Umeanza vibaya kwa kumpiga. Mke hapigwi narudia, mke hapigwi.
Yuko jamaa yangu mhehe alikua anajifanya kidume anarudi saa tano sita. Mke analalamika jamaa anakomaa.
Kuna siku mke karudi saa saba usiku, akamgongea mlango mwamba, mwamba akasema sifungui mlango, mwanamke akapandisha sauti na kusema nitavunja vioo vyote vya madirisha na kwenda kulala kwa bachelor yoyote aliye jirani huku akigonga mlango kwa jiwe. Mbona mwamba alifungua mlango huku mtaa mzima watu wanatega sikio, waifu aliendelea kusema ukinigusa tu mashahidi wangu Ni mtaa mzima, nakupeleka mahakamani.
Aisee mwamba alikaa ndani kwa kutulia utadhani sio mhehe.