KERO Uondoshaji wa mizigo bandarini ni shida kubwa, TBS inatuumiza Waingizaji wa Shehena (importer) nchini

KERO Uondoshaji wa mizigo bandarini ni shida kubwa, TBS inatuumiza Waingizaji wa Shehena (importer) nchini

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Kwa sasa TBS imekuwa ni mzigo na imekuwa ikizalisha vilio vikubwa sana kwa Waingizaji wa Shehena au Bidhaa nchini (IMPORTER).

Mfumo wao wa utendaji umekuwa mbovu sana na kila siku katika ofisi zao zilizopo TPA ONE STOP [BANDARINI] utakuta misururu mikubwa ya MAWAKALA WA FORODHA wakipambana kuclear mizigo ya wateja wao.

TBS wamekuwa ni JIPU sidhani kama Hayati Magufuli angekuwepo utendaji wao ungekuwa vile. Wamewasababishia IMPORTERS STORAGE za kila siku zisizokuwa na maana kwa kushindwa kumalizia clearance process kwenye system yao ya OAS... Hiki ni kilio kwa kweli.

Unakuta mteja ameshalipia ushuru, wharfage na gharama nyingine za mamlaka nyingine kama GCLA, TMDA, ATOMIC n.k lakini anakuja kukwamishwa na TBS kwa zaidi ya siku 10 hadi shehena inaingia STORAGE.

Kuna wateja wametelekeza mizigo yao bandarini kwa kushindwa kulipia storage zilizokuwa Accumulated baada ya Mkwamo wa mfumo wa TBS hakuna tamko hata la viongozi wao juu ya WAIVER kama tatizo limesababishwa nao kama wanavyofanyaga TRA bali wao wamechagua kuwa MABUBU kwenye hili.

Hapo awali kulikuwa na smooth flow lakini wakafanya INTEGRATION ya mfumo wao OAS na wa TRA - TANESW hapa ndiyo shida ilipoanzia. Taasisi haina watendaji wa kutosha hasa wa PVoC LOW NUMBER OF MAN POWER, hili liwafikie mabosi wa TBS na Wizara ya Uuchukuzi na Wizara ya Fedha.

Uondoshaji wa mizigo bandarini kwa sasa ni shida kubwa sana na viongozi wa TAFFA , TACAS NA CALAT hawajachukua hatua yoyote kuwakutanisha Mawakala wa Forodha na mabosi wa TBS ili watoe kero zao kwao.
 
Mkipewaga mic mbele ya camera mnasema ufanisi bandarini umeongezeka na mama hamumdai nyuma ya camera na kwenye kybord mnatoa milio
Wanaopewa mic ni machawa tena ambao wanakuwa washapewa script ya namna ya kukisifia chama na mama.

Wahanga huwa hawapewi nafasi
 
Kwa kweli kuna haja ya Serikali kulichukulia ili suala kwa uzito mkubwa utendaji wa TBS umekuwa mbovu sana na wamshindwa kabisa kutoa huduma kwa wakati na matokeo yake ni kusababisha gharama ambazo si za lazima.

Kila mara wanaishia kutoa statements za kuomba msamaha bila kujua waagizaji wanaingia gharama kubwa kwa ucheleweshaji wa kupata huduma
 
Tunapenda kuwasilisha malalamiko yetu rasmi kuhusu changamoto zinazoendelea kujitokeza katika matumizi ya mfumo wa TBS OAS, ambao kwa sasa umekuwa moja ya vyanzo vikubwa vya ucheleweshaji wa utoaji wa mizigo bandarini na kusababisha wafanyabiashara kuingia katika gharama zisizo za lazima.

Kwa muda sasa, tumekuwa tukishuhudia mizigo ambayo tayari imefanyiwa ukaguzi na taratibu zote zinazohitajika kukamilishwa ikishindwa kutolewa kwa wakati kutokana na changamoto za mfumo wa OAS. Katika baadhi ya matukio, mfumo umekuwa ukikwama kwa siku kadhaa mfululizo, wakati huo huo muda wa wafanyabiashara wa kutoa mizigo ukiendelea kuhesabika.

Hali hii imekuwa na athari kubwa kwa wafanyabiashara, kwa kuwa storage charges, truck waiting charges na gharama nyingine za ziada zinaendelea kuongezeka wakati ucheleweshaji hausababishwi na mteja wala clearing agent, bali na changamoto za mfumo. Kwa mfano, endapo mteja anapewa muda mfupi wa kukamilisha taratibu za kutoa mzigo, lakini mfumo wa TBS OAS unatumika kwa siku tatu bila kufanya kazi ipasavyo, mteja anaweza kujikuta akitumia sehemu kubwa ya muda wake uliopangwa kwa kusubiri mfumo badala ya kukamilisha utoaji wa mzigo.

Zaidi ya hapo, tunapenda kuonesha kwamba mfumo wa sasa unaleta mzunguko wa ziada wa kiutendaji, kwa kuwa mzigo unatakiwa kuonekana na kuachiliwa katika mfumo wa TBS OAS pamoja na TANeSW/TRA kabla ya kuweza kutoka bandarini. Hii inaongeza utegemezi wa mifumo miwili kwa ajili ya hatua moja ya mwisho ya release.

Kwa upande mwingine, tunaona umuhimu wa kujifunza kutoka kwa mifumo inayotumiwa na taasisi nyingine zinazohusika na mchakato wa bandari, kama vile GCLA, WMA na TAEC, ambapo baada ya ukaguzi na taratibu zao kukamilika, mchakato wa release unaweza kuunganishwa vizuri zaidi na mfumo wa TRA/TANeSW. Mfumo wa TANeSW kwa ujumla umeendelea kuimarika na kuwa sehemu muhimu ya mchakato wa customs clearance, hivyo tunashauri TBS itafute njia ya kupunguza utegemezi wa mfumo wa ziada pale ambapo release inaweza kuthibitishwa moja kwa moja kupitia TANeSW.

MPAKA SASA SYSTEM YA TBS HAUIJAIMARIKA DOCUMENT HAZIONEKANI UPANDE WA TBS OAS NA WANASHINDWA KUFANYIA KAZI.

PHOTO-2026-10-01-18-46-13.jpg
 
Back
Top Bottom