Matatizo yenu huwa hamsomi vingenevyo usingeandika kitu ambacho sijakisema!!!
Nilichosema ni kwamba, kabla ya ujenzi wa Bomba la Mtwara kulikuwa na upungufu mkubwa wa umeme! Baada ya kujenga bomba, Serikali ya JK ikapanga kujenga Vituo 4 vya kuzalisha umeme... Kinyerezi I, II, III, na IV ili kuongeza uzalishaji wa umeme!
JK akafanikiwa kujenga Kinyerezi I, lakini kwavile muda wake ulikuwa umeisha, Kinyerezi II iliishia tu kwenye hatua za awali ikiwa ni pamoja na kusaini mkataba!!
Magufuli alipoingia, alitakiwa kujenga Kinyerezi II, III, na IV lakini kinyume chake, akajenga tu Kinyerezi II ambayo mchakato ulishaanza, na ile III na IV akapiga chini akaanzisha Bwawa la Nyerere!!
Sasa kwavile Bwawa la Nyerere linahitaji investment kubwa na time, matokeo yake hadi amekutwa na umauti, mradi ulikuwa hujakamilika!
Matokeo yake, hadi kesho umeme unaotegemewa kwa kiasi kikubwa ni ule ule ambao aliukuta huku wa gesi ukiwa 57% na wa maji 36% na kiasi kilichobaki ni vyanzo vingine!
Hivi kiangazi na ukame ni kitu kile kile?! Au unataka kubisha kwamba hakuna ukame?!
Man, kama si JK kujenga Bomba la Gesi kutoka Mtwara hali ingekuwa MBAYA! Watu mnampa credit JPM kwa sababu ule mradi ulifanyika mwishoni kabisa mwa utawala wa JK, kwahiyo manufaa yake yameanza kuonekana wakati wa JPM, na ndo maana mnadhani JPM ndie alitatua tatizo la umeme!!
Kinyerezi I kwa mfano, tumeanza kutumia umeme wake October 25, 2015!! Na Kinyerezi I na II, zimeingiza zaidi ya 400 MW kwenye grid ya taifa, let alone Ubungo II ambayo installed capacity ni zaidi ya 100 MW!!
Hivi ulishawahi kujiuliza ukitoa hizo 500MW, huyo JPM angekuta hali gani?!
Na kwanini wakati wa huo upungufu hakuonekana nishasema hapa mara nyingi! Kwanza, SIO KWELI kwamba eti hapakuwa na upungufu!! Lakini hayo tuyaache! Ripoti ya CAG imesema wazi kwamba:-
View attachment 2017728
Hayo sio maneno yangu bali ni maneno ya CAG! Na wala sio Ripoti ya wakati wa JK au Samia bali ni wakati wa JPM mwenyewe! CAG hapo anasema hapo TANESCO walikuwa wanakataliwa kuzima mitambo na kufanya ukarabati kwa sababu hifadhi ya umeme ilikuwa ndogo to the point, kama mitambo ingezimwa, ingesababisha mgao!!
Kwahiyo ili serikali ijioneshe hakuna tatizo la umeme, ikawa inalazimisha hizo mashine ziburuzwe hivyo hivyo kwa hofu wakizima, mahali kama Dar penye watu wenye kelele nyingi, ingeingia kwenye mgao! Kwahiyo ikawa "bora punda afe, lakini mzigo ufike"!
Sasa lau kama Kinyerezi III na IV zingejengwa, hiyo hofu isingekuwepo!!
Now tell me: Katika hali ya kawaida tu, hakuna ukame wala nini, bado TANESCO walikuwa wanapigwa STOP kuzima mashine kwa sababu umeme ulikuwa hautoshi... what about chanzo kimoja kinapoathirika?
Hebu nijibu yafuatayo:-
1. Hivi kiangazi na ukame ni kitu kile kile?
2. Unabisha kwamba kina cha maji kwenye mito yetu kimepunguwa?
Look at you... "namba mnazotoa"
Hizo namba ni za kwangu mimi hadi useme "...namba mnazotoa"?
Let me guess... you're the victim of political lies kwa sababu, inaonesha unaamini zaidi kauli zinazoongelewa na wanasiasa na watu wao kuliko ripoti za kitalaamu!!
Hapo kuna takwimu kutoka National Audit Office na zingine kutoka Wizara ya Nishati; na zote hizo ni za wakati wa JPM!! Sasa zangu kivipi?
Na hilo la wapigaji... hivi nchi hii ni lini palikosekana kuwa na wapigaji?
Au nawe ni wale wanaoamini JPM alidhibiti ufisadi?! Hivi ufisadi wakati wa JK watu tulikuwa tunaufahamu vipi kama sio kupitia bungeni na kwenye vyombo vya habari?!
Hiyo awamu ya JPM mnayotaka kutuaminisha hapakuwa na ufisadi, hilo bunge lilikuwa na uwezo wa kujadili hayo mambo?