KERO University of Iringa (UoI) Wanataka tuwape Elfu Arobaini ya Joho. Ni wizi

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Mnapenda kulalama tu
 
Hakuna niliposema bure. Acha kupotosha mjadala. Nimesema tutoe elfu nane sababu ni mtumba wa miaka kibao
Umesema: β€œUniversity of Iringa - UoI, Wanataka tuwape Elfu Arobaini ya Joho. Ni wizi mkubwa.

Joho unavaa halafu halafu baadaye jioni unarudisha.”

Kimsingi, hukubaliani na hiyo sera ya kulipia joho. Maana yake unataka joho upewe bure. Kama malalamiko yako yangekuwa yanahusu ukubwa wa fee, ungesema hivyo clearly!

BTW, hiyo fee ni ya kawaida sana. Vipo vyuo vinavyotoza fee kubwa kuliko hiyo.
 
Chuo kipi kinatoa joho bure? Huo utaratibu ni tangu enzi za mwalimu
Ana hoja, sio kwa sababu miaka yote yanatolewa kwa fedha basi inaleta uhalili.

Je hiko kiasi is it fair. Joh 15yrs linatumika. Huku kila mwaka ukilipa 50,000.

Inabidi waangalie pia kieango cha kuchangia.

Maana wao chuo mbali na kushona kipi kingine wanafanya?
 
Gharama ya joho haiishii kwenye kununua. Kuna maintenance costs (e.g., dry cleaning). Hata ukilivaa kwa saa moja haliwezi kutolewa to the next person hivyo hivyo…
 
Gharama ya joho haiishii kwenye kununua. Kuna maintenance costs (e.g., dry cleaning). Hata ukilivaa kwa saa moja haliwezi kutolewa to the next person hivyo hivyo…
So mwingine analivaa baada ya mwaka sio?
 
Ukitola hapo unakuja mtaani kulalamika kuhusu serikali
Wewe ni mlalamishi tu🀠
 
Tena kuna chuo kama SAUT unalipia joho na unapewa siku 2 za kukaa na joho baada ya graduu, ukichelewa kurudisha siku husika unapigwa fine 10000 kila siku. Ukichelewa siku 7 utalipa fine 70000.
Hakuna namna toa tuu ufurahie moment.
 
Gharama ya joho haiishii kwenye kununua. Kuna maintenance costs (e.g., dry cleaning). Hata ukilivaa kwa saa moja haliwezi kutolewa to the next person hivyo hivyo…
Huwa wanatoa majoho machafu, unaenda kulifua mhusika. Yaani likirudishwa mwaka huu linatunzwa hivyo hivyo mpaka mwakani anachukua mwingine apambane akafue mwenyewe au avae chafu.
 
Huwa wanatoa majoho machafu, unaenda kulifua mhusika. Yaani likirudishwa mwaka huu linatunzwa hivyo hivyo mpaka mwakani anachukua mwingine apambane akafue mwenyewe au avae chafu.
Hao sasa wana matatizo! Utaratibu wenyewe huo ni recipe ya inconsistent care ya majoho. Lazima yachakae mapema.
 
Chuo kipi kinatoa joho bure? Huo utaratibu ni tangu enzi za mwalimu
Mimi nilipata undergraduate degree wakati wa Mwalimu. Tulikuwa tunaweka caution money Sh 100; na baada ya graduation unarudisha joho lao na kupata cheti cha digrii yako. Siku hizi graduate anaondoka na joho lake kwa hiyo ni lazima alilipie.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…