Tazama hii simple logic;
Wakati wa JK mgao wa umeme ulikuwepo, na ulikuwa wa kutengeneza ndio maana zikazaliwa Richmond na madudu mengine.
Upo sahihi kabisa, manake hata Magufuli alisema Wapiga Deal huwa wanaziba maji kutengeneza mgao ili wauze majenereta!!
Hizo ndo hoja zenu, kwa sababu kama nilivyokueleza hapo mwanzo, source yenu ni Wanasiasa!!!
Turudi kwenye Ripoti za Kitalaamu...
Sasa how come, wale wale waliokuwa wanatengeneza mgao kwa kuziba maji, Ripoti ya JICA inaonesha ndio wamezalisha umeme mwingi zaidi wa maji kuliko wale ambao walikuwa hawazibi maji?
Turudi kwenye Ripoti ya Wizara ya Nishati ya mwaka 2016
Ripoti inaonesha watengeneza mgao kwa KUZIBA MAJI, by 2014 walikuwa na installed capacity of 562 MW kwa upande wa wa umeme wa maji!!
Hali ilikuaje baada ya kuingia JPM ambae aliwatia adabu wale waliokuwa wanaziba maji?! Ripoti nyingine ya Wizara ya Nishati inasema:-
Yaani, WAZIBA maji, by 2014 walikuwa "wanazalisha" 562 MW, lakini wale waliodhibiti uzibaji wa maji wakawa "wanazalisha" 573.7 MW by 2019... yaani kukiwa na ongezeko la 11.7 MW kwa miaka 5?!
Halafu naona kama napoteza muda wangu tu kwa sababu, mtu kama wewe mwanzoni kabisa umesema data zangu ni za kitapeli, kwa sababu unataka tutumie reference za maelezo ya wanasiasa!!!!
Hivi hata huo umeme wa gas ulioongezeka from 501 MW in 2014 to 892.72 in 2019, ikiwa ni ongezeko la 391.72!! Je, hapo kwenye ongezeko la 391.72 MW za umeme wa gas, ukitoa zile 150 MW za Kinyerezi I, na 240MW za Kinyerezi II, Je Timu ya Wasio Wapigaji na Watengeneza Mgao wanakuwa wamefanya installation ya MW ngapi?
waliokuwa wanatengeneza tatizo kwa kuziba maji kama ambavyo alidai Magu, ndo hao hao wamezalisha umeme mwingi zaidi wa maji kwa kipindi cha kutoka 2010 hadi 2014 kuliko umeme uliozalishwa from 1980 to 2000 na wakati wao hawakuwa watengeneza matatizo?
Labda hapa nirudie tena...
Ukitoa umeme wa maji ambao tumerithi, huku Mkapa akichangia Kihansi, 57% ya umeme WOTE ambao unatokana na gesi, hiyo ni kazi iliyoanzia 2008 hadi 2014!!
Of course, Ubungo I ilijengwa na Mkapa lakini tulikuwa tunatumia mafuta. Tumeanza kutumia gesi Ubungo I mwaka 2008!! Ubungo II mwaka 2012, Kinyerezi I mwaka 2015, Kinyerezi II, ujenzi ulianza 2016 lakini taratibu zote zilikamilika by 2015!!!
Sasa hao ambao SIO WEZI wamezalisha umeme upi?!
Magufuli amekuja akatumia umeme ule ule uliokuwepo wakati wa JK, na hapakuwepo na mgao wa umeme wa hovyo kama uliokuwepo wakati wa JK.
Duh!!
Hivi huwa mnasoma kwa haraka haraka au tatizo ni kuelewa?!
NImekuambia wazi kwamba, JPM alipata advantage ya kukuta pool ya 390 MW za ambazo jitihada zilifanyika wakati wa KIkwete lakini umeme wake ukaja kutumika wakati wa JPM!! Hizo units 390 za ziada alizokuja ku-enjoy JPM, Mzee wa Msoga alifanya kazi ya kuzitengeneza tu lakini hazikutumika wakati wake!
Kwa maana nyingine, as compared to current status, Utawala wa JK ulikuwa na upungufu wa 390 MW!!
Kwenye umeme 390MW ni nyingi sana hizo kwa sababu, kwa Tanzania hii huo umeme unaweza kutumiwa na MIKOA YOTE excluding Dar es salaam!!!
Dar es salaam ndie Jini Mnyonya Umeme huku ikitumia takribani 25% ya UMEME WOTE unaozalishwa!!
Leo Samia ameshika hatamu, amechukua na baashi ya watendaji wenye vinasaba vya wizi waliokuwepo enzi za JK, mambo ya mgao yamesharudi after only 8 months alizokuwepo ikulu.
Nilichogundua tatizo lako wewe ni Kikwete, and nothing else vinginevyo sioni mantiki ya kusema Samia kawarudisha watu wa Kikwete!!
Na hizi kelele zipo sana baada ya kuteuliwa January Makamba ambae hata hivyo, wakati wa JK alikuwa just NAIBU WAZIRI!
Sasa kwanini uone Makamba aliyerudishwa ni wa enzi za KIkwete na sio wa enzi za Magufuli?!
Unaweza kunitajia waziri MMOJA TU aliyekuwa nishati or any related ministry wakati wa JK na sasa Samia amemrudisha kwa title ya "waliokuwepo enzi za Kikwete?
Matokeo yake, nami umeniamisha kwenye hoja za msingi najikuta namjadili Kikwete!!!
Lakini bado nakukumbusha, UMEME WOTE WA GESI umeletwa na huyo uliye na matatizo nae!!!
Ndio maana nakwambia simple logic inaondoa maana yote ya huu utitiri wa namba zako ulizotuwekea hapa, hayo manamba yote yanaweza kugeuzwa vyovyote ilimradi wezi wapate sababu ya kutupiga, nani atawaamini?
Habari ya kutangazwa bungeni sijui wapi ufisadi hiyo haina maana, umeme ukikatika kila mara kila mtu atajionea popote alipo, hakuna sababu ya kuleta story mpya hapa.
Hakuna logic yoyote unayotumia...
Na kwanini utumie logic kwa suala lenye takwimu?!
Nimekuuliza maswali simple sana... NAOMBA UNIJIBU manake kila ninachokuuliza, unakwepa kujibu na kukimbilia "ukitumia logic"
Man...
1. Je, kiangazi na ukame ni kitu kile kile?
2. Je, unakataa hakuna upungufu wa maji?
Mbona maswali yapo straight forward?! Kwanini huyajibu?! Au hayo hayahitaji logic?