Unapata hisia gani ukifikiria kuhusu Umri wako?

Unapata hisia gani ukifikiria kuhusu Umri wako?

Mimi huwa nawasalimia watu wa 60’s kwa amani kabisa, hawa wengine kwakweli nashindwa. Nawauliza tu habari? Za kwako? Basi

Sasa kuna siku nikayakanyaga akaja mzee mmoja ofisini, yuko kwenye mid au late 50’s nikamwambia “Habari?”
Aiseeee alinichambaaaa, mpaka leo wenzangu wananitania!
Mi sitoagi shkamoo ovyo ovyo hadi nione kweli huyu mzee kwa mwonekano.
 
Leo nmesalimiwa shkamoo na jamaa lina mindevu, nkaitikia marahaba (ila moyoni nkajisemea mmh hii sasa kuzeeshana bila sababu)
Wengine ni miyeyusho, zaman ukimwona dogo anakusalimia mambo unaona anazingua, una mkazia ebu amkia, leo akikusalimia mambo unashukuru unaenda na flow, wale wazee waliokua wanakataa shikamoo nilikua naona waajabu ila leo nawaelewa. Kuna wengine ndo nuksi kabisa utaskia flan eeh mbona unazeeka haraka wananitiaga nuksi walee,
 
Mimi huwa nawasalimia watu wa 60’s kwa amani kabisa, hawa wengine kwakweli nashindwa. Nawauliza tu habari? Za kwako? Basi

Sasa kuna siku nikayakanyaga akaja mzee mmoja ofisini, yuko kwenye mid au late 50’s nikamwambia “Habari?”
Aiseeee alinichambaaaa, mpaka leo wenzangu wananitania!
Bora wewe, mi nilishawahi hadi amkia wadogo zangu kisa hii miili

Hasa wadada kuna baadhi unaweza hisi wameenda age kumbe hata wewe umemzidi😂 au kakupita mmoja
 
kawaida tu. Ukikaa kwa kutulia busy na maisha, utakuja kugundua age is really just a number. Why bother with something u gat nothing to do about it??
Nina miaka 60 ninajiona kama mtu mwenye umri wa miaka 35 umri si kitu chcochote ni namba umuhimu ni uwe na Afya nzuri ya kuweza kufanya kazi yoyote ile ya kuweza kukuingizia pesa.
 
Nina 19 ila najiona mkubwa sana na sijafanya chochote cha maana na maisha yangu😢
Ulitaka ufanye nini sasa, uwe na nyumba, gari, kampuni na familia 😁?....

Either ways nakuelewa sana tu maana kila mmoja hujipima kutokana na pale alipo dhidi ya kule anapotamani kwenda regardless ya jamii ina mtazamo gani.

Ila kama haina majukumu mazito ya kukuzuia kuishi kidogo, jitahidi ufurahie maisha kabla ya majukumu halisi kuja maana yatakupa nafasi chache za kupata furaha halisi.
 
Huwa nafadhaika sana pale wadada ambao kwa macho nawaona kama tupo sawa wanaponiita M'BABA badala ya M'KAKA

Pia vijana wa kiume ambao nawaona ni wa rika langu wanaponiita FATHER badala ya BROTHER

Huwa najiuliza hivi ni kweli ndo nimekuwa mkubwa kiasi hiki? Ghafla hivi? Mbona ni jana tu najikumbuka nikiwa nacheza michezo ya kitoto nikiwa primary! [emoji26][emoji26]
 
Back
Top Bottom