MTAENDELEA KUBISHANA LAKINI TAMBUENI KWAMBA HAKUNA MSHINDI ATAKAYAEPATIKANA
Nilifunzwa huko nyuma, nikafanya utafiti kidogo, nikajiridhisha na hatimaye nikajiwekea kanuni kwamba nitajiweka mbali na mijadala yote yenye mwelekeo wa ushabiki wa kiimani kama dini, kwasababu masuala haya yanahusisha hisia zaidi na si mantiki, hivyo nikajiwekea kanuni zaidi kwamba kama inabidi nishiriki kwenye mjadala unaohusisha ushabiki wa kiimani, basi ni lazima nijue lengo la washiriki wa huo mjadala ni nini, na ikiwezekana niwafahamu wao ni akina nani, na hata uwezo na upeo wao ili nichague maneno na lugha ifaayo kwao.
Kwenye masuala haya ya kiimani za dini, nimegundua kuna mijadala ya aina mbili, kuna ile yenye lengo la kuelimisha kwa dhati kabisa na kujikita kwenye hoja, ambayo kwa kawaida huhusisha mantiki (Mfano nini maana ya Kwaresima? Nini maana ya Mwezi wa Ramadhani? Nini maana ya kufunga, n,k. ,
Pili, ni ile mijadala inayohusisha ushabiki na mihemko zaidi, yenye hisia zaidi badala ya mantiki, ambayo hailengi kutoa elimu, bali ni kuonesha kejeli na kwamba 'imani yangu' ndiyo imani bora kuliko yako, kwamba 'mimi niko sahihi' kuliko wewe, inalenga zaidi kutafuta ushindi zaidi na sio kuelimisha, inakwepa hoja ya msingi badala yake inajikita kwenye mashambulizi binafsi.
Kwa maoni yangu mjadala uliopo hapa jamvini una mwelekeo wa kishabiki zaidi, wenye mihemko, haulengi kutoa elimu, una kejeli imani fulani dhidi ya nyingine, kila mmoja anatumia nguvu nyingi kutaka kuonesha kwamba imani yake ni bora kuliko ya mwingine na matokeo yake hisia hutawala na wengi hukereka, baadhi wameanza kushambulia watu binafsi na kujiweka mbali na hoja ya msingi, lakini pia siwafahamu washiriki wa mjadala huu wala uwezo na upeo wao. Kwa mtindo huu tambueni kwamba hakuna mshindi atakayepatikana.
JADALA HUU NA YA AINA KAMA HII HAINA TIJA, HUUMIZA ZAIDI BADALA YA KUPONYA