Unapoanzia uchawi ndipo sayansi inapoishia

Unapoanzia uchawi ndipo sayansi inapoishia

Mshana Jr kuna dawa ya kuzuia zongo? Nilishapigwa mbili sitasahau nilivyoteseka. Ndani ya muda mfupi tumbo liliuma sana na kuanza kuvimba. Wazee walinipa mizizi nikatafuna na kutapika kile chakula kizimakizima. Ilikuwa supu na nyama. Yaani alifika mama jirani akakuna kichwani tu sikuchukua round.
 
Hujajibu swali,basi tuambie kanda gani hakuna uchawi?
Uchawi uko kila mahali ila kuna kunakoongoza kama ilivyo darasani wanaongoza na wengine wanafuata in ascending order.
 
  • Thanks
Reactions: uth
Uchawi uko kila mahali ila kuna kunakoongoza kama ilivyo darasani wanaongoza na wengine wanafuata in ascending order.
Kwa mujibu wa hoja yako ya ukanda kwamba kanda yenye uchawi mwingi ni vilaza unaonaje tukateua rais anaetoka kwenye hiyo kanda ambayo ww unasema haina uchawi mwingi?je jiwe anatoka kanda gani?
 
Kweli mkuu, natokaje hapo maana hadi naogopa kutembea na hela mfukoni.
Fanya hivi chukua noti tano kisha baadhi zichane vichungi, yaani kule kwenye pembe. Ondoa kabisa... Kama ni ishu ya ushirikina hazitapotea tena
Mchawi hata siku moja hachukui kitu kisicho kamili
 
Kuna wakati niliyajua matabano ya zongo ilibidi tufundishwe maana enzi hizo watoto wa Dar mkifika bush asubuhi mnacheza mkiwa mmevaa ndala vibibi vinashindana kuwarushia mazongo
Ule utaalamu ningeuhifdhi sasa hivi tungepiga pesa bro Mshana Jr
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Kuna mtu humu jf jina limenitoka,alipandisha uzi hapa jf kuwa mshana Jr ni kibaraka wa shetani humu jf,nilicheka sana hivi ule uzi uliuona mwenyewe?
Anaitwa maishapopote [emoji3] [emoji3] [emoji3].... Nilicheka sana
 
  • Thanks
Reactions: uth
Ila pia watoto wengi wa WACHAWI kichwa ni butu mno. Wengi hawa cross secondary na huwa hata mikoa yao kielimu inashika mkia. Kumbukeni mikoa kama Tanga, Lindi na Mtwara matokeo ya NECTA miaka iliyopita. Bila kusahau Pemba. Msinipige makofi. Mshana Jr atanitetea.
Ni sahihi kabisa... Mchawi hahitaji elimu ya mzungu... Ili aifanyie nini sasa
 
  • Thanks
Reactions: uth
Mshana Jr kuna dawa ya kuzuia zongo? Nilishapigwa mbili sitasahau nilivyoteseka. Ndani ya muda mfupi tumbo liliuma sana na kuanza kuvimba. Wazee walinipa mizizi nikatafuna na kutapika kile chakula kizimakizima. Ilikuwa supu na nyama. Yaani alifika mama jirani akakuna kichwani tu sikuchukua round.
Nadhani Zongo halizuiliki ila linatibika... Ule utaalam ni kiboko unakaa machoni. Na transmission ya ni eye to eye contact
 
  • Thanks
Reactions: uth
Kwa mujibu wa hoja yako ya ukanda kwamba kanda yenye uchawi mwingi ni vilaza unaonaje tukateua rais anaetoka kwenye hiyo kanda ambayo ww unasema haina uchawi mwingi?je jiwe anatoka kanda gani?
@bobwe2 Shauri yako...! [emoji40] [emoji40]
 
  • Thanks
Reactions: uth
Nadhan umeshapewa ushauri,

Swali langu ni kwamba,

Jinamizi ni linini?

Husababishwa na nini!?
Mkuu; ushauri uliotolewa ni sawa. Ndio maana wamesema Usilale chali. Jinamizi ni ndoto sumbufu yaani utaota unakosa pumzi, unakabwa au unaota mtu mzito kakukalia shingoni/kifuani au umesongwa na kitu kinachokufanya usipumue/unakosa hewa vizuri na kuishiwa nguvu. Maelezo ya kisayansi kuhusu kisababishi ni kwamba:

Ukila chakula na kushiba (Tumbo likajaa chakula)halafu mara ukaingia kitandani kulala (especially kulala chali) basi tumbo (stomach) litaegemea kiwambo kiitwacho Diaphragm ambacho huwa kinaruhusu kutanuka kwa mapafu unapovuta hewa. Kiwambo hiki (kipo upande wa juu ya tumbo kati ya mapafu na tumbo) hivyo kitashindwa kufanya kazi yake vizuri kwa kuwa kina mzigo uliokielemea yaani tumbo lililojaa chakula. Kwa hiyo matokeo yake ni kwamba utapumua kwa shida sana - utapata hewa isiyokutosheleza.

Sasa kwa kuwa upo usingizini utajihisi na kuota ndoto kwamba unakabwa au unasongwa na jitu fulani hivi na unashindwa kujitoa au kujiweka huru kutokana na kukosa nguvu (hewa ya oxygen ni kidogo kwenye upumuaji wako ambao tayari ni wa shida) na ukijaribu kupiga kelele kuomba msaada sauti haitoki.

Hapo unasema ni Jinamizi = ndoto sumbufu. Wewe katika kusimulia unasema Walinikaba n.k. usiku nilipokuwa nimelala! Hii kitu ukilala kifudifudi au kulala baada ya saa nzima au zaidi baada ya kula chakula au ukala chakula kilaini na usishibe mno hutaipata.

Mpaka hapo naomba na wenzangu waongezee....
 
mshana Kuna yale madude ambayo hufungwa watoto kiunoni kwa kutumia kitambaa cheusi wengine unakuta mkononi... hivi husaidia nini???




cc Smart911
 
Mkuu, benki kuna zindiko la kufa mtu hawathubutu wanaogopa kunasa. Hata wewe ukiwa na zindiko la uhakika wanaishia kufyonza tu. Wanaoishi vizuri hapa duniani ni wanaojua jinsi ya kuwakomesha wachawi.

Unakuta mtoto wako analia na kuugua bila sababu wewe unaishia kusema Yesu Maria na Yoseph, hosipitali ikishindikana pambana na ulinwengu wa roho. Ujue wanoko hawatakuonyesha njia ya kweli uwe makini.
 
Kuna uhakika gani kwamba ni kweli kama hatuwezi thibitisha kimwili?
Ithibati ya pekee kimwili ni zile zana kama tunguli nk ama la matokeo ya kilichokwisha fanyika
 
  • Thanks
Reactions: uth
Back
Top Bottom