Unayoyajua na usiyoyajua kuhusu wanyama wa kufugwa

Kuhusu hilo la mwanae ni ukweli nimewahi kushuhudia live
Fanye yote lakini sio mwanae, mtakosana

That's why unakuta punda mbele ana mzigo au nyuma mbele mtoto yuko free anapiga misele .
Binafsi niliwahi kujaribu kumletea masihara mwanae kabla sijapewa kovu kwenye paji la uso karibu na upara kwa teke zito kabisa


Usimjaribu mtoto wake ..!
 

Kuku wa kienyeji nao kuna wenye roho mbaya na wenye roho nzuri km binadamu katika malezi ya vifaranga.

Wapo ambao ukimuwekea vifaranga vya kuku mwingine anabagua atavidonoa balaa.

Wapo ambao hawana tatizo wanalea vifaranga vya kuku mwingine kiroho safi.
 
Kitu namisi ni kuona zile battle za madume ya mafahali.

Tukiwa machalii wadogo tulikuwa tunachonganisha mafahali halafu tunakaa kuangalia battle.

Wale mafahali wanafikia hatua ya kuwa na bifu na unakuta wako busy kunoa pembe zao kwenye vichuguu.
Ng'ombe ambaye mapembe yake yamekaa horizontally huwa wabishi sana kupigwa, wanaweza wakapigana siku nzima.

Ng'ombe ambao mapembe yao yapo kama U na yamenyoka kiaina kwenda juu huwa wanapiga ng'ombe wengi sana sababu mapembe yao ni makali.

Ng'ombe hunolewa mapembe kwa kuwekwa viazi vya moto akiwa mvivu kujinoa mwenyewe.

Mbuzi ni mwoga sana wa maji usiombee mvua inyeshe ya nguvu ikakukuta machungoni ukataka kurudi na mifugo nyumbani, utapishana naye nchi 1 tu akiwa kwenye kichaka ila utapiga kelele hata kwa kilugha lakini huishia kukutizama tu usoni bila hata wasiwasi (lazima uloane) au ukubali kuingia kwenye kichaka uchomwe na miba ili umtoe na akitoka hapo ataingia tena kwenye kichaka kingine yani ni pasua kichwa.

Ng'ombe akimzoea mkamuaji maziwa mmoja ni vigumu sana kusogelewa na Mtu mwingine la sivyo atamchoma mapembe na kumdhuru au kumuua. Bibi alipokuwa hayupo tulikuwa tunavaa nguo zake na kuimba nyimbo zake ili kumbembeleza ng'ombe akubali kukamuliwa maziwa.

Ng'ombe huogopa sana mvua ya upepo ambapo ukizubaa utawakuta hata km 10 mbali na machungoni ikiwa mvua ilikuwa nyingi sana na ya upepo huelekea huko huko kwenye upepo.

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
Halafu kuna jamaa hapo ukimwambia anabisha eti uongo
 
Halafu kuna jamaa hapo ukimwambia anabisha eti uongo
Mpotezee tu, ila kingine ng'ombe huangaliwa sana na Mchungaji anapozaa asile ule mfuko wa uzazi aliomtolea ndama tumboni mwake, Mchungaji akichelewa tu ng'ombe akala basi huyo ng'ombe hufa mazima.

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
MBWA.
MBWA ni mnyama mwenye kutunza sana kumbukumbu. MBWA haptei njia hatakama ni mara ya kwanza kufika eneo Hilo. MBWA huweka alama kwa kutumia to mkojo wake. Lakini pia kama ukimpiga MBWA asiye wa kwako e.g umekutana naye njiani halafu ukimpiga kwa makusudi , siku ikatokea umeendal ktk nyumba anakoishi lazima akutie jino i.e. Atakukumbuka na atajilipiza kisasi.
 
Mpotezee tu, ila kingine ng'ombe huangaliwa sana na Mchungaji anapozaa asile ule mfuko wa uzazi aliomtolea ndama tumboni mwake, Mchungaji akichelewa tu ng'ombe akala basi huyo ng'ombe hufa mazima.

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
Sasa kuna ndugu hapo alijisahau akamuacha ng'ombe ajifungue mwenyewe matokeo ndama akafa
 
Hiyo ya kumnyonya ndama kwa mdomo mnajiweka kwenye hatari kubwa ya kuambukizwa, ni bora kumning'iniza kwa kumnyanyua miguu ya nyuma ili majimaji yachuruzike kutoka puani, kumpangusa pua na kitambaa na hata kumumwagia maji ya baridi ili aanze kupumua vizuri.​
 
Sio kweli miaka na miaka wazee wamefanya hivyo na wapo tu
Anatakiwa pia kumwagiwa mkojo wa mama yake wewe unasema maji ya baridi unataka kumuua ndama?

Hata hivyo unaweza kumpangusa na kumfuta futa ila hii ndio the best ndama atakuwa ng'ombe bora sana
 
Kuku mimi sifugi hawana ishu
Hawawezi kustahimili mazingira magumu
Wepesi sana kushikwa na magonjwa kama mdonde
Wakinyeshewa tu na maji sana hata kufa anakufa ..!
Siwezi kuhimili hiyo pressure
Vizuri mkuu ila yupi anakupa faida mapema..? More risk more profit.... chukua hiyo bro
 
Changia ujualo na wewe mkuu
Mie experience yangu labda kwa kuku tu na mbwa ndo nimewafuga kwa muda mrefu sana.

Hivi kuna mnyama wa kufugwa anapenda ngono kama mbwa dume?

Kuku wanatofautiana tabia kama binadamu, pia kuku wanamtambua binadamu mbaya, wanatoa ishara kwa namna tofauti ya milio yao.

Mbwa ni mnyama mzalendo zaidi anaweza kuwa rafiki kuliko hata binadamu, Unavyomfundisha ndivyo anavyokuwa.
 
Ukienda kuwinda na mbwa porini na hilo eneo kukawa na chatu basi jua upo kwenye hatari ya kuliwa.
Chatu anapokua anawinda anatoa harufu ya kuvutia ambayo inamvutia mbwa, mbwa atasogea lakini akigundua kwamba ni chatu basi hukimbilia kwako na hapo ndo cha moto utakiona
 
Maelezo mengi ila hujaeleza chochote kuonesha uongo wa mtoa Uzi dhidi ya ukweli wako, ndo nini sasa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…