kiranga, kabla ya noah pia kulikuwa na waafrica, possibly mke wa noah alikuwa mwafrica[/QUOTE
naomba ufafanuzi. Nakubali kabla ya Nuhu kulikuwa na waafrika. sasa baada ya gharika ambayo kimantiki inaonyesha iliangamiza dunia nzima ina maana walimwengu woooote kuanzia waafrika weusi, jamii ya kichina china (mongolic), wahindi, wazungu..... ni kizazi cha nuhu maana dunia mpya ilianzia hapo!!??? hii imekaaje? Historia ya uchagani ninakotoka inaonyesha wakati wachaga wanaingia kutoka huko walikotoka wabantu wengine waliwakuta wenyeji wa ule mlima. wale wenyeji walikuwa weusi sana na wafupi sana (wakoningwa/mbilikimo). sasa hivi hakuna hata mmoja, ina maana waliwaua au walitoweka kutokana na mazingira kubanwa. Tukienda kwenye jamii za kihindi na wenyeji wa asili wa marekani na italia tunaona kuna watu weusi lakini si waafrika wala hawajawahi kukutana. inaashiria watu weusi walikuwepo kwenye kila eneo la kijiografia - manake ni kuwa hata wachina weusi kwa asili walikuwepo. Hata watoto wa isaka hawakufanana rangi. mmoja nadhani esau alikuwa mwekundu na mwenye nywele nyingi zaidi. nisichokijua ni kwa nini watu wenye rangi nyeusi walichukiwa na wenzao weupe kiasi cha kuangamizwa na kumalizwa kabisa katika baadhi ya maeneo, na kwingine kubaki wachache na mpaka leo wanabaguliwa. kwa hiyo siamini kuwa kigezo cha uafrika ni rangi sema tu afrika ilikuwa na weusi wengi. mabara mengine yamefanikiwa kuangamiza watu wao wenye rangi nyeusi.