Unawezaje kuishi na mwanamke mwenye hasira kali na mrahisi wa kuzila na kufoka?

Unawezaje kuishi na mwanamke mwenye hasira kali na mrahisi wa kuzila na kufoka?

Wakuu,

Hapa nimeyakanyaga. Yaani, hata kitu ni kidogo au unamtania - yeye anakuja juu na kufokafoka. Ile wewe unaita kunogesha penzi na tu-story twa hapa na pale, yeye kwake ni kero!

Ana sura nzuri, umbo zuri; na hatujaoana.

Kuishi kwingi, kuona mengi. Wenzangu mlioishi kwingi, watu kama hao mliishi nao vipi?
Bado hujazijua code zake. Nenda nae mdogo mdogo utamtuliza
 
Kwa huyu ukimkaza vizuri ndio kabisaa anasema unamchosha yeye sio punda
Hahaha......pole mkuu, tafuta nafasi ukae naye umweleze nini unapenda na nini hupendi kutoka kwake, kuishi na mtu mliyekutana ukubwani kuna hitaji utashi

Zamani wakati tunakuwa kulikuwa na msemo kwamba "Ukipenda boga utapenda na ua lake"
 
Anafoka kweli na anaweza kukasirika hadi analia kwa kitu kidogo mpaka unashangaa hiki tu ndio kikukasirishe!

Mfano kuna weekend tulitoka out, tukiwa beach nikamtoroka nikaenda sehemu hanioni akapiga simu uko wapi nikamtania nimetoka ukimaliza utanikuta sehemu fulani alooh uo msala haukuwa wa nchi hii alipanic Ile serious hadi usafiri aligoma kupanda na alipuyanga kivyake na tulipokutana homu anafoka hatari eti kwanini nimemdanganya
Au ana mimba?
 
Wakuu,

Hapa nimeyakanyaga. Yaani, hata kitu ni kidogo au unamtania - yeye anakuja juu na kufokafoka. Ile wewe unaita kunogesha penzi na tu-story twa hapa na pale, yeye kwake ni kero!

Ana sura nzuri, umbo zuri; na hatujaoana.

Kuishi kwingi, kuona mengi. Wenzangu mlioishi kwingi, watu kama hao mliishi nao vipi?
Nikabidhi mimi ili uondokane na huo usumbufu.
 
sana tu, sasa uyo anataka waangaliane kama miti msituni, duh..... ata akimlenga na mto anaweza tolewa ngeu na glass 🙈
4921253E-9A56-47E2-B056-80EFC63D555A.jpeg

🤣
 
Back
Top Bottom