Uongo na Ukweli Kuhusu TANESCO Kuzuiwa Kufanya Maintenance

Hapa umeniacha... unazungumzia mkataba upi?
====
Mkataba huo hapo wa karibu shilingi za kitanzania bilioni 69.
 
Taarifa zozote za Tanesco ni za kusikiliza kwa masikio sita vinginevyo tutapigwa tuchakae
 
Taarifa zozote za Tanesco ni za kusikiliza kwa masikio sita vinginevyo tutapigwa tuchakae
Hapo kuna taarifa ya CAG na Wizara ya Nishati...

Taarifa ya TANESCO hapo ni moja tu inayoonesha maendeleo ya ukarabati pale Ubungo II, na hiyo taarifa ni wakati wa JPM!!

So, unaamini TANESCO wangeweza kuutangazia umma kwamba ukarabati unaendelea wakati hakuna tatizo?!

Hivi uwezekano mkubwa hapo ni upi kati ya kutangaza ukarabati unaendelea wakati hakuna tatizo au kusema hakuna tatizo wakati kuna tatizo? Ni taarifa ipi kati ya hizo ingekuwa safe kwao?
 
Hii taarifa ni mpya kwangu...

Na kwavile mleta mada hajaleta details... nashindwa hata kutia neno!! Itabidi nifanye homework mwenyewe!!

Natakiwa kufanya homework hasa kwavile, naona mtoa mada kazungumzia kirahisi tu kwamba "mfumo wa ufanisi" huku akihusisha kuondolewa kwa watu kama akina Kalemani ni kwa ajili ya kupitisha "madili" kama hayo!!

Wakati mleta mada ameongea kirahisi rahis tu, third
party source inasema:-
Nilipoangalia kwa haraka haraka, nikakutana na tender ambayo ilitangazwa na TANESCO January 29, 2021. Sina uhakika kama tender yenyewe ndo huo mkataba lakini maelezo yake yanafanana sana na maelezo ya thirid party source, kwamba:-



Sasa wakati mleta mada amezungumza kirahisi rahisi tu na kuhusisha upigaji wa akina Makamba, kumbe tenda ilitangazwa tangu enzi za Kalemani1

On top of that, inaonekana ni World Bank Financed Project!!

Sasa je, kwa maelezo ya kwenye hiyo tender, unaamini hicho ni kitu rahisi rahisi tu?

c.c Nazgur

Full tender description, ni hii hapa chini:-
 

Attachments

Kuibinafsisha, HAPANA, huwezi kubinafsisha utlity company!

Unaweza kubinafsisha baadhi ya kazi za TANESCO, kama vile power generation... na hilo lipo kwa miaka kadhaa sasa!!

Ungesema kufanya Management Contract, ningekubaliana na wewe! Hata hivyo, unafanya Management Contract pale unapojiridhisha kwamba tatizo la TANESCO ni management!!

Kwamba post inasagia kunguni utawala uliopita, hilo sio lengo bali kuweka kumbukumbu sawa ili watu waache ushabiki na mahaba ya kisiasa kwenye serious issues! Watu tukiacha ushabiki wa kisiasa, hata wanasiasa wataanza kuwa responsible! Lakini haya mambo jambo hata kama ni la ovyo bado unalitetea kwa nguvu zote kisa tu kimefanywa na umpendae, hilo ni angamizo kwa taifa!!
 
Nilipoangalia kwa haraka haraka, nikakutana na tender ambayo ilitangazwa na TANESCO January 29, 2021. Sina uhakika kama tender yenyewe ndo huo mkataba lakini maelezo yake yanafanana sana na maelezo ya thirid party source, kwamba:-
Asante sana mkuu kwa kufanya homework kisha kujana na maelezo yanayotupa mwanga ya kujua kinachoendelea. Hata hivyo, kwa kuwa huna uhakika kama taarifa ya third part ndiyo inahusiana na mkataba wa mleta mada basi tuvute subira ili tupate uhakika kabla hatujajikita kujibu swali lako muhimu kwenye bandiko nilikonukuu maelezo yako niliyobandika hapo juu.
 
Man,

Data zinaonesha maintenance ilikuwa infanyika?! Hebu ziangalie vizuri hizo data:-

Unaona hapo, kwa mfano mashine #1 ilitakiwa kufanyiwa maintenance baada ya ku-operate saa 30,000 lakini wakati ripoti inatolewa, mashine ilikuwa imepiga mzigo kwa saa 40,356 na hapo baada maintanence ilikuwa haijafanyika!!
 
Tukipata JPM watatu tu kuongoza nchi ya bongolala ni dhahiri baada ya hapo nchi inaweza kuingia machafukoni maana haitatatawalika kabisa. Wananchi wamelishwa sumu mbaya sana kiasi wameweza kuaminishwa kila aina ya uongo na kuamini ukweli. Mtoa mada ametoa a well balanced argument lakini wapiii, kuna watu hawaelewi.
 
Ingawaje nilisema ni third source, and YES, it's a third souce lakini link yake niliipata kutoka kwenye website ya kampuni iliyopewa hiyo tenda...


Aidha, nilisema sina uhakika kwa sababu, mwanzoni source yangu ilikuwa ndo hiyo hiyo third party source, na wala sikuwa na mpango wa kutafuta upande wa pili. Yaani nilitaka kuishia hapo hapo!!

Lakini kama ujuavyo, huwa sipendi kutoa incomplete information, baadae nikaamua kutafuta hiyo tenda kutoka kwa mtoa tenda ambae ni TANESCO!! Lakini hata baada ya kuipata hiyo tenda, sikuhangaika tena kutaka ku-edit nilichoandika!!

That having been said, I'm very confident kwamba tender husika ndo hiyo!!
 
Mkuu Chige ,bandiko lako limeweka mambo mengi sana wazi ambayo yalifichwa "sirini".
Kongole kwa uzalendo wako na Mungu akubariki.
Ningependa kuchangia kwa hoja lakini kwa kuwa napata VAT 69 muda huu,nitapenda kuchangia nitakapokuwa "sober" ili nisije kuandika kitu kilevilevi.
Ubarikiwe sana.
 

Labda ungetusaidia kufafanua hio segment ya mwisho ina maana gani…hours running without maintanance
 
Na wewe unakubali sana kabisa kuwa walikuwa wanakatazwa kufanya maintanance inaingia akilini ?

Sent from my SM-G9350 using JamiiForums mobile app
 
Labda ungetusaidia kufafanua hio segment ya mwisho ina maana gani…hours running without maintanance
Kwa mfano, Machine #1, Hours Required For Maintenance is 30,000 Hours, and Actual Machine Running Hours is 40,356.

Maana yake ni kwamba, kitalaamu hiyo mashine ilitakiwa kufanya kazi kwa saa 30,000 na zikishagonga saa 30,000 hapo inatakiwa kufanyiwa maintanence.

Lakini wakati ilitakiwa kufanya kazi kwa saa 30,000 kisha kufanyiwa maintanence, hadi ripoti inatolewa mashine hiyo ilikuwa imefanya kazi kwa Saa 40,356.

Sasa, 40,356 - 30,000 = 10, 356. Yaani mashine iliendelea kuburuzwa hivyo hivyo kwa saa zingine 10,356 huku ikiwa bado haijafanyiwa maintenance. Ni kama umeambiwa ukimbie 30,000KM kisha upumzike na kupata chakula, lakini baada ya kumaliza zile 30,000KM unalazimishwa ukimbie 10,356KM nyingine, na hivyo kuwa umekimbia 40,356KM bila kupata chakula ulichoahidiwa!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…