Uongo na Ukweli Kuhusu TANESCO Kuzuiwa Kufanya Maintenance

Uongo na Ukweli Kuhusu TANESCO Kuzuiwa Kufanya Maintenance

Hebu pitia mwenyewe ulichokuwa unaandika...

Ulichokuwa unakiandika, nikiangalia sasa hivi huwa ncheka. Kuna mwingine wa Banking industry kufa.
Mlitabiri sana Tanzania kuwa kama Zimbabwe, kuwa tutaenda sokoni na matoroli ya hela.

Anyways,

Umesoma nilichoandika?! I doubt kwa sababu ungesoma ungeona nimegusia nyanja mbalimbali! Na katu siwezi kusema it's exclusively ni scientific/operational na ndo maana hata @Mzee Mwanakijiji nilimjibu

Nimesoma ulichoandika, na mimi siyo Mwanakijiji, sijakuuliza tatizo la umeme litapunguzwa na nini.
Hili tatizo la umeme sasa hivi ni tatizo la kisiasa. Unaanza na HYdro halafu una-backup na thermal. Wangeanza na Rufiji na Rusumo halafu waka backup na thermal angalau 300MW to 400MW.

Ujenzi ungeanza 2016, au even earlier, leo tungejenga angalau natural gas powered plant ya 300MW au 200mw as a back up. Watanzania bado hatuwezi kutumia 2000MW hata 2025. Huu umeme unaolalamikiwa na watu wengi ni kwa ajili ya kuwasha taa na sub-woofers.
Yaani Temeke pale Sudan na majaribio kila kibanda kinapiga mziki wa subwoofers kelele kibao mna-overload grid for nothing.
Tatizo mnataka matokeo ya papo kwa papo bila mpangilio.
Again, umesoma?!

Hivi nimesema thermal power plants zimeharibika (pluralism) au nimenukuu Ripoti ya CAG (Special Audit) iliyoonesha mashine #1 to #3 kutofanyiwa maintanence?!
Ukweli ni upi na uongo ni upi?
Sema basi kifupi tuelewe, zimeharibika au zipo down for maintanance? Maana TANESCO wanadai hakuna maji Kidatu na Pangani.
Na wewe mkuu sababu ni ipi?
Kivipi yaani unaona nimelazimisha mgao over the last six years let alone kulazmisha kuwa at the same rate?
Si umesema nyinyi huko Shamba mlikuwa na mgao kama kawaida? Yaani huu mgao ulikuwepo tu hamna cha kushangaza?
Au labda sijakuelewa? Si useme kifupi basi mgao ulikuwa haupo in last six years kama huu tunaouona sasa hivi??
Maana labda mimi mtoto wa kishua.
 
Tazama hii simple logic;

Wakati wa JK mgao wa umeme ulikuwepo, na ulikuwa wa kutengeneza ndio maana zikazaliwa Richmond na madudu mengine.
Upo sahihi kabisa, manake hata Magufuli alisema Wapiga Deal huwa wanaziba maji kutengeneza mgao ili wauze majenereta!!

Hizo ndo hoja zenu, kwa sababu kama nilivyokueleza hapo mwanzo, source yenu ni Wanasiasa!!!

Turudi kwenye Ripoti za Kitalaamu...

Hydro.png


Sasa how come, wale wale waliokuwa wanatengeneza mgao kwa kuziba maji, Ripoti ya JICA inaonesha ndio wamezalisha umeme mwingi zaidi wa maji kuliko wale ambao walikuwa hawazibi maji?

Turudi kwenye Ripoti ya Wizara ya Nishati ya mwaka 2016

Hydro by 2015.png


Ripoti inaonesha watengeneza mgao kwa KUZIBA MAJI, by 2014 walikuwa na installed capacity of 562 MW kwa upande wa wa umeme wa maji!!

Hali ilikuaje baada ya kuingia JPM ambae aliwatia adabu wale waliokuwa wanaziba maji?! Ripoti nyingine ya Wizara ya Nishati inasema:-
Power-B.jpg


Yaani, WAZIBA maji, by 2014 walikuwa "wanazalisha" 562 MW, lakini wale waliodhibiti uzibaji wa maji wakawa "wanazalisha" 573.7 MW by 2019... yaani kukiwa na ongezeko la 11.7 MW kwa miaka 5?!

Halafu naona kama napoteza muda wangu tu kwa sababu, mtu kama wewe mwanzoni kabisa umesema data zangu ni za kitapeli, kwa sababu unataka tutumie reference za maelezo ya wanasiasa!!!!

Hivi hata huo umeme wa gas ulioongezeka from 501 MW in 2014 to 892.72 in 2019, ikiwa ni ongezeko la 391.72!! Je, hapo kwenye ongezeko la 391.72 MW za umeme wa gas, ukitoa zile 150 MW za Kinyerezi I, na 240MW za Kinyerezi II, Je Timu ya Wasio Wapigaji na Watengeneza Mgao wanakuwa wamefanya installation ya MW ngapi?

waliokuwa wanatengeneza tatizo kwa kuziba maji kama ambavyo alidai Magu, ndo hao hao wamezalisha umeme mwingi zaidi wa maji kwa kipindi cha kutoka 2010 hadi 2014 kuliko umeme uliozalishwa from 1980 to 2000 na wakati wao hawakuwa watengeneza matatizo?

Labda hapa nirudie tena...

Ukitoa umeme wa maji ambao tumerithi, huku Mkapa akichangia Kihansi, 57% ya umeme WOTE ambao unatokana na gesi, hiyo ni kazi iliyoanzia 2008 hadi 2014!!

Of course, Ubungo I ilijengwa na Mkapa lakini tulikuwa tunatumia mafuta. Tumeanza kutumia gesi Ubungo I mwaka 2008!! Ubungo II mwaka 2012, Kinyerezi I mwaka 2015, Kinyerezi II, ujenzi ulianza 2016 lakini taratibu zote zilikamilika by 2015!!!

Sasa hao ambao SIO WEZI wamezalisha umeme upi?!
Magufuli amekuja akatumia umeme ule ule uliokuwepo wakati wa JK, na hapakuwepo na mgao wa umeme wa hovyo kama uliokuwepo wakati wa JK.
Duh!!

Hivi huwa mnasoma kwa haraka haraka au tatizo ni kuelewa?!

NImekuambia wazi kwamba, JPM alipata advantage ya kukuta pool ya 390 MW za ambazo jitihada zilifanyika wakati wa KIkwete lakini umeme wake ukaja kutumika wakati wa JPM!! Hizo units 390 za ziada alizokuja ku-enjoy JPM, Mzee wa Msoga alifanya kazi ya kuzitengeneza tu lakini hazikutumika wakati wake!

Kwa maana nyingine, as compared to current status, Utawala wa JK ulikuwa na upungufu wa 390 MW!!

Kwenye umeme 390MW ni nyingi sana hizo kwa sababu, kwa Tanzania hii huo umeme unaweza kutumiwa na MIKOA YOTE excluding Dar es salaam!!!

Dar es salaam ndie Jini Mnyonya Umeme huku ikitumia takribani 25% ya UMEME WOTE unaozalishwa!!
Leo Samia ameshika hatamu, amechukua na baashi ya watendaji wenye vinasaba vya wizi waliokuwepo enzi za JK, mambo ya mgao yamesharudi after only 8 months alizokuwepo ikulu.
Nilichogundua tatizo lako wewe ni Kikwete, and nothing else vinginevyo sioni mantiki ya kusema Samia kawarudisha watu wa Kikwete!!

Na hizi kelele zipo sana baada ya kuteuliwa January Makamba ambae hata hivyo, wakati wa JK alikuwa just NAIBU WAZIRI!

Sasa kwanini uone Makamba aliyerudishwa ni wa enzi za KIkwete na sio wa enzi za Magufuli?!

Unaweza kunitajia waziri MMOJA TU aliyekuwa nishati or any related ministry wakati wa JK na sasa Samia amemrudisha kwa title ya "waliokuwepo enzi za Kikwete?

Matokeo yake, nami umeniamisha kwenye hoja za msingi najikuta namjadili Kikwete!!!

Lakini bado nakukumbusha, UMEME WOTE WA GESI umeletwa na huyo uliye na matatizo nae!!!
Ndio maana nakwambia simple logic inaondoa maana yote ya huu utitiri wa namba zako ulizotuwekea hapa, hayo manamba yote yanaweza kugeuzwa vyovyote ilimradi wezi wapate sababu ya kutupiga, nani atawaamini?

Habari ya kutangazwa bungeni sijui wapi ufisadi hiyo haina maana, umeme ukikatika kila mara kila mtu atajionea popote alipo, hakuna sababu ya kuleta story mpya hapa.
Hakuna logic yoyote unayotumia...

Na kwanini utumie logic kwa suala lenye takwimu?!

Nimekuuliza maswali simple sana... NAOMBA UNIJIBU manake kila ninachokuuliza, unakwepa kujibu na kukimbilia "ukitumia logic"

Man...

1. Je, kiangazi na ukame ni kitu kile kile?
2. Je, unakataa hakuna upungufu wa maji?

Mbona maswali yapo straight forward?! Kwanini huyajibu?! Au hayo hayahitaji logic?
 
Umeanza siasa,

Na umejibu kijuu juu mno.
Hili ni suala la kitaalamu inabidi lijadiliwe kitaalamu...

Ni uswahili tu upo hapa, we hujui umuhimu wa hizo taarifa kwenye huu mjadala kweli?

Kwa hizo data kuwekwa bayana tutafahamu ni uzembe au kuna kinachoendelea nyuma ya pazia.
We jamaa mtu wa ajabu sana...

Yaani pamoja na kukutajia source bado unataka mimi ndo nikasome ripoti yooooote, kisha nije kukuandikia hapa?!

Hivi nini maana ya kuandika reference?!

Kama umefika elimu ya chuo, hivi huko mlikuwa mnanukuu kitabu kizima, au unachukua sehemu tu na kuweka source?
Nimekuuliza unaanza kusema nauliza maswali ili nifanye league, haya bwana, siwezi kujadili chochote na wewe, umekaa mkao wa kutetea uozo unaondelea na kwa hilo siwezi kubadili chochote.
Hebu angalia maswali yako ambayo sikukujibu...
Naomba kufahamu ni mashine models zipi, gharama yake ya ununuzi.

Naomba kufahamu hivyo vifaa vinavyobadilishwa ni vipi, na vina gharama ipi?

Naomba kufahamu pia zinatumia gas kiasi gani per day.

Naomba kufahamu pia gharama ya maintenance inakuwaje.

Kwa kunijibu haya, tunaweza kujadili mambo kitaalamu na tuache blah blah blah, data mnazotoa nikisema ni mfu nakuwa sikosei.
Kama jibu huna basi ni uswahili tu unaendelea humu...
Hivi hayo ni maswali ya kuuliza kwenye mijadala kama hii? Are you serious?

Isitoshe, ni wewe ndie umesema nimekuja na data za uongo...
Mnakuja na data zenu za uongo na kweli mnaunga unga upuuzi tu, wananchi wanataka umeme sio siasa.
NImekuambia leta wewe basi hizo data za kweli, umeshindwa na matokeo yake unataka nikuletee bei ya nini na sijui, mara model number... like serious?!
 
Tatizo la umeme litapungua kwa kiasi kikubwa ONLY IF one or the combination of the 2 happens:-

1. Endapo Kinyerezi III na IV itajengwa na hivyo kuongeza kiwango cha umeme kwenye national grid, and/or
2. Bwawa la Nyerere litakamilika na kuanza kuingiza umeme kwenye grid ya taifa!

Kinyume na hapo, upungufu utaendelea kuwepo kwa sababu kila siku wateja wapya wanazaliwa, na matumizi yanaongezeka!! Sasa haiwezekani kila siku wateja wapya wanazaliwa, na kiwango cha umeme kinabaki kile kile halafu tutarajie tatizo la upungufu wa umeme litaisha!!
Bwawa la Nyerere maji watayatoa wapi na huu ukame?
 
Chief usiwasikilize hawa,hizi ni propaganda tu za kuwasha mitambo ya emergency ya akina Symbion na IPTL ili upigaji wa raslimali za taifa uendelee,time will tell
Unatufanya sote ni mapimbi siyo? Kaa ukijua kwamba tuna ndugu, rafiki na majirani ambao wanafanya kazi huko kwenye hiyo mitambo na wanatuambia hali halisi.
 
Mmmh, upungufu wa maji umesababishwa na nini?! Ukweli una tabia ya kuumiza. Magufuli alikuwa ni tapeli mwenye roho mbaya, hawa wa sasa ni matapeli wenye tabia za ujanja ujanja.
Kwa hiyo Magufuli roho mbaya yake ilikuwa inasababisha maji na umeme visikatike?
 
Umeanza siasa,

Na umejibu kijuu juu mno.
Hili ni suala la kitaalamu inabidi lijadiliwe kitaalamu...

Ni uswahili tu upo hapa, we hujui umuhimu wa hizo taarifa kwenye huu mjadala kweli?

Kwa hizo data kuwekwa bayana tutafahamu ni uzembe au kuna kinachoendelea nyuma ya pazia.
Nimekuuliza unaanza kusema nauliza maswali ili nifanye league, haya bwana, siwezi kujadili chochote na wewe, umekaa mkao wa kutetea uozo unaondelea na kwa hilo siwezi kubadili chochote.
Acha kupayuka pauyuka weka data zako za kweli.

Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app
 
Wanasoma basi hawa wajane wa mwendazake.

Wao wanachojua enzi za magu umeme haujawahi kukatika wala kuwa na mgao.

Kwa sababu magu alikuwa kiongozi 'kweri kweri'

Hapa tunawakea ushaihidi kwamba hata wakati wa magu mambo yalikuwa kama ya sasa wanaanza kubadili gia angani.

Hata Juzi niliwawekea thread kibao za matatizo ya umeme enzi za magu ili kweka records sawa maana walikuwa wanasema kipindi cha magu umeme ulikuwa haukatiki wala hakukuwa na mgao.

Nakumbuka kipindi cha magu Gridi ya taifa ilikata....Kwa nature ya miundombinu yetu ilivyo haiwezekani umeme usikatike,ngizo zimepita kwenye chemchem,nyanya zimepita kwenye miti,wezi wa mafuta ya transformer ,wezi wa nyanya za umeme,vitu hivyo vinasababisha kukatika kwa umeme sometimes.
 
Kwa hiyo Magufuli roho mbaya yake ilikuwa inasababisha maji na umeme visikatike?

kipindi cha magu nani alikwambia kwamba maji na umeme vilikuwa havikatiki? Search thread humu watu wakilalamika migao ya maji na umeme kipindi cha JIWE...sema nyie Push Gang mnatafuta pa kujifichia.....Legacy inajitetea yenyewe haitetewei(Nape).

Iundwe tume ya kuchunguza madeni ya miaka mi5 nyuma yametumikaje -Nape.

Acha bla bla wananchi wanataka maji na umeme - Wilson Mahera.
 
Hata Juzi niliwawekea thread kibao za matatizo ya umeme enzi za magu ili kweka records sawa maana walikuwa wanasema kipindi cha magu umeme ulikuwa haukatiki wala hakukuwa na mgao.

Nakumbuka kipindi cha magu Gridi ya taifa ilikata....Kwa nature ya miundombinu yetu ilivyo haiwezekani umeme usikatike,ngizo zimepita kwenye chemchem,nyanya zimepita kwenye miti,wezi wa mafuta ya transformer ,wezi wa nyanya za umeme,vitu hivyo vinasababisha kukatika kwa umeme sometimes.
Ilifikia hatua hii?
 
Ilifikia hatua hii?

Hatua gani mkuu? Huku kwetu Tanesco wanatoa taarifa siku 3 kabla kwamba watakata umeme kwa ajili ya kuweka nguzo za zege ila kama ikitokea umekatika basi ni fault ambayo ni out of control labda nguzo kukatika au transfomer kubutuka etc ambayo within 2hrs inakuwa imetatuliwa.

tatizo kubwa la TANESCO ni delay katika kuwaunganisha wateja wapya.
 
Hatua gani mkuu? Huku kwetu Tanesco wanatoa taarifa siku 3 kabla kwamba watakata umeme kwa ajili ya kuweka nguzo za zege ila kama ikitokea umekatika basi ni fault ambayo ni out of control labda nguzo kukatika au transfomer kubutuka etc ambayo within 2hrs inakuwa imetatuliwa.

tatizo kubwa la TANESCO ni delay katika kuwaunganisha wateja wapya.
Aha! .. Basi sawa mkuu.
 
Baada ya maelezo yako marefu, je wanatuhakikishia kuwa kwa vile sasa wanaweza kufanya matengenezo inavyotakiwa Tanzania haitakuwa na tatizo la upungufu wa nishati ya umeme? Je, matengenezo ya muda na kiasi gani yataondoa tatizo la mgao?
Yaan sasa hivi kila mtu anajifanya mtaalamu wa umeme na kutoa uchambuzi wa kukosoa umeme wa maji hasa bwawa la Nyerere na kupigia chapuo gesi huku wakisahau kuwa gesi tulikuwa nayo miaka mingi tu sijui wakina songasi lakini shida ya umeme ilikuwepo.

Pia wanasahau kuwa umeme wa maji ndio umeme wa kuaminika maana ni renewable energy ukilinganisha na gesi ambayo ni non renewable, pia umeme wa maji ni rafiki wa mazingira kulinganisha na vyanzo vingine vya umeme.

Ninavyoelewa mimi kwa plan ya JPM bwawa lingekamilika 2022 hivyo 2115MW singeingia kweny grid ya taifa jumlisha 80MW za Rusumo huko Ngara, umeme huu ni karibu mara mbili ya umeme wote tulio nao sasa ambao ni takribani 1650MW, hivyo tatizo la umeme lingekwisha mwakani.
 
Maneno ya mkosaji, njia rahisi ya kujitetea ni kutupia lawama wengine.

Moja ya ‘case law’ inayotumika sana duniani ni ‘Caparo industries v Dickinson’ mlalamikaji anadai alinunua kampuni kwa sababu auditor aliridhia hesabu za hiyo biashara.

This is why private auditing firm nyingi zimesajaliwa ‘limited liability company’ (LLC) na baada ya audit report kuna ‘disclaimer’. Neno la CAG linaanza kuwa sacred nchii, wakati not much is done to scrutinise the merit of final opinion.

Jamaa baada ya kununua akakuta hesabu zenyewe ni overstated na biashara ina hasara, kwanini asimfungulie case auditor; jibu ni kwamba an audit is just an opinion.

Jukumu la kupanga sera za umeme ni serikali sio auditor (internal audit) ni mapendekezo tu. Moreover mtu analeta vipande tu, vipi auditor aliongea na mkonge wa taifa kupata maelezo yao inawezekana watu wanataka kufanya matengenezo kwenye kipindi ambacho source moja haba.

To cut the story short utetezi wa hawa mafisadi una make sense kwao wenyewe and the gullibles mtu mwenye akili zake timamu awezi kumeza hoja za kitoto hivi.
 
Back
Top Bottom