KERO University of Iringa (UoI) Wanataka tuwape Elfu Arobaini ya Joho. Ni wizi

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Sasa hii ndo hoja inayotakiwa kujadiliwa. Alilenga chuo kimoja nilikuwa namwambia kwamba ni utaratibu wa vyuo vyote kwa miaka mingi.
Kiukweli ni pesa ndefu.
 
Mimi nilipata undergraduate degree wakati wa Mwalimu. Tulikuwa tunaweka caution money Sh 100; na baada ya graduation unarudisha joho lao na kupata cheti cha digrii yako. Siku hizi graduate anaondoka na joho lake kwa hiyo ni lazima alilipie.
Kumbe majoho wanaondoka nayo sikujua. Enzi zetu tulirudisha joho na pesa hailurudi. maana bila kurudisha joho hupati cheti.
 
Ndugu yangu, sisi tulio maliza miaka takribani 22 iliyopita tulilipa hiyo, sasa wewe Leo unataka iwe chin?

Ulizia vyuo vingine gharama yake, utajua hiyo 40K bado wanawaonea huruma.
Hata kama ulimaliza enzi za zamadamu, haimaanishi kuwa hii ni sahihi. Wanatulangua.
 
Na kile kimfuko cha kuliweka joho unalipia Ukipoteza tena benki mbona utajutraa!πŸ˜‚

Ukifata cheti unalipia joho uwe ulifanya au hukufanya mahafali!
NIlichelewa kurudisha siku moja, nikalipa faini 10k bank tena hawana masikhara
 
Toa fedha kijana acha janja janja.
Toa hela kijana,acha janja janja.
 
Aisee we jamaa bado unasoma siku zote hizo?
Mi nakuonaga mkongwe humu kumbe bado uko shule tena degree ya kwanza.
Aisee hongera
Huyu figganigga hata mimi nimeshangaa huyu jamaa ni wa siku nyingi humu fb na tena ni platnum Member kumbe bado anasoma? Nadhani anatetea vijana wake au wadogo zake.
Kwa mada anazotoaga humu fb za maana zilizoshiba anastahili kuwa na PhD
 
Binafsi sikushiriki sherehe za kuhitimu.
Na wengi walinishangaa sana, nilichokuwa nakutafuta chuoni kwa muda wote wa kuwapo pale nilikuwanacho kichwani hivyo mengine niliona ya ziada tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…