Unawezaje kuishi na mwanamke mwenye hasira kali na mrahisi wa kuzila na kufoka?

Jitahidi kuheshimu matakwa yake kwa kuweka na kuheshimu space au boundary kati yenu.

Punguza attention na wewe usijipe umuhimu wa kutaka kubadilisha tabia zake hiyo si kazi wala wajibu wako.

Unapaswa kujitambua wewe kwanza, mabadiliko yanapaswa kuanzia kwako.
 
Inaonekana hujaweza kumfahamu huyo baby wako kiasi cha kujua kipi hapendi na kipi anaweza kufurahia

Ili uweze kuishi vizuri na mpenzi/mke wako ni lazima ufanikiwe kumfahamu kiundani kwenye nini hapendi na kipi anapenda

Kwa uzoefu wangu inaonekana huyo mpenzi wako ana stress (hasa stress za hela/ajira/maisha)

Badala ya kuona mna mazungumzo ambayo yanalenga kuonesha mnatokaje kwenye changamoto fulani mnazopitia yeye anakuona mnapiga stori asizozitaka.(Inaonekana mnaweza kukaa pamoja hata masaa 4 lakini haoni ukizungumza kuhusu mipango ya maisha)

Wanawake wa hivyo, hata ukiwa naye faragha usitegemee utamfikisha kibo 🙌
 
Mtu kama huyo hafai. Hakuna mahaba mtu anakasirika kasirika kila mara sasa ndo nini?.. Mfanye abadilike, awe na utu na utulivu. Kama hawezi kujitwist Achana naye.

Kumbuka jukumu la kumtengeneza mke wako na kumshape utakavyo ni lako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…