Mkuu, hivi ndivyo watanzania wengi tunavyofikiri. Yaani serikali imetudumaza akili kiasi hatuwezi kufanya reasoning.
Wengi hapa wanakupinga kwa kuwa tu ukodishaji umekuwa ni jambo la mazoea, kwa hiyo hawaoni kuwa wanapigwa. Hawaoni hoja yako kuwa elfu 40 kwa vazi la kuvaa masaa 4 tu ni gharama kubwa. Wao wanakuona wewe mshamba na usiyejua lolote.
Mawakili wanapofanya sherehe ya kuandikishwa kwenye daftari la mawakili, ni lazima wavae joho, na joho hilo mahakama hailiuzi, unatakiwa utafute mwenyewe huko mitaani.
Sasa Joho kali kabisa unanunua kwa Tshs 80,000 mpaka Tshs. 120,000/= na linakua la kwako kabisa utaendelea nalo kuingia mahakamani hata kwa miaka 3. Hivyo vyuo vingeruhusu watu wanunue ya kwao, au la wapunguze bei..ni wizi huo sema ndio vile sisiemu imeshatudumaza mpaka wizi tunaukumbatia na kuona ni halali