Unamtafsiri vipi mwanamke mwenye tabia hii?

Unamtafsiri vipi mwanamke mwenye tabia hii?

Li
Kwenye mapenzi mbali na ngono kuna mambo ya kusaidina matatizo madogo madogo na hata makubwa kama yapo ndani ya uwezo wenu.

Mfano mwanaume umemuambia mwanamke wako akuazime let's say Tshs 20,000 na ukamuahidi kwamba utamrejeshea baada ya siku tano lakini baada siku moja kabla ya kufika siku ya ahadi unamuambia bila hata yeye kukuuliza kwamba hela unayotegemea kumlipa bado hujaipokea ila unamuhaidi kwamba haitovuka siku tatu nitakua nimekupatia tena zaidi hata ya uliyonipa.

Lakini kesho yake kabla hata siku uliyomuahidi kumrejeshea haijapita anaanza kuulizia tena kwa fujo yani kana kwamba wewe hujawahi kumsaidia pesa yoyote tena bila hata ya kuhitaji kurejeshewa

Je, ni kosa kumlipa hela yake na kuvunja uhusiano kimyakimya?

NB: Lengo sio kumdhulumu hela yake ila naongelea reaction yake katika kukudai kana kwamba anahisi unataka kumdhulumu hela ndogo kama hiyo

Nini maoni yako au mtazamo wako kwa mtu kama huyo ambae umeshamsaidia pesa nyingi tena mara nyingi bila hata ya kumkopesha?
Lipa pesa ya watu mkuu
 
Lipa deni kwanza ndipo ufikirie kumuacha, hiyo ulikopa hukuomba.
 
Achana na Hela ya mwanamke,ni ya moto....ova
 
Dawa ya deni ni kulipa na ni vizuri kulipa kwa wakati bila kuvunja ahadi.
 
Back
Top Bottom