Unywaji wa pombe aina ya Banana inaathiri nguvu kubwa sana ya vijana

Bushmamy ni kweli kabisa. Hii pombe mkoa wa Kilimanjaro ni janga. Inatakiwa ipigwe marufuku. Haina tofauti na gongo. Unaishi/unatokea maeneo hayo nini?
 
Hali ya huko ni mbaya kwa vijana. Hata mimi nilijionea. Hiyo pombe ya banana haina tofauti na madawa ya kulevya. Kila anayekunywa ni lazima anaathirika.
Kweli Kabisa banana haijawahi muacha mteja wake salama, wote wanaotumia hiyo pombe hata kwa macho ya kawaida unajua tu huyu ni mnywaji wa banana.
 
Bushmamy ni kweli kabisa. Hii pombe mkoa wa Kilimanjaro ni janga. Inatakiwa ipigwe marufuku. Haina tofauti na gongo. Unaishi/unatokea maeneo hayo nini?
Pombe nyingi zinazopatikana kwenye chupa za kijani kama vile Banana, Raha Poa, Simba n.k nyingi ni FAKE!!!

Zilizosajiliwa na kuthibitishwa ni chache sana.

Nyingi zinasindikwa kwenye viwanda bubu, na zinauzwa kimagendo na kusafirishwa usiku wa manane.

Hizi pombe za magendo zinauzwa mpaka 300 kwa chupa.

Na kwasababu huku uchaggani pombe ni kama maji ya kunywa, vijana wengi wasio na kipato hizo pombe ndio kimbilio lao.

Wengi wakishaanza kunywa tu, hata kuiga hawaogi, wanadharaukika na hata kuwa na familia hawawezi kabisa.
 
Kwani hizo banana za huko moshi zinautofauti na za huku nilipo Mimi nilishawahi kunywa Kama vitano na nikaondoka nipo vizuri ila Kuna bia hiyo inaitwa bigwa sinywi zaidi ya tatu
 
Vijana wa kimeru na kiarusha wanateketea
 
Banana zinatengenezwa maeneo mengi Kwa Arusha na Moshi nipombe za kienyeji zinazowekwa kwenye chupa
Zimawekwa na makemiko huko na wala hazina hata expire date. Inaonekana hata hizo asilimia zilizoandikwa kwa nje ni za uongo maana wanywaji ukiwaona wanatia huruma sana, kundi kubwa la vijana limeangukia huko
 
Tatizo lipo kwa serikali kuruhusu kila kitu kifanyike holela holela
 
Tatizo lipo kwa serikali kuruhusu kila kitu kifanyike holela holela
Tatizo ni viwanda bubu, ambayo inahitajika nguvu ya ziada hasa kukiwa na kikosi kazi kushibiti.

Wenye hivyo viwanda wenyewe wanalalamikia viwanda bubu, na wanawajua kabisa watengenezaji lakini serikali bado haitilii mkazo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…