Undani kuhusu ajali ya Ndege ya Precision Air, Kudondoka kwake hadi hatua za Uokozi

Undani kuhusu ajali ya Ndege ya Precision Air, Kudondoka kwake hadi hatua za Uokozi

Nimepoteza shemeji yaani mke wa jamaa yangu kwenye hii ajali. Amefariki yeye na dada yake
Ni tragedy
Poleni sana aisee Aneth ni college mate wangu pale UDSM alikuwa amenizidi darasa moja. Inaumiza sana kwa kweli, kuna picha moja nimeona yupo na mumewe na wanae sijui wana hali gani huko walipo. Mwenyezi Mungu azilaze roho za marehemu hawa mahala pema peponi.
 
Kuna uzi unaelezea sababu ya ajali sio hali ya hewa bali ni tairi zilishindwa kufungu ana kutaka maelekezo akalazimika kuzurula huku akingoja maelekezo, anadai baada ya kuzunguka mda mrefu akahofia wese kukata ikabidi wamuelekeze akatue ziwani timu ya uokozi ipo tayari inamfuata, ndugu yetu akajiamini akaenda kuchumpa na maji yalivyo shida ikawa imefika car wash! Kilichofuata mpaka wanatua wote walikua salama na bado walikua wanawasiliana wakati tayari wakiwa salama salmini yaliyo fuata wote tumeshuhudia ss na huyu ndugu yetu anatuambia tatizo lilikua hali ya hewa wapi na wapi
Nauliza tu hivi haiwezekani kama ameshindwa kutua akageuza kuelekea mwanza au dar?
 
Kama ni hivyo basi bado kuna shida sana. Kama alishabaini tairi hazifunguki, basi hapakuwa na sababu kubwa ya kendelea kuzurura juu kwa juu, uamuzi mzuri ulikuwa ni kurudi mwanza penya uwanja mkubwa na vifa zaidi. Muda wa kutoka bukoba kurudi mwanza ungetosha mwanza kujiandaa, na hao ndiyo wangemwambia tua sehemu fulani ndipo tumejiandaa kwa uokozi. Wanamwelekeza atue bukoba eti wameshajiandaa - Huo ni utani
Uko sahihi alitakiwa arudi mwanza tho wanasema alihofia kuishiwa mafuta, hivi na ndege wanaweka mafuta ya bajeti? Kweli?
 
Poleni sana aisee Aneth ni college mate wangu pale UDSM alikuwa amenizidi darasa moja. Inaumiza sana kwa kweli, kuna picha moja nimeona yupo na mumewe na wanae sijui wana hali gani huko walipo. Mwenyezi Mungu azilaze roho za marehemu hawa mahala pema peponi.
Shukran mkuu.
Aneth ni mdogo wake Linda Atulinde Biteya ambaye kwa muda mrefu amekuwa dada yangu na shemeji kwa jamaa yangu.

Mungu awapokee na kuwapumzisha marehemu wetu wote wa ajali
 
bado nauliza swali, kama Rubani angeamua kurudi Mwanza ama kutua uwanja wa Magufuli Chato au Kahama asubiri hali ya hewa itengemae hilo lisingewezekana?

kuna muda sisi tulitoka Mza - Ngara, hali ya hewa ikawa mbaya balaa Ngara, ikabidi turudi Mwanza - baada ya masaa 3 tukarudi tena - ni gharama ila unaepuka ku risk.

Binafsi, Ile habari kwamba ndege matairi yaligoma kutoka naona Ina mashiko, na itakua ndio sababu kubwa ilimshawishi rubani kutua kwenye maji.

Ni kawaida sana rubani kuahirisha kutua au kwenda kutua uwanja wa karibu inapotokea Hali ya kewa kuwa mbaya.
 
Kama ni hivyo basi bado kuna shida sana. Kama alishabaini tairi hazifunguki, basi hapakuwa na sababu kubwa ya kendelea kuzurura juu kwa juu, uamuzi mzuri ulikuwa ni kurudi mwanza penya uwanja mkubwa na vifa zaidi. Muda wa kutoka bukoba kurudi mwanza ungetosha mwanza kujiandaa, na hao ndiyo wangemwambia tua sehemu fulani ndipo tumejiandaa kwa uokozi. Wanamwelekeza atue bukoba eti wameshajiandaa - Huo ni utani

Kwa taratibu zao ilitakiwa asikilize na kupewa maelekezo na watu wanaoongoza ndege uwanjani, hiyo kuzunguka itakua ilikua kusubiria kupata maelekezo ya Nini Cha kufanya.

Kwa ndege ambayo matairi yamegoma kutoka, kutua kwenye maji ilikua njia salama zaidi.

Faida za kuitafuta Mwanza ni kama ifuatavyo, kwanza ndege ingekua nyepesi Kwa vile mafuta yangetumika wakati wa safari na kupunguza athari wakati wa kutua kwenye maji.

Pili, japo hili Sina uhakika (Kwa uzoefu na historian za awali kwenye mambo ya uokoaji) ndege kutua ziwani karibia na Mwanza ingeweza kupata msaada kwenye zoezi la kuokoa abiria.
 
Kwani mpaka sasa, kwa wale walioweza kuiona hiyo ndege kwenye maji, vipi imetoa matairi ama la?

Kama matairi yamejitokeza, maana yake issue ya kushindwa kutoa matairi tunaifuta mara moja, na kama matairi hayajajitokeza basi tunaanzia hapo hapo kuchambua.
 
Ndugu mnapandaje chombo kimoja?
Siyo kila mmoja ni muelewa wa hii ishu lakini wachaga wanapoenda kupeleka mikate Kilimanjaro unakuta familia mbili kibao zimerundikana ndani ya mabasi yanayoenda huko
 
Huenda alipiga hesabu akaona mafuta yaliyobaki kwenye Tank yasingetosha kufika Mwanza, akalazimika kutumia Uzoefu wake ili kutua...

Anyway, R. I.P Wahanga wote..
inauma sana sana, sema tu hatuwezi ku-reverse na ndege ikarudi juu kisha tukasahihisha. Waongoza ndege yawezekana hawakumpa taarifa ama ushauri mzuri rubani, kumbuka rubani kabla ya kufanya uamuzi wake wa mwisho ni lazima awasiliane na uongozi wa uwanja wa ndege.

Yawezekana pia uamuzi wa rubani haukuwa sahihi, ndege haiwezi kutoka mwanza ikiwa na mafut kidogo hilo halipo, angeweza kutafuta kiwanja kikubwa chenye facilities za uokoaji hasa Mwanza.

Nitaelewa zaidi kama ndege labda ilipata hitlafu nyingine zaidi ya ile ya matairi, lakini kama ni suala la matairi tu option ya kurudi mwanza ingekuwa bora zaidi.

Kingine kibaya zaidi ni sisi watanzania kushindwa kuwaokoa ndugu zetu, yaonekana ndege ilivyoanguka abiria wengi walikuwa hai wakiwemo ma-rubani wote, Serikali yetu ijitathimini kwenye hili, wengi wamelaumu sana karne ya 22 mtu kufa kwa kukosa hewa, yaani anakufa anajiona - hili halikubaliki kabisa.

Kwa serikali makini hakuna hata haja ya kuunda tume, ni kuvunja kitengo ya Uokoaji na maafa kitaifa na lazima waziri husika achomoke - hatufai.

Kwa mliowahi kupanda hiyo ndege, hebu jiweke ungekuwa humo afu unashutukia upo kwenye maji na unatumia zaidi ya saa moja hakuna wokozi na unakufa unajiona.

so sad.
 
Siyo kila mmoja ni muelewa wa hii ishu lakini wachaga wanapoenda kupeleka mikate Kilimanjaro unakuta familia mbili kibao zimerundikana ndani ya mabasi yanayoenda huko
Sijasema kabila moja kupanda chombo kimoja. Ninasema ndugu wa familia moja kupanda chombo kimoja.
 
Binafsi, Ile habari kwamba ndege matairi yaligoma kutoka naona Ina mashiko, na itakua ndio sababu kubwa ilimshawishi rubani kutua kwenye maji.

Ni kawaida sana rubani kuahirisha kutua au kwenda kutua uwanja wa karibu inapotokea Hali ya kewa kuwa mbaya.
Binafsi, Ile habari kwamba ndege matairi yaligoma kutoka naona Ina mashiko, na itakua ndio sababu kubwa ilimshawishi rubani kutua kwenye maji.

MKuu tairi huwa hazitolewi ndege ikiwa inakaribia kugusa runway...zinatolewa mapema kabisa ndege ikiwa angani huko ili kama zikigoma kutoka rubani hasishushe ndege....ishu hapa rubani alitaka kutumia uzoefu kushusha ndege katika mazingira ambayo hakutakiwa kufanya hvyo
 
Kuna uzi unaelezea sababu ya ajali sio hali ya hewa bali ni tairi zilishindwa kufungu ana kutaka maelekezo akalazimika kuzurula huku akingoja maelekezo, anadai baada ya kuzunguka mda mrefu akahofia wese kukata ikabidi wamuelekeze akatue ziwani timu ya uokozi ipo tayari inamfuata, ndugu yetu akajiamini akaenda kuchumpa na maji yalivyo shida ikawa imefika car wash! Kilichofuata mpaka wanatua wote walikua salama na bado walikua wanawasiliana wakati tayari wakiwa salama salmini yaliyo fuata wote tumeshuhudia ss na huyu ndugu yetu anatuambia tatizo lilikua hali ya hewa wapi na wapi
Hakuna Utaratibu wowote wa kwamba Ndege ikishindwa kutoa matairi basi ikatue kwenye maji, never. Ndege ikishindwa kutoa matairi inatakiwa itue Airport pale pale, labda tu, kando ya Runway kwenye majani. Kwenye Maji ndio mbaya zaidi
 
Kuna uwezekano mkubwa wa "Human Error" katika hii ajali, nakaribu asilimia 90 za ajali za Ndege duniani ni Human Error, makosa ya Kibinadamu. Na human Error inakuja pale kukiwa na mchanganyiko wa vitu vingi, mfano pale hali ya hewa ilikuwa mbaya, Rubani Kama binadamu akalazimisha kuwa na Option mbili, moja kulazimisha kutua kwa uzoefu, ya pili kurejea Mwanza kusubiri hali ya hewa itengemae.

Taratibu za Ndege Hazina option mbili, Kama hali ya hewa Ni mbaya unatakiwa tu, utafute uwanja mwingine. Ila Rubani ni binadamu akachagua kuwa na Option mbili, ambayo moja huwa ni Risk Sana, kwani iki shindwa inakuwa Disaster, hiyo ya kutumia uzoefu kutua kwa kulazimisha, hatujui zaidi kilichotokea ila mpaka black box, ila inaonekana baada ya kushindwa kutua kwa uzoefu,

Aliamua Take Off Go Around, rugha Yao, yaani kuacha kutua na aelekee Mwanza, au ajaribu Tena, na ndio maana aliingiza tairi, ili azunguke Tena, Hapo Sasa ndio, sababu za kitaalam Zina kuja, pengine hakukamilisha Go Around Procedure na Kusababisha Ndege ika "Stall" na kuangukia Ziwani, au Kwa vile Ndege ilikuwa kwenye low Attitude ukichanganya na hali ya hewa kuwa mbaya Sana,

Basi Go Around iligoma, na Ndege ika "Stall" na kuangukia Ziwani, Ndio maana wenzetu waliweka Black Boxes kwa ajili ya kugundua nn kilitokea hapo, Ndege haikuwa na Shida, ndio maana Rubani hakuita Mayday Mayday ! Ila aliripoti kuwa Ni hali ya hewa tu.

" Human Error" Zina sababisha ajali nyingi za Ndege Duniani, ila tukumbuke, Usafiri wa Ndege ndio salama kuliko Usafiri wowote Duniani,. Lakini Sasa Kuna hicho kitu. "Human Error" Rubani Siyo malaika, anaweza kufanya mistake anytime hasa, Hawa wanaojiita Wazoefu, Kujiamini huwa Kuna wa Cost Sana, na Kuwa Cost watu Wengine. Nashauri tusubirie majibu ya Black Boxes
 
Binafsi, Ile habari kwamba ndege matairi yaligoma kutoka naona Ina mashiko, na itakua ndio sababu kubwa ilimshawishi rubani kutua kwenye maji.

MKuu tairi huwa hazitolewi ndege ikiwa inakaribia kugusa runway...zinatolewa mapema kabisa ndege ikiwa angani huko ili kama zikigoma kutoka rubani hasishushe ndege....ishu hapa rubani alitaka kutumia uzoefu kushusha ndege katika mazingira ambayo hakutakiwa kufanya hvyo

Narudia Tena, sio lazima niwe sahihi ni mtizamo wangu tu.

Naelewa fika ndege inatia matairi ikiwa juu Tena mbali kabisa kabla ya kukaribua said uwanja.

Nimeshawahi kupanda air Tanzania, ikiwa imeshatoa tairi ili itue ilitokea mvua na ukungu tairi zikarudishwa ndani, tukaahirisha na kuanza Tena zoezi la kutua.

Kama ni tatizo la Hali ya hewa, waongiza ndege wa kituo Cha chini walimruhusu kutua? Mbona ni Mara nyingi tu kesi ya ndege kuahirisha kutua kutokana na Hali ya hewa zinatokea?

Tusubirie matokeo ya uchunguzi na taarifa zitakazopatikana kwenye black box
 
Binafsi, Ile habari kwamba ndege matairi yaligoma kutoka naona Ina mashiko, na itakua ndio sababu kubwa ilimshawishi rubani kutua kwenye maji.

MKuu tairi huwa hazitolewi ndege ikiwa inakaribia kugusa runway...zinatolewa mapema kabisa ndege ikiwa angani huko ili kama zikigoma kutoka rubani hasishushe ndege....ishu hapa rubani alitaka kutumia uzoefu kushusha ndege katika mazingira ambayo hakutakiwa kufanya hvyo
Exactly, tairi zinafunguliwaga mapema sana
 
Back
Top Bottom