Kwenye mapenzi mbali na ngono kuna mambo ya kusaidina matatizo madogo madogo na hata makubwa kama yapo ndani ya uwezo wenu.
Mfano mwanaume umemuambia mwanamke wako akuazime let's say Tshs 20,000 na ukamuahidi kwamba utamrejeshea baada ya siku tano lakini baada siku moja kabla ya kufika siku ya ahadi unamuambia bila hata yeye kukuuliza kwamba hela unayotegemea kumlipa bado hujaipokea ila unamuhaidi kwamba haitovuka siku tatu nitakua nimekupatia tena zaidi hata ya uliyonipa.
Lakini kesho yake kabla hata siku uliyomuahidi kumrejeshea haijapita anaanza kuulizia tena kwa fujo yani kana kwamba wewe hujawahi kumsaidia pesa yoyote tena bila hata ya kuhitaji kurejeshewa
Je, ni kosa kumlipa hela yake na kuvunja uhusiano kimyakimya?
NB: Lengo sio kumdhulumu hela yake ila naongelea reaction yake katika kukudai kana kwamba anahisi unataka kumdhulumu hela ndogo kama hiyo
Nini maoni yako au mtazamo wako kwa mtu kama huyo ambae umeshamsaidia pesa nyingi tena mara nyingi bila hata ya kumkopesha?
awali ya yote, huyo manzi hakujali kabisaa wewe na shida zako kwa sasa. Yuko very focused na malengo yake na sio kwamba hakupendi 🐒
Lakini pili, hakuamini kabisaa wewe, uwezo wako na ahadi zako. Huenda hamjazoeana vya kutosha. Sio kwamba hakuamini kimapenzi, la hashaa kwenye pesa tu 🐒
Tatu, hana muda na wewe wala kujua shida na matatizo yako kama yameisha, ispokua akili, mawazo, malengo na moyo wake uko kwenye pesa na mali zake. Yuko bize kutafuta pesa, hana muda na Mapenzi kwa sasa. Mvumilie ule maisha ndani ya penzi 🐒
nne na mwisho kwa uchache kwa leo, huyo manzi ni mbinafsi ambae hayuko tayari kua kwenye mauhusiano siriazi ya kimapenzi kwa sasa, ispokua biashara au mahusiano ambayo ndani yake pawepo pesa za kutosha. Anajitafuta kwanza 🐒
Subra yavuta kheri na mvumilivu hula mbivu.
Ile jambo muhimu kabisa, ni kua mstahimilivu na mwenye subra.
Usifanye uamuzi wa haraka.