sasa mtu kama huyu, unaona kabisa hana hoja za msingi kutokupokea simu. Na hapo shida ilikuwa yake. Je kuna dharura ngapi atapishana nazo? Huwezi jua muda huo mtu anakuhitaji kiasi gani hadi anakupigia simu.

Afu inshu ya msg ni senseless. Mimi kutuma msg ni last option unless sina dakika.

Wakuu mnakwama....mnakwama tena sio kidogo.
Kama ilivyo last option kwako kutuma msg
Basi na Kwa wengine kupokea simu ni last option.

Kwahiyo usitake kutulazimisha tupokee mkuu.
 
Kama ilivyo last option kwako kutuma msg
Basi na Kwa wengine kupokea simu ni last option.

Kwahiyo usitake kutulazimisha tupokee mkuu.
Hujalazimishwa....Mbona mihemko mkuu...au jamaa kapiga hajakulipa?
 
Haijanitokea kwa mtu mmoja au wawili. Ni watu wengi sana. Wengine ni watu wangu wa karibu. Unampigia simu kwa namba ngeni halafu hapokei baadaye anakwambia hapokeagi namba ngeni.

Mwingine labda ni mtu ambae hamjawahi kuwasiliana na ndiyo kwa mara ya kwanza labda umepata namba yake. Nayeye hana namba yako na una shida ungependa kuongea nae. Unapiga simu hapokei. Baadae atakuja kukwambia namba ngeni hapokei.

Nini siri ya kutopokea namba ngeni? Faida zake ni zipi au hata nyinyi mnafanya bila kujua faida na hasara zake?
Ila si unaacha meseji, ukijitambulisha? Akikujua atakutafuta.
 
Ila si unaacha meseji, ukijitambulisha? Akikujua atakutafuta.
Jaribu kufikiria, mfano ni simi ya dharura ambayo inabidi majibu yapataikane haraka.

Mimi naamini hata wewe ukiwa na haraka sana na mtu huwa hutumi msg. Option ya kwanza ni kupiga direct
 
Bongo kuna watu wapuuzi sana, wengine hua matapeli, wengine huwa malaya, Ila wengine huwa wajinga tu
 
Back
Top Bottom